CCM tuhubiri na Haki sio Amani tu

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,842
Ukimsikiliza kila kiongozi ndani ya chama chetu cha CCM kuanzia kwa mgombea wetu John Pombe Magufuli na wengine wote hakuna anayetamani kugusia neno Haki katika mikutano yao kila mmoja anahubiri Amani tu, hii si sahihi.

Amani ni zao la HAKI, hebu tuichambue kauli hii au sentensi hii kwa undani kwa muktadha wa uchaguzi

Kila mgombea kuanzia udiwani, ubunge na Urais kutoka vyama vyote angependa atendewe haki katika uchaguzi huu, haki hiyo inaanzia kuanzia kwenye mikutano ya kampeni inayoendelea, kuapisha mawakala, kutoa barua za utambulisho kwa mawakala wa vyama vyote, kutoa fomu ya matokeo kwa mawakala wa vyama vyote na kutangaza mshindi aliyeshinda, hii ndiyo haki, Tume au wasimamizi wa uchaguzi wakikiuka haya yote ambayo ni haki kwa mgombea wa nafasi yoyote katika uchaguzi huu watakuwa wanahatarisha Amani ya nchi yetu hivyo, naomba wagombea wote hasa wa Urais na hasa hasa wa chama changu cha CCM ndugu Magufuli asipate ukakasi kutamka hadharani kwamba Tume au wasimamizi wa uchaguzi watende haki ili Amani itamalaki.
 
Back
Top Bottom