CCM tunaomba kuwekana sawa kwenye hili Jambo

CCM tunaomba kuwekana sawa kwenye hili Jambo

CARIFONIA

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2013
Posts
656
Reaction score
1,604
CCM naomba kuwambia jambo moja makosa na udhaifu wa wanachama wenu mnayajua vizuri, na ni bora mkawawajibisha au kuwafukuza kabisa ili kulinda heshima ya chama chenu mapema, kabla wao hawajaamua kufunguka mabaya yanayoendelea ndani ya chama chenu.

Yahani ni mara mia mkaa kimya kuliko kuwajibu wa kina Polepole, Gwajima na Mpina mnasubiri mpaka waje waanike mabaya yenu public ndio nanyie mnakuja kuwajibu kwa kuibua mabaya yao walifanya nyuma, kwanini hamkuwachukulia hatua kama mlijua wanamakosa.
Au kwenye chama chenu mnalindana? Mnasubiri mpaka mtu atoe malalamiko yake ndio na nyie mje kutuletea makosa yake huu ni upuuzi wa hali ya juu.

Sisi tutamuamini yule wa kwanza kumsema mwenzake sababu kama mlijua ana makosa na mkamchukulia poa sababu mnalindana ni bora mkakaa kimya kwani sisi hatutwaamini tena.

Na kama kuna wakina Polepole wengine ni bora mkawawajibisha mapema msisubiri mpaka wakaja public kutoa mabaya yenu na nyie ndio mje na brabra kibao.
Ni hayo tu nadhani tumeelewana
 
Ni mwendo wa kuviziana. Hawawagus ss, ngoja uchaguzi uishe. Ile enzi za Magu itakua cha mtoto, vyuma vitakaza kazana. Akipita huyu bb
 
Back
Top Bottom