CCM tufanye nini Ili Watanzania mnene ya kwamba sasa kweli matunda ya Uhuru tunayaona?

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Inawezekana kila tunalolifanya, hamtuelewi au mnapotoshwa na hivi vyama uchwara na baadhi ya wasaka tonge,mbali ya ilani zetu kedekede ambazo zinazidi kufurika hadi hatuna pa kuziweka, bado tunaona Watanzania wamejawa na shauku ya kama kuna jambo wanalihitajia ili waone tumefikia kule tunakokwenda.

Wewe kama Mtanzania ulie huru tuwekee hapa unaloliona hili likitimizwa na Serikali yetu adhwimu inayoongozwa na Raisi Mlezi mama Samia Suluhu Hassan basi mambo si mabaya, huko tunakoelekea njia nyeupe na tutanenepeana kwa raha na furaha.

msiwasikilize hawa Wapinga Maendeleo ambao ni wagagagigikoko waliomcheka Bulicheka ambae alivuka bahari kwa meza,CCM imebeba matarajio ya WaTanzania ukilinganisha na wapinzani wanaoishia behind bars kwa kushindwa kuvumilia na wamejawa na tamaa.
 
Unapata faida gani kuipaka rangi chama chakavu?

January aondolewe wizarani kisha mchakato wa katiba mpya uanze haraka na muhakikishe teuzi zote za raisi zinafanywa kuwa kama ubunge tu wananchi ndio wachague nani wanamtaka na kuwe na kura za kutokuwa na imani za kumuondosha anytime akivurunda!

Hii biashara ya raisi anachagulia anaowataka kwa kulipana fadhila huku wananchi tunaumia sio sawa!
 
  • Uhuru wa kujieleza (kujieleza wazi wazi sio kwa kujificha ficha kama humu watu tumejaza fake ID kwa ajiri ya usalama wetu)
  • Uhuru wa mahakama.
  • Uhuru wa kuwawajibisha viongozi wa umma wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.
  • Uhuru na haki ya kufanya shughuri za kisiasa ndani ya nchi pasipo upendeleo.
  • Taifa inatakiwa liwe na plans zake na ziwe ndio kipaumbele namba 1 na sio liendeshe kwa sela za vyama au kiongozi aliopo madarakan hii iwe ni kwa vyama vyote vitakavyo kuwa vimeshika madaraka (nahisi umeona jinsi miradi mingi inavyo kufa pindi serikali inaposhikwa na kiongozi mpya)
  • Uhuru wa vyombo vya habari
  • kutokomeza ufisadi, ubinafsi, udini, ukanda, ukabira, ushikaj, uchawa, uchama linapokuja swala la maendeleo ya nchi.
  • Tuone vitendo vingi kuliko kusikia maneno mengi(hii kwa vyama vyote vitakavyo pata nafasi ya kushika madaraka)
  • Uchaguzi huru na wahaki (sio kufanya uchaguzi ili kukamilisha ratiba)
Ni ayo tu niliyokuwa nafikiria baada ya wenge la usingiz mengine wataongezea wajuzi.
 
Inawezekana kila tunalolifanya ,hamtuelewi au mnapotoshwa na hivi vyama uchwara na baadhi ya wasaka tonge,mbali ya ilani zetu kedekede ambazo zinazidi kufurika hadi hatuna pa kuziweka,bado tunaona waTanzania wamejawa na shauku ya kama kuna jambo wanalihitajia ili waone tumefikia kule tunakokwenda.

Wewe kama Mtanzania ulie huru tuwekee hapa unaloliona hili likitimizwa na Serikali yetu adhwimu inayoongozwa na Raisi Mlezi mama Samia Suluhu Hassan basi mambo si mabaya ,huko tunakoelekea njia nyeupe na tutanenepeana kwa raha na furaha.

msiwasikilize hawa Wapinga Maendeleo ambao ni wagagagigikoko waliomcheka Bulicheka ambae alivuka bahari kwa meza,CCM imebeba matarajio ya WaTanzania ukilinganisha na wapinzani wanaoishia behind bars kwa kushindwa kuvumilia na wamejawa na tamaa.
Katiba mpya, tume huru ya uchaguzi, uhuru wa habari, uwanja sawa was siasa, mvunje magenge ya wasiojilokana yanayonyanyasa na kubambikoa raia wasio na hatia🤔.
 
hatuwezi kuishi kama tupo Peponi,hilo haliwezekani ni lazima ulinzi na usalama uwepo na hata hayo magenge ni lazima yawepo alimuradi yapo chini ya serikali na vyombo vyake,Ni na ndio maana hadi leo Tanzania imebaki kuwa nchi salama,hata uweke chandarua vipi mbu watakuwepo ila hawatosumbua sana,na ndipo Tz ilipo kiusalama na faida inaletwa na hayo magenge mnayoyapiga vita.mshukuru sana vitengo hivyo vinafanya kazi usiku na mchana ,ili kuiweka nchi salama. Msione vinaelea huo ni msemo ulio wazi.
 
Human being are so complicated,Kwa Africa Tanzania ni ya tatu Kwa uhuru ulioutaja.
Sio kweli, kuna watu wamepotea kwa kuelezea kile wanachokiamini na wengine wamelemazwa. Hakuna nchi ya hovyo kama hii.

Leo hii Tanzania ni moja ya nchi inayofahamika kwa ukiukwaji wa haki za binadamu duniani, kumbuka kuna wengine wamebambikiwa kesi ya uongo. Tanzania ina polisi wenye weledi wa kipekee wa kubambikia watu vyesi feki. Takataka kabisa.
 
Sio kweli, kuna watu wamepotea kwa kuelezea kile wanachokiamini na wengine wamelemazwa. Hakuna nchi ya hovyo kama hii.

Leo hii Tanzania ni moja ya nchi inayofahamika kwa ukiukwaji wa haki za binadamu duniani, kumbuka kuna wengine wamebambikiwa kesi ya uongo. Tanzania ina polisi wenye weledi wa kipekee wa kubambikia watu vyesi feki. Takataka kabisa.
Huyo unamtetea mpaka sauti yake ilirekodiwa,na makapuni ya simu, sawa sijui unatakaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom