CCM Tabora kuingia Igunga ikiwa na majeruhi kibao! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM Tabora kuingia Igunga ikiwa na majeruhi kibao!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanzo, Aug 24, 2011.

 1. M

  Mwanzo Member

  #1
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika dalili zote zinazoonekana kuwa CCM ina hali mbaya kwa uchaguzi mdogo wa Igunga tayari ina makosa mengi ambayo viongozi wa ccm mkoa na taifa watalazimika kujipanga vizuri na makosa hayo ni kama yafuatayo
  1. alipojiuzuru Rostam baadhi ya wana ccm walilia kwa uchungu na wengine kuzimia hapa ccm ikasema waliolilia wote walikodiwa na kupewa fedha ili walie jambo ambalo kama kuna waliolia na hawakupewa fedha wanaona wamedharauliwa na wana hasira.
  2.Mkiti wa CCM mkoa wa Tabora mheshimiwa Hasan wakasuvi katika kikao cha kamati ya siasa mkoa kilichofanyika Igunga alitumia muda mwingi kuwaponda wapambe wa Rostam kwa maneno ya kashfa na mafumbo kibao akisisitiza kuwa watu wa Igunga wana penda wasipende lazima ccm ishinde igunga wanaona nuna watajiju hali iliyopelekea mweka hazina wa ccm Taifa Mh mwigulu kuingilia kati na kumwambia mkiti huyo kuwa lugha anayotumia si nzuri.
  3.siku mbili kabla ya uchaguzi wa kura za maoni zilisambazwa karatasi zenye ujumbe mchafu dhidi ya bwana Abubakar Shabaan ambaye ni mkiti wa halmashauri wilaya ya igunga na bwana Kafumu(Dr) kuwa hawafai kuwa vingozi hata hivyo Dr kafumu ndiye aliyeongoza kura za Maoni Igunga na uwezekano wa kuteuliwa kuwa mgombea wa ccm ni mkubwa sana
  4.Mkiti wa Halmashauri ya wilaya ya Igunga alitaka kuchukua form za kugombea ubunge lakini baadae ccm makao makuu ikamlazimisha asichukue il hali alishaanza kampeni kabla hivyo kumfanya yeye na wapambe wake kuwa na hasira
  5.Kamati ya siasa mkoa wa Tabora imemfukuza kazi katibu wa vijana wa ccm mkoa Tabora bwana Daniel Muhina kwa sababu zinazosemekana za makundi ya kisiasa ya mkoa wa Tabora baadhi wakiwa ni wapambe wa mkiti wa ccm mkoa Tabora na baadhi wakiwa ni wapambe wa mkiti aliyepita.
  tutazidi kufahamishana zadi kwani nipo Igunga kwa kazi maalumu hadi siku ya uchaguzi mkuu
   
 2. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  igunga amkeni msituchagulie mzomeaji bungeni
   
 3. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunaomba utujuze na hali ya vyama vingine, hususan cdm na cuf huko.
  Kwa hali ilivyo, ni kipi chenye ushawishi na mvuto kwa wapigakura?
   
 4. saliel

  saliel Member

  #4
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kazi nzuri kep update
   
 5. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maandamano.
   
 6. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  Hawa tayari imeshakula kwao hilo jimbo wangefanya kulisahau tu kama walivyomsahau aliyekuwa analiongoza mwanzo
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ni kama story ya kitoto lakini hata kama ni mimi nililia siwezi kutoa kura yangu, huku ni kudharauliwa! wakati mwingine najiuliza mji wa igunga ulivyo mdogo, unaenda kuwa national political battle ground, hawa waendesha vita watalala wapi, watakula nini? si ajabu tukasikia watu kulishwa sumu pia!
   
 8. G

  GATZBY Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi hasara kwa mwenye mali na vita vya panzi furaha ya kunguru. Hasira ya Mkizi tijara kwa Mvuvi.
   
 9. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Vip kuhusu mwamko wa Wananchi????..

  IGUNGA AMKENI:CCM wote magamba, wanaotajwa ni mifano ya magamba waliopo CCM
  Igunga take care.
   
Loading...