CCM: Serikali iifute kodi ya Sh 1,000 kwa simcards!

CCM: Serikali iifute kodi ya Sh 1,000 kwa simcards!

Simba mnyama

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
348
Reaction score
129
Leo magazeti mengi yamebeba vichwa vya habari kuwa CCM inapinga tozo la simu la shilingi 100 kila mwezi kwa kila simu iliyosajiliwa. Kwangu mimi huu ni usanii, unafiki na hadaa kubwa kwa watanzania.

Naongea haya kwa sababu CCM, chama kilicho na wabunge wengi katika bunge letu ndio waliopitisha tozo hili, tena kwa kishindo wakati wa kujadili bajeti.

Tena katika kuonesha kuwa hawakuwa na dhamira ya dhati na walilenga kumkomoa mlipa kodi mtanzania, maamuzi ya kupitisha tozo hili katika simu zetu waliyafanya wakati watetezi wa watanzania, wabunge wote wa chadema walipokuwa katika msiba mkubwa wa wanachama wao waliolipukiwa na bomu jijini Arusha. CCM acheni unafiki kuwahadaa watanzania.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekuja juu na kuitaka Serikali kuangalia njia nyingine mbadala ya kukusanya kodi na kuachana na mpango wa kuanza kuwatoza wananchi tozo ya Sh 1,000 kila mwezi kwa kila laini ya simu ya kiganjani.

Hatua hiyo, inatokana na kilio cha wananchi ambao tangu Bunge la Bajeti kwa mwaka 2013/14 kupitisha sheria hiyo, kumekuwa na manung'uniko mengi.

Uamuzi huo, ulipitishwa na Bunge baada ya mjadala mkali pindi bajeti ilipotangazwa kitendo kilichomfanya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. William Mgimwa kuomba Serikali ipewe muda wa kutosha wa kujadili suala hilo.

Baada ya majadiliano na Kamati ya Bajeti ambayo inaongozwa na Mbunge wa Bariadi, Chenge Chenge (CCM), Waziri Mgimwa pamoja na Bunge waliridhia wananchi waanze kutozwa fedha hizo, kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye mjini Dar es Salaam jana, ilisema CCM inapinga tozo hiyo kwa sababu itaongeza mzigo kwa mwananchi wa kawaida na kusababisha usumbufu usiokuwa na sababu kwa walalahoi.

Tozo hiyo, ilipitishwa na Bunge la Bajeti ikielezwa kuwa ni utaratibu wa kawaida wa kuibua vyanzo vipya vya kodi pale vinapoondoshwa vilivyopo kwa sababu mbalimbali.

Katika taarifa hiyo, Nape alisema licha ya umuhimu huo, vigezo vilivyotumika kupanga viwango sawia vya kodi hiyo kwa kila mtu mwenye laini ya simu, havijazingatia hali ya utofauti wa kipato kwa Watanzania.

Alisema wengi wao, matumizi yao ya simu ni ya kiwango cha chini mno tofauti na Serikali inavyofikiria.

"Kama chama tawala, tunaona hatuwezi kukaa kimya kwenye jambo ambalo tunaliona linawabebesha mzigo wananchi na huenda likarudisha nyuma maendeleo na kuchelewesha jitihada za kuboresha maisha ya Watanzania kwa ujumla," ilisema taarifa hiyo.


Source: Gazeti la Mtanzania.

Wakati wa vikao vya bunge lililopita ndipo bajet hii ilipitishwa. Cha kushangaza waliopitisha kwa kusema wanaunga hoja mkono kwa 100% ni wabunge wa CCM! Leo CCM inapata wapi moral authority ya kuishauri serikali kuondoa kodi hii huku ikiwa wao ndio waliipitisha?
 
Undiminakuwili wa wanaccm unazidi kujidhihirisha mara baada ya bwana Nape Mnauye kuja na lake kuwa CCM nayo inapinga tozo za simu wadai ni mzigo kwa wananchi.

Najiuliza hivi CCM ni nani????? Na wale CCM wanoitana kupitish bajeti ni CCM ipi?
 
Chama chama Mapinduzi kimeishauri serikali kuondoa kodi ya sh 1000 kwa kila laini ya simu na kwamba itafute njia nyingine ya kuongeza Mapato.

Wamesema kwmba swala la serikali kuwakamoa wananchi ktk hili la kodi ktk line za simu halifai na kwamba kuna njia zingine nyingi rasmi ambazo zinaweza kuongzea serikali mapato badala ya hii ya kuongeza kodi kwenye lain za simu.

Wakati huohuo MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA imesema kwamba itakua inakusanya bilion 28 kwa mwezi kwa kukata sh 1000 ktk kila lain ya simu. Inasemekana kuwa Watanzania wanao tumia simu sasa nchi nzima ni zaidi ya ml 28.

Source; Gazeti la Mtanzania.

Wakati wa vikao vya bunge lililopita ndipo bajet hii ilipitishwa. Chakushangaza waliopitisha kwa kusema wanaunga hoja mkono kwa 100% ni wabunge wa CCM! Leo CCM inapata wapi moral authority ya kuishauri serikali kuondoa kodi hii huku ikiwa wao ndio waliipitisha?
 
Huo ndio unafiki dhahiri wa CCM!tarehe 19th august tuzizime simu zetu zote kwa saa 24,wape ujumbe na wengine

Sijui nini kifanyike dhidi ya unafiki wa magamba hawa. Wabunge wao walipitisha gharama hizi, wote wakashangilia kama kawaida yao, leo wanakuja kinyume chake? Huu ni unafiki uliokithiri. Tunaomba cdm ipige kelele zaidi ambavyo imwahi kufanya. Na sapport mgomo wa kizima simu
 
Huu ni unafiki mkubwa sana kwa viongozi hawa wa CCM tuliowapa dhamana ya kutuongoza. We fikiri kikao cha bunge kilichopita wote wabunge wa CCM walipitisha kwa mbwembwe mapendekezo hayo ya kutoza kila lain sh 1000. Halafu leo wanatujia na NGONJERA.
Kwanza tangia kupitishwa kwa bajet hii sio tu kuwa ni sh 1000 imeongezwa isipokua kwa wale km mimi ambao nilikua nanunua sekunde 18000 (yaani dk 300) kwa sh 5000,sasa hivi nanunua sh 6000. Kwahiyo kwa mwezi huwa nanunua mara 4 kwahiyo tayari kuna ongezeko la sh 4000. Hiyo ni km nitakua natumia hizo sekunde 18000 kwa siku 5. Lakini mara zingine natumiaga siku 2 tu halafu zinakua zimeisha na hairuhusiwi tena kununua ya 5000 hadi siku tano ziishe,hivyo inabidi ninunue sekunde 6000 kwa 2000,ambapo sasa nanunua kwa sh 2500 kwa hiyo kwa mwezi nimeongezewa kodi ya zaidi ya sh 5000 ukijumlisha na tozo ya sh 1000 ya line nitakua nalipa sh 6000 kwa mwezi.

Hata wale waliokua wananua muda wa maongezi wa sh 500 kwa siku sasa hivi wananunua sh 600 kwa masaa 24 yaani siku moja. Hivyo kwa kila siku kuna ongezeko la sh 100. Kwa mwezi ni sh 3000 ukijumlisha na tozo ya line sh 1000 itakua ni sh 4000 kwa mwezi. Bado kwenye M- pesa kuna ongezeko la sh 500 kwa mtu aliekua akikatwa 1000 wakati wa kutoa pesa.

CCM watakua wanafiki endapo watazungumzia tu sh 1000 inayokatwa km tozo ya lain kwa mwezi huku wakiacha kuzungumzia hizi za kwenye muda wa maongezi. Hii nchi inaongozwa kisiasa mno ndio maana kila kitu bora liende.

Tunawaomba CHADEMA na wanaharakati kulipinga hili kwa nguvu zote na kuachana na hawa Wasanii wa CCM wanaopitisha bajet ya kutukamua halafu leo wanatujia na Hadithi!
 
Nikichekesho kweli kweli,kama kweli Nape anageuka wakati anajua wabunge wake ndio walio itika ndiyooo,hapo napo hapa hitaji majibu yakwenda shule
 
Leo magazeti mengi yamebeba vichwa vya habari kuwa CCM inapinga tozo la simu la shilingi 100 kila mwezi kwa kila simu iliyosajiliwa. Kwangu mimi huu ni usanii, unafiki na hadaa kubwa kwa watanzania. Naongea haya kwa sababu CCM, chama kilicho na wabunge wengi katika bunge letu ndio waliopitisha tozo hili, tena kwa kishindo wakati wa kujadili bajeti. Tena katika kuonesha kuwa hawakuwa na dhamira ya dhati na walilenga kumkomoa mlipa kodi mtanzania, maamuzi ya kupitisha tozo hili katika simu zetu waliyafanya wakati watetezi wa watanzania, wabunge wote wa chadema walipokuwa katika msiba mkubwa wa wanachama wao waliolipukiwa na bomu jijini Arusha. CCM acheni unafiki kuwahadaa watanzania.

wameianzisha wenyewe halafu wanaipinga wenyewe kuwadanganya wananchi kuwa wanawatetea wananchi. CCM wana mbinu za kitoto-toto, chama wamempa kipofu mwigulu akiongoze.
 
Kuna kipindi wengine tulidhani labda wazee wa CCM wameishiwa mbinu ktk siasa za kisasa kumbe vijana wao ndio balaa kabisa.
CCM fanyeni siasa acheni mazingaombwe.
Mnatufanya mabwege? Kizuri mnajinadi kimefanywa na serikali ya CCM likitokea tukio la ajabu mnaikana serikali yenu?
Ndio maana January Makamba ameanza kufanya siasa zake mwenyewe na si za CCM isiyo na dira inayoongozwa na Mtela,Shonza,Tambwe Hiza,Mwigulu na Nape.
 
Ushauri kwa Nape Nnauye: hama CCM, unadhalilishwa sasa..... Yaani wao waseme ndiyooooooooo halafu wewe uje uwasemee hapanaaaaaaaa....!!! UJINGA
 
Undiminakuwili wa wanaccm unazidi kujidhihirisha mara baada ya bwana Nape Mnauye kuja na lake kuwa CCM nayo inapinga tozo za simu wadai ni mzigo kwa wananchi.

Najiuliza hivi ccm ni nani????? Na wale ccm wanoitana kupitish bajeti ni ccm ipi?


double standard kwa watawala wengi wa afrika ni kawaida tu kwa sasa
 
Unafik wa waziwazi bila hata haya????
Shame on you!!!
 
Back
Top Bottom