GE2025 CCM Simiyu yamtupa nje Luhaga Mpina kuwania ubunge jimbo la Kisesa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
DAIMA MSEMA KWELI HANA RAFIKI!!

GIZA NA MWANGA HAVINA URAFIKI HATA WA KINAFIKI!!

Mihemko ya mwenyekiti na kauli tata za vijembe, mipasho na kejeli vilitosha kutuma ujumbe kwa umma na Mpina mwenyewe kukaa kando!!

Siasa za CCM zimejipambanua wazi kuwa ni za kujikomba komba na kujichekesha kwa mwenyekiti na sio siasa za kujenga hoja na kuikosoa serikali.....kujaribu kwenda kinyume ni sawa na kujiondoa kwenye mambo yoyote yenye idhini ya chama!!!
 
Mbunge wa Jimbo la Kisesa anayemaliza muda wake Luhaga Mpina huenda safari yake ya kuwawakilisha wananchi wa Kisesa ikafikia tamati ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu baada ya vikao vya mchujo kwa ngazi ya wilaya ya Meatu na mkoa wake wa Simiyu kumtupa nje ya mbio za kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu; vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya kikao cha kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu vimeitonya Jambo TV.

Mpina Mbunge machachari ndani na nje ya Bunge aliyejipatia umaarufu kwenye takribani miaka mitano sasa kwa kuibana serikali ndani ya Bunge na hata nje ya Bunge kwa hoja mbalimbali amekumbana na rungu la chama chake ngazi ya wilaya na mkoa baada ya vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Meatu kumtupa nje kwa kutopendekeza jina lake- maamuzi ambayo yamebarikiwa na chama ngazi ya mkoa hivyo sasa nafasi ya mwisho ya yeye kupenya jina lake kwa ajili ya kwenda kwenye mchakato wa kura za maoni ikibakia vikao vya ngazi ya taifa kwa maana ya Kamati Kuu ambayo imepewa mamlaka ya kufanya uteuzi wa mwisho.

Katika jimbo hilo, wagombea waliokuwa wakichuana katika hatua ya awali walifikia 14, lakini kupitia kikao cha wilaya na mkoa, majina yaliyopendekezwa ni Sitta Risinge, Mussa Mbuga, na Silinde Gumada.

Kiujumla, majina yote yaliyopendekezwa ngazi ya wilaya na mkoa hupelekwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, na Kamati kuu hiyo ina uwezo wa kuja na mapendekezo yake ya majina kwa kurejea majina ya awali ya wote waliochukua fomu, waliopendekezwa nkwa upande wa wilaya na hata yale ya mkoa.

Baada ya hapo Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitapokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge kwa ajili ya maandalizi ya vikao vya uteuzi, kisha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitafikiria na kuteua majina ya WanaCCM wasiozidi watatu walioomba nafasi ya Ubunge na ili wakapigiwe kura za maoni na hatua zaidi ndani ya chama zitafuata kabla ya kumpata mgombea atakayekiwakilisha chama katika jimbo husika.

kama Mpina ni kweli ni mpigania haki za wanaKisesa na waTanganyika kwa ujumla wake ajiunge na No Reforms, no election Atoke upande wa shetani aje upande wa Mungu Aliye hai
 
Nachojua ameshapata mtaji kwahiyo akaribia katika kujiajiri kuna maisha nje ya ubunge.
 
Maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote yalikuwa very clear na wafanya maamuzi ya kupendekeza majina obviously wamehofia usalama wa vyeo vyao pamoja na uhai wa maisha yao

Tanzania imefikishwa hapo
 
Wakiwa huko CCM, ukiwaambia tudai Katiba mpya iliyo Bora zaidi, wanakuona hamnazo,

Kungekuwa na nafasi ya mgombea binafsi Mpina angechukua Jimbo kirahisi kwani anakubalika sana, ndani ya Jimbo na hata nje ya Jimbo,

Sasa kifuatacho kwake, kama ana biashara yoyote, ajiandae na ugeni kutoka TRA na mengine mengi ya gizani Hadi anyooshe mikono juu,

Muda ndio hakimu wa haki
Mgombea binafsi nalo ni wazo zuri nimeona kwa wenzetu Kenya wamefanikiwa,wagombea ambao hawajatendewa haki wanakuwa Independent candidate na kama anakubalika anachaguliwa vizuri tu, ninachoona mbeleni kama hakutakuwa na reform na wapinzani wakapewa nafasi,ccm kutakuwa na makundi na kitagawanyika na mbeleni huko kutakuwa na matabaka ya wenye nguvu ya pesa ndo wanapata nafasi za ubunge then maskini walio wengi watakosa haki na kujiondoa kwenye hiki chama katili na ndo itakuwa mwisho wa ccm
 
Mbunge wa Jimbo la Kisesa anayemaliza muda wake Luhaga Mpina huenda safari yake ya kuwawakilisha wananchi wa Kisesa ikafikia tamati ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu baada ya vikao vya mchujo kwa ngazi ya wilaya ya Meatu na mkoa wake wa Simiyu kumtupa nje ya mbio za kuwania kuteuliwa na CCM kupeperusha bendera kwenye nafasi ya ubunge katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu; vyanzo vya kuaminika kutoka ndani ya kikao cha kamati ya siasa ya CCM Mkoa wa Simiyu vimeitonya Jambo TV.

Mpina Mbunge machachari ndani na nje ya Bunge aliyejipatia umaarufu kwenye takribani miaka mitano sasa kwa kuibana serikali ndani ya Bunge na hata nje ya Bunge kwa hoja mbalimbali amekumbana na rungu la chama chake ngazi ya wilaya na mkoa baada ya vikao vya Kamati ya Siasa ya CCM wilaya ya Meatu kumtupa nje kwa kutopendekeza jina lake- maamuzi ambayo yamebarikiwa na chama ngazi ya mkoa hivyo sasa nafasi ya mwisho ya yeye kupenya jina lake kwa ajili ya kwenda kwenye mchakato wa kura za maoni ikibakia vikao vya ngazi ya taifa kwa maana ya Kamati Kuu ambayo imepewa mamlaka ya kufanya uteuzi wa mwisho.

Katika jimbo hilo, wagombea waliokuwa wakichuana katika hatua ya awali walifikia 14, lakini kupitia kikao cha wilaya na mkoa, majina yaliyopendekezwa ni Sitta Risinge, Mussa Mbuga, na Silinde Gumada.

Kiujumla, majina yote yaliyopendekezwa ngazi ya wilaya na mkoa hupelekwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM taifa, na Kamati kuu hiyo ina uwezo wa kuja na mapendekezo yake ya majina kwa kurejea majina ya awali ya wote waliochukua fomu, waliopendekezwa nkwa upande wa wilaya na hata yale ya mkoa.

Baada ya hapo Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitapokea na kuchambua majina ya wagombea Ubunge kwa ajili ya maandalizi ya vikao vya uteuzi, kisha Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kitafikiria na kuteua majina ya WanaCCM wasiozidi watatu walioomba nafasi ya Ubunge na ili wakapigiwe kura za maoni na hatua zaidi ndani ya chama zitafuata kabla ya kumpata mgombea atakayekiwakilisha chama katika jimbo husika.

Source: Jambo TV
Watampitisha kama njia ya watu kuoga ugwadu mwilini mwao na kupata kula ya "Paskali"
 
Kuliwa na Upinzani CCM itapoteza sana haiwezekani wagombea wanaokubarika ndio inawakata.
 
Mgombea binafsi nalo ni wazo zuri nimeona kwa wenzetu Kenya wamefanikiwa,wagombea ambao hawajatendewa haki wanakuwa Independent candidate na kama anakubalika anachaguliwa vizuri tu, ninachoona mbeleni kama hakutakuwa na reform na wapinzani wakapewa nafasi,ccm kutakuwa na makundi na kitagawanyika na mbeleni huko kutakuwa na matabaka ya wenye nguvu ya pesa ndo wanapata nafasi za ubunge then maskini walio wengi watakosa haki na kujiondoa kwenye hiki chama katili na ndo itakuwa mwisho wa ccm
Sio tuu wa ngazi za Ubunge Hadi udiwani pia.
 
Hata sasa mkuu, kama hutambuliki na wakubwa huko CCM, bado huwezi kupita,

Pia wakikuhitaji hata kama hujulikani unaweza kuwa mbunge hata pengine uwaziri, rejea nzuri ni kwa Mwana FA, walivyomtupa Mzee Adadi Rajabu, DCI mstaafu
 
Maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote yalikuwa very clear na wafanya maamuzi ya kupendekeza majina obviously wamehofia usalama wa vyeo vyao pamoja na uhai wa maisha yao

Tanzania imefikishwa hapo
Sim moja tu OUT

Ova
 
Back
Top Bottom