CCM: Serikali iifute kodi ya Sh 1,000 kwa simcards!

CCM: Serikali iifute kodi ya Sh 1,000 kwa simcards!

Viongozi wa CCM, kwa sasa wako katika hatua ya "Confusion & frustration" hatua ya juu kabisa ambayo kiongozi yeyote anapoifikia lolote laweza kutarajiwa.Katika kipindi hiki mpaka kufikia 2015, tutarajie kuona mambo mengi yasiyokuwa ya kawaida kutoka kwa watu hawa.
 
Dah, huu unafiki wa mwaka! CCM ndiyo iundayo serekali ka asilimia karibu zote, sasa haya mambo ya CCM kuiambia serekali yametoka wapi? How can you tell your own self!
 
nchi kama china wanasiasa waongo huchapwa viboko hadharani!!
 

316404_101272749985852_359014438_n.jpg
hivi cheni shingoni na tumafutamafuta tunaruhusiwa kwa wanaume siku hizi!? Nauliza tu.
 
si ajabu kwa CCm kuweka kikao cha kujidanganya wenyewe, wakiisha maliza kikao wanakula ruzuku...kama selikali inapingana na chama tawala, ni sawa na mtu kupingana na nafsi yake, roho inataka kwenda mjini lakini ubongo unataka kwenda ubunge,au labda kwa kifupi niseme wameisha poteza muelekeo, wantapatapa kukata roho...
 
hivi cheni shingoni na tumafutamafuta tunaruhusiwa kwa wanaume siku hizi!? Nauliza tu.
si tumafuta tu, ata mkorogo, kwakiasi unachoweza kujisavia, alafu ukitoka hapo unakwenda kutukana watu na akili zao kwenye mikutano kwasababu wamesifia chadema
 
Kuna nini cha kuchangia hapo na kila mmoja anatiwa mawazo yake, nawaonea huruma mnavyotolewa mapovu na Nape.

Ngojeni na Mwigulu arudi ndio kabisa kiboko yenu.

Keki ya taifa si mnaifaidi nyie wachache na vijukuu na wakwe zenu subirini sasa
 
wewe una afford kabisa. Kama kodi yako ni laki sita kwa mwezi maana yake una take home 10M+ kwa mwezi, sasa huoni hiyo elf saba kwa sim card 7 ni negligible, lipa bana acha ubahili au na wewe ni wakutoka kule milimani kwa wabahili?

Hahahahaah! Acha kuishi maisha ya kufikirika ndugu, live the real life, Hiyo 10M+ umeipata kwa ukokotozi upi?

Ushawahi sikia Mzimu unaoitwa P.A.Y.E, hizo laki 6 ni madhara ya hilo dude,

Kiuchumi hata senti haipaswi kutumika bila sababu za msingi hivyo elf 7 kwangu ni big deal, ndo hizo wanazotumia watoto na hawara zao kutanulia. hata hizo simcard 7 kwangu ni lazima, 4 nazitumia kwa modem na 3 kwa hand sets.
 
Amenikukumbusha shoo za masingaombwe wakati nasoma primary.....Mchanga unabadilishwa kuwa wali na udongo kuwa ugali. Nape acha kiini macho Watanzania hatudanganyiki kijinga.
 
Leo magazeti mengi yamebeba vichwa vya habari kuwa CCM inapinga tozo la simu la shilingi 100 kila mwezi kwa kila simu iliyosajiliwa. Kwangu mimi huu ni usanii, unafiki na hadaa kubwa kwa watanzania.

Naongea haya kwa sababu CCM, chama kilicho na wabunge wengi katika bunge letu ndio waliopitisha tozo hili, tena kwa kishindo wakati wa kujadili bajeti.

Tena katika kuonesha kuwa hawakuwa na dhamira ya dhati na walilenga kumkomoa mlipa kodi mtanzania, maamuzi ya kupitisha tozo hili katika simu zetu waliyafanya wakati watetezi wa watanzania, wabunge wote wa chadema walipokuwa katika msiba mkubwa wa wanachama wao waliolipukiwa na bomu jijini Arusha. CCM acheni unafiki kuwahadaa watanzania.

Ninachotaka kusema CCM waache za kizamani kwa sasa wananchi wamesoma na wanaelewa so waache kutuzuga,bajeti wapitishe wao alafu sasa wao hao hao wanajifanya kuishauri serikali kwani serikali inaongozwa na chama gani?tuseme hilo hawakuligundua kuwa linawatesa wananchi kabla hawajaamua kuipitisha hio tozo?na tena kukwepa vikwazo wamepitisha tozo Chadema wakiwa nje ya bunge kwa maombolezo ya kuuwawa kwa wanachama wao na mashabiki wao baada ya bomu kurushwa kwenye mkutano wa kufunga kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwan Arushai?Acheni kutuzuga mshalikoroga mlinywe tuonane 2015 na keshokutwa Sombetini Arusha.VIVA Chadema
 
Ccm ni chama dhaifu,serikali dhaifu endelleni tu kujiingiza kitanzi 2015 zamu yetu kuwaadhibu
 
Jamani mbona leo siwaoni humu wakirusha madongo kama walivyozoea? Jamani mko wapi njooni muokoe jahazi la wanaosema ndiooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Nape atasema yeye si mbunge kwi kwi kwi kwi kwi inji hii bwana kazi kweli kweli ndiyoooooooooooooooooooooooooooo
 
Halafu kuna mijitu ya CCM humu ilikuwa inaunga mkono hii kodi wakati chama chao kinataka ifutwe.
 
Hizi ni dalili tosha za mfa maji. Kifo cha ccm kinakaribia. Iweje wabunge wa ccm wapitishe halafu baada ya kuona upepo unakuwa mbaya Nape anakanusha???
 
chadema ndiyo wa kwanza kudai kodi hii iwepo tena mdee.

Wacha weee!!!!!kwa hiyo waliopitisha kwa kutumia uwingi wao,na slogan ya ndioooooooo!!! Ni kina Mdee????ufafanuzi tafadhari.
 
AKILI NDOGO INAONGOZA AKILI KUBWA! tehe tehe tehe, kwi kwi kwi kwi!
 
Back
Top Bottom