Nimesoma habari ya Jaji Warioba katika gazeti la Raia Mwema la leo, nikagundua kuwa CCM bado inafikiri kuwa Watanzania kuwa ni wajinga kiasi hicho, wanachofikiri wao ni kuwa bado kuna watu wanaweza kufikiri vizuri kwa ajili ya watu wengine.
Kingine nilichogundua ni kuwa CCM wanaweweseka, na CCM ndio itakayoleta vurugu nchi hii kwa kuwa haiko tayari kushindwa kidemokrasia yamejidhihirisha katika mazungumzo hayo ya Jaji Warioba.
Lingine nililojifunza ni kuwa CCM sasa wanatumia mbinu zozote zile zidi ya CHADEMA kuwa kuwa haiwezi tena kushindana na CHADEMA kisera imebakia kuropoka, sasa wamebuni mbinu za kuwatumia watu maarufu kama Warioba kujifanya wanazunguzia mustakabali wa nchi bila upendeleo huku wakiingiza maoni ya kuiponda CHADEMA.
Warioba anasema Chadema kule igunga wasifikiri wanapanda chati ile inaweza kuwa nguvu ya soda halafu anaingiza propaganda za CCM za udini na kuwa CHADEMA si chama cha watu.
Tumuulize Warioba atupe data zinazoonyesha kuwa kule si kupanda chati bali ni nguvu za soda si kuzungumza kisiasa na kinadharia. Wengine sisi si wanasiasa tunataka analysis and fact.
Angalizo kwa CHADEMA ni kuwa kuna nguvu iliyo nyuma ya pazia ya kuiangamiza ambayo ni kubwa sana, sasa hivi wanawatumia wakongwe hao wameanza na Warioba, atafuata Salim, gazeti la Raia Mwema limeshachukuliwa! Kumbuka Warioba na Jenerali na Mkapa walikuwa marafiki wakubwa sana kabla ya wawili wao hawajagombana.
Mimi nimefanya kazi kwa Jenerali Ulimwengu wakati wanaanzisha gazeti la Mtanzania nawafahamu vizuri.
Watanzania tusikubali kuruhusu watu kufikiri kwa niaba yetu, CCM hawako tayari kuona chama kingine kwa kuwa wanaogopa utawala mwingine kwa kuwa wanajua katika CCM hakuna aliyemsafi kamili. Watajifanya kujikosoa wenyewe ili wabaki madarakani ili kulinda madhambi yao. Tuendelee kupambana mapaka ukombozi kamili upatikane.
Mungu ibariki Tanzania.