CCM Tunajipanga kwa Mapambano 2015

CCM Tunajipanga kwa Mapambano 2015

Taarifa kwa WanaJF mlizoea kusema vibaya dhidi ya CCM wakati huo mkiwapa misifa CDM;

CCM kama chama mama nchini mwetu tunaendesha mambo yetu kisayansi kwa kukaa chini na kutafakari kupitia vikao vya ndani ambavyo havihitaji kuandikwa kwenye magazeti. Ikumbukwe huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama ikiwa lengo kuu la uchaguzi ni kuwachuja makapi na kupanga timu ya USHINDI kuelekea 2015.

Wapenzi na wakereketwa wa CCM mkae mkao wa KULA PWEZA ili kucharge nguvu, tupate mvurumisha CDM na vyama vyote vya upinzani.

Msije kuumiza vichwa kutokana na ziara zisizo na tija zinazofanywa na askari uchwara wa CDM huku mikoani, hizo ziara zimepangwa kwa nia ya kuboresha mifuko ya viongozi wao kwa kulipana posho tu. Hizo mbinu za kufungua matawi papo kwa hapo pasipo uchambuzi yakinifu zimepitwa na wakati. Haingii akilini leo hii kwenda kijijini Mtwara kumuuzia mwanakijiji sera ya chama na siku hiyohiyo kufungua tawi!!!!!!!

Kidumu chama cha mapinduzi na sera zake za kuwapa nuru watanzania.

Science ipi? ya kienyeji, kwani nanihii kesharudi? Hamna usayansi wowte mtakaoweza kufanya katika miaka hii miwili. Labda tu mazoezi ili msife kabisa 2015.
 
Kuahirisha uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni sehemu ya mkakati wa kujipanga upya. CCM ni jabari lina mbinu nyingi za kujihami na kujiokoa toka katika lindi la changamoto. Ni kweli tupo katika kipindi kigumu ambacho BUSARA na UZOEFU wa mapambano unatusaidia kukwepa dhoruba za CDM hatahivyo mwisho tutashinda

Mkuu mwanachama mwenzangu wa ccm labda mbinu tunayotakiwa kufanya nikujipanga KUIBA TUU hasa vijijini kama kawaida yetu, Ila kwa kusubiri ushindi wa wananchi ni ngumu saana!
 
Mkuu mwanachama mwenzangu wa ccm labda mbinu tunayotakiwa kufanya nikujipanga KUIBA TUU hasa vijijini kama kawaida yetu, Ila kwa kusubiri ushindi wa wananchi ni ngumu saana!
hahaha,nachukia rangi ya kijani,nikiona mtu kavaa kijani nahisi ni mwizi au jambazi.duuh.
 
Taarifa kwa WanaJF mlizoea kusema vibaya dhidi ya CCM wakati huo mkiwapa misifa CDM;

CCM kama chama mama nchini mwetu tunaendesha mambo yetu kisayansi kwa kukaa chini na kutafakari kupitia vikao vya ndani ambavyo havihitaji kuandikwa kwenye magazeti. Ikumbukwe huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama ikiwa lengo kuu la uchaguzi ni kuwachuja makapi na kupanga timu ya USHINDI kuelekea 2015.

Wapenzi na wakereketwa wa CCM mkae mkao wa KULA PWEZA ili kucharge nguvu, tupate mvurumisha CDM na vyama vyote vya upinzani.

Msije kuumiza vichwa kutokana na ziara zisizo na tija zinazofanywa na askari uchwara wa CDM huku mikoani, hizo ziara zimepangwa kwa nia ya kuboresha mifuko ya viongozi wao kwa kulipana posho tu. Hizo mbinu za kufungua matawi papo kwa hapo pasipo uchambuzi yakinifu zimepitwa na wakati. Haingii akilini leo hii kwenda kijijini Mtwara kumuuzia mwanakijiji sera ya chama na siku hiyohiyo kufungua tawi!!!!!!!

Kidumu chama cha mapinduzi na sera zake za kuwapa nuru watanzania.

Hata mgonjwa alie mahututi haamini Kama atakufa mara nyingi anajipa matumaini ya kupona,ccm hamponi.
 
Wananchi wameanza kurudisha imani kutokana na:

1. Kuwatosa mawaziri ambao ni wakala wa ufisadi
2. Iddi Simba kapelekwa Kisutu

Pia tunafanya mchakato wa watoa siri nyeti ndani ya serikali na wakala wote wa CDM tunapiga chini

Wapi study au survey mliyofanya ikawapa hizo data kuwa mmerudisha imani?au ndiyo yale mambo ya wanachama 6mil since 77
 
hahaha,nachukia rangi ya kijani,nikiona mtu kavaa kijani nahisi ni mwizi au jambazi.duuh.

daa tunakazi kweli sisi ccm jamani tunaweza kupambana ndani msikimbie chama cha ukombozi ni wachache akina JK ndo wameharibu chama chetu wakuu!
 
KWA MKAKATI WETU WA M4C KUENDELEA KUVUKA MALENGO YA KUKAMATA VIJIJI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 80 % KOTE NCHINI, CHADEMA KUWA 'CHAMA CHENYE WABUNGE WENGI KULIKO CHAMA CHOCHOTE NCHINI' HATA KABLA YA 2015

Wakuu wanaharakati wenzangu,

Naomba ieleweke kwamba siku zote katika siasa, MKAKATI NI WATU kuwa upande wako na wala si DOLA MIKONONI. Naona CDM tunaendelea vema sana na mikakati yetu chini ya M4C hadi hivi sasa kutafuta maana halisi kwetu ya kaulimbiu ya NGUVU YA UMMA kila kona ya nchi hii.

Naam, nasema hivi naona CHADEMA hivi sasa kweli tumeshaelewana somo na fomula vema. Kwa mtindo huo wala hatuhitaji kumwambia Mbunge yeyote alioko huko CCM kwamba akahamie CDM maana kama ni urefu wa kamba kila mmoja keshapimishiwa kisawa sawa huko majimboni mwao na mwelekeo wa upepo wa kisiasa wananchi tayari wameshautoa mchana kweupe.

Mwenye kuchagua kwenda kinyume na matakwa ya wananchi hadi hivi sasa kwenye ushiriki wao kule bungeni Dodoma shauri yakeee!!!!!!!

Kwa tafsiri nyepesi tu, ukweli mambo ni kwamba CHADEMA tukiendeleza mkakati huu vema kukamata uongozi mashinani kwa zaidi ya asilimia 80 % maana yake ni kwamba chama chetu ndicho kitakachokua na VITI VINGI ZAIDI BUNGENI KULIKO CHAMA CHOCHOTE KILE NCHINI.

Nasema hivo kwa maana kwamba hadi hapo ni ukweli usiofichika kwamba kisiasa sasa 'UWEZO TUNAO' hivi sasa kuwaelekeza wabunge zaidi ya 200, nje ya wale wa ndani ya chama chetu, kupitia nguvu ya umma tulionayo majimboni kwao hivi sasa ili wakaseme nini pale mjengoni Dodoma kwa faida ya wananchi kupitia CDM na wala si CCM.

Endapo mbunge kama huyu ambaye jimbo lake tayari tumelishika kwa zaidi ya asilimia 80 % atakataa kutii maelekezo ya Nguvu ya Umma wala lawama hazitotuangukia tena maana atakua amejichagulia mwenyewe KUJILISHA KIPANDE CHA WEMBE KISIASA kwa kwenda kinyume na maelekezo ya wapiga kura.

Mahesabu yetu kupitia M4C hivi sasa ni kama hisabati ya 1 + 1 = 11 na ni vema sana. Wao wana mtandao wa Ma-DC karibia 150 hivi kote nchini na sisi tunao mtandao wa wapiga kura wa leo na wa kesho karibia milioni 26 hivi kote nchini.

Hiyo 'Nguvu ya Umma' tukishaipata kwa zaidi ya asilimia 80 %, ndio tutakayoitumia kwa malengo mazito zaidi ikiwa ni pamoja na:

(1) kuandika na kupitisha KATIBA MPYA YA WANANCHI;

(2) KUWEKA NAYO SERIKALI MPYA BILA UCHAKACHUZI MADARAKANI; na vile vile

(3) kulinda nayo rasilmali za nchi ili ziweze kuneemesha WaTanzania kwa ujumla wetu Bara na Visiwani bila ubaguzi wala 'familia teule' kuendelea kuhodhi kila kitu kwa simanzi ya walalahoi kote nchini.

Utaifa mbeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeele kama taifa; CDM Nguvu ya Umma!!!!!!!!!!!

Katika uchaguzi wa uliofanyika Katika kata mbalimbali za Chato, Magamba wamepigwa mweleka na CDM maana hata vijijini CCM haitakiwi.

VIJIJI ILIVYOSHINDA CHADEMA NI:-
1. Mjengo kata ya Mganza
2. Kazunguti Kata ya Nyamilembe
3. Mikonto Kata ya Nyamilembe
4. Izubangabo Kata ya Bwanga.
5. Majengo Kata y aBuziku
6. Kasala Kata ya Makuluguzi
7. Mwenda Kulima kata ya Ipalamasa
8. Nyakakalango kata ya Nyamilembe

CCM ni mkungo kata ya Bukome, Mwabasabi kata ya Ipalamasa, Mnekezi kata ya Ipalamasa

Mchakato wa M4C unaendelea kata hadi kata. Wilaya ya Chato ina kata ishirini na mbili (22) katika hizi tumezunguka kata kumi na nane na kila kata ambazo tumepita ukiitishwa uchaguzi leo kata hizo (CCM) wataambulia moja au hamna bahati nzuri umeshuhudia(Mimi Tamuganyizi nilishuhudia) M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato(CCM) akilalamika mafuriko wanayoyapata na tarehe 1/6/2012 tunaenda kata ya Bwera siku ya ijumaa.

Hii oparesheni bomoa makufuri ni kimbuga cha 2015 kuchukua Halmashauri.

Matokeo ya mIkutano yetu kila tulipopita hakuna mkutano tulipiTa bila kuvua gamba na kuvaa gwanda jumla ya magamba 66 yamevuliwa na kuvaa magwanda na wanachama zaidi wamejiunga na chama cha ukombozi(CHADEMA),

Manyanyaso mpaka sasa tuna kesi mahakamani ya M/Kiti wa kijiji cha minkoto pamoja na wenzake wawili walibambikizwa kesi ya kuchoma moto na kuua ngombe za mtuhumiwa wa ujambazi.

Kijiji anamotoka M/kiti wa halmashauri, na yeye ameshirikiana na polisi kubambikiza kesi ya ujambazi kwa wanachama wetu wawili waliofinikisha tukachukua vitongoji viwili ndani ya kata yake. Bado M/Kiti wetu kijiji cha Kibumba kata ya Makurugusi na
yeye alibambikizwa kesi ya mauaji mpaka sasa yuko mahabusu Bihalamulo.

CHANGAMOTO

Vifaa vya chama kama Bendera, Kadi na Katiba hatuna kabisa lakini tuliadika barua makao makuu pamoja na mkoa tumeelezwa kuwa bado vifaa haijaja kutoka vilipoagizwa.

My Take

Haya ni mahojiano niliyoyafanya na Katibu wa CDM wilaya ya Chato. Jamaa yuko simple ni kijana yuko Stendi pale Chato. Storage ya nyaraka muhimu alizonazo sio nzuri. Binafsi naandaa walau storage ya Hard Copies alizonazo kijana kwa kuanzia na baadaye ufumbuzi kamili. Leo CDM inaharibu kule Kata ya Bwera…nitawapa update.

Kwenye Kibanda cha kazi anapopigia kazi Kamanda huyo ametype na kuprint maandishi yasomayo hivi….." VUA GAMBA VAA GWANDA, VUA UKADA UVAE UKAMANDA"

Katibu huyo anaitwa Mange Sayi Ludongo – Wasiliana naye kwa update zaidi….0752911438

S.L.P 15,
CHATO.

Mafilili wasiwasi wako unaleta picha halisi ya kihoro kilichopo huko magamba!

Hii M4C, Haina huruma!
 
Taarifa kwa WanaJF mlizoea kusema vibaya dhidi ya CCM wakati huo mkiwapa misifa CDM;CCM kama chama mama nchini mwetu tunaendesha mambo yetu kisayansi kwa kukaa chini na kutafakari kupitia vikao vya ndani ambavyo havihitaji kuandikwa kwenye magazeti. Ikumbukwe huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama ikiwa lengo kuu la uchaguzi ni kuwachuja makapi na kupanga timu ya USHINDI kuelekea 2015.Wapenzi na wakereketwa wa CCM mkae mkao wa KULA PWEZA ili kucharge nguvu, tupate mvurumisha CDM na vyama vyote vya upinzani. Msije kuumiza vichwa kutokana na ziara zisizo na tija zinazofanywa na askari uchwara wa CDM huku mikoani, hizo ziara zimepangwa kwa nia ya kuboresha mifuko ya viongozi wao kwa kulipana posho tu. Hizo mbinu za kufungua matawi papo kwa hapo pasipo uchambuzi yakinifu zimepitwa na wakati. Haingii akilini leo hii kwenda kijijini Mtwara kumuuzia mwanakijiji sera ya chama na siku hiyohiyo kufungua tawi!!!!!!!Kidumu chama cha mapinduzi na sera zake za kuwapa nuru watanzania.
Toka mmeanza kufanya hiyo mikutano ya siri imetusaidia nini? mara nyingi mikutano yenu ya siri ni kuwaonya wanaonda kinyume na mafisadi, tuamini vipi leo mna mikakati tofauti na tulioizoea?
 
CCM pamoja na ushetani wote huu bado tu mnataka kuitawala Tanzania?
mauaji.jpg
 
ni kwelimkabosa ccm mmejipanga kwa mapambano 2015.kwani uongo/wewe unafikiri sitta na lowasa wanaweza kukaa bila kupambana by 2015?hivi ni kweli kuwa membe atanyamaza kuona lowasa anapitishwa kuwa mgombea urais?hivi inawezekana mwakyembe akapona kweli kama lowassa atapitishwa kuwa mgombea urais?hapo hakuna namna isipokuwa mapambano makali baina ya makada wa ccm.
 
Wananchi wameanza kurudisha imani kutokana na:

1. Kuwatosa mawaziri ambao ni wakala wa ufisadi
2. Iddi Simba kapelekwa Kisutu

Pia tunafanya mchakato wa watoa siri nyeti ndani ya serikali na wakala wote wa CDM tunapiga chini

ili muibe?
 
Wananchi wameanza kurudisha imani kutokana na:

1. Kuwatosa mawaziri ambao ni wakala wa ufisadi
2. Iddi Simba kapelekwa Kisutu

Pia tunafanya mchakato wa watoa siri nyeti ndani ya serikali na wakala wote wa CDM tunapiga chini

Anzeni na Nape kwanza kisha mfate yule wa Magogoni,hapo kidogo mtawavuta watu.
 
Ikumbukwe huu ni mwaka wa uchaguzi ndani ya chama ikiwa lengo kuu la uchaguzi ni kuwachuja makapi na kupanga timu ya USHINDI kuelekea 2015.
Juzi hapa hapa JF niliona thread kuwa mmemchagua marehemu kama kiongozi wa kijiji...kama ndiyo sanyansi zenyewe basi chadema hazitufai..............
 
Wananchi wameanza kurudisha imani kutokana na:

1. Kuwatosa mawaziri ambao ni wakala wa ufisadi
2. Iddi Simba kapelekwa Kisutu

Pia tunafanya mchakato wa watoa siri nyeti ndani ya serikali na wakala wote wa CDM tunapiga chini
Kwa jinsi CCM ilivyo chafuka na jinsi watanzania walivyo washitukia hata mkileta mtto mchanga ambae hana makosa yoyote hachaguliki ili dhana tu kuwa huyu ni mtoto wa ccm basi kasha kosa kura yangu.....
 
Hadi kufika hiyo 2015 ni watanzania wachache sana watakaokuwa wanakumbuka kitu inaitwa CCM, hasa ukizingatia kuwa washabiki wenu wengi ni wazee na wazee wa kitanzania wanapoteza sana kumbukumbu kwa sababu ya msongo wa mawazo unaotokana na pensheni kidogo mnazowapa. Nawashauri mjikaze kiume mwende kujitetea kwa wananchi ili angalau mpate wabunge wachache muwe wapinzani wenye nguvu.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
dah hyo picha ya mwenyekit we2 imenikumbusha machungu, one day yes coz haya mambo yanamwisho.
 
Laiti ungejua tunavyoichukia ccm ivi una habari ccm imeshauza hii nchi na wewe pia umeuziwa humo ndani pole zako!
 
2Q==
Mapambano yapi? Ya kuendeleza mauaji?? Ama kweli CCM hamna aibu!!
 
Back
Top Bottom