CCM njiapanda Urais 2015: Kumpitisha Lowassa au chama kumeguka

Hakuna anaempenda lowasa, ananunua na kufanya propaganda nyingi kulaghai wa tanzania aonekane anakubalika. CCM kupitia wabunge wake walishakosa imani nae wakamwangusha uwaziri mkuu, Wakimleta tena kwa wananchi na kuanza kumsafisha katika kashfa ambazo wao CCM walishindwa kumvumilia itakuwa maajabu sana na itabidi waibe kura maana watashindwa, wananchi wataonyesha hasira zao kwenye sanduku la kura.
CCM iteuwe mtu safi mwadilifu, mchapakazi asiye na ma kashfa mengi then wamnadi na kumfanyia kampeni kama chama.

Sasa wewe mkuu ccm ina wabunge wa maana pale? wale si wafuata upepo tu hata e
leo ukiwakusanya pale bungeni na kuwaamrisha wamsifie Lowasa watafanya na vigelegele juu@!! yaani yapo yapo tu :sleepy:
 
Mpaka sasa kamati ya maadili ya Chama Cha Mapinduzi CCM bado iko njia panda katika kufanya maamuzi magumu juu ya wanachama wake waliofungiwa kwa kuanza kampeni mapema.

Imebainika kuwa sababu kubwa inayowafanya wajumbe kamati hiyo inayoongozwa na Philip Mangula kuwa wakati mgumu kutona na kwamba viongozi wa juu wa chama hicho kushinikiza jina la Lowassa kutwa.

Kinachosumbua mpaka sasa ni ushawishi mkubwa wa mh. Lowassa ndani ya chama na nje ya chama hicho na imegundulika kuwa si kweli kwamba kamati hiyo inajadili majina yote ya waliofungiwa inasema kuwa muda mwingi zaidi ya asilimia 70% ya muda wote kamati inapo kutana ni kumjadili Lowassa tu.

Tatu,vijina wenye mapenzi mema na nchi wameanza kujiorganize nchi nzima kuhakikisha kuwa nchi inatawaliwa na mtu mwenye maamuzi magumu na ya uhakika wamechoka kubuluzwa.

Hapa mawili LOWASSA RAIS AU MWISHO WA CCM.

yetu macho
 
Ni wazi kuwa Mzee Lowassa anaungwa mkono na wenyeviti wa CCM wa zaidi ya Mikoa saba, nikitaja kwa uchache, Geita, Singida, Arusha, Manyara, Shinyanga, Mara, Kilimanjaro, Dar es salaam.

Watu hawa wana nguvu na ushawishi mkubwa na ndio nguzo ya kampeni ya chama Mikoani na Wilayani, jaribio lolote la kumkata Lowassa, litashusha kishindo kikuu Mikoani ambapo zitaendeshwa kampeni za kumpinga au kumdhoofisha yeyote atakayeteuliwa.

Mpaka sasa Lowassa ana kura milioni moja kutoka kwa wana CCM wachache, hii inatokana na wengi kukosa nafasi ya kumdhamini.

Akikatwa ni wazi kura milioni moja zimekwenda, achilia mbali za mamilioni kadhaa wasio wana CCM ambao ni washabiki wake.

Taarifa zinaeleza kwamba kama angepata muda wa kutosha, Lowassa alikuwa na uwezo wa kupata wadhamini milioni nne ndani ya CCM pekee.


Mimi mwenyewe nilikataliwa kudhamini kutokana na kuambiwa kuwa sio mwanachama wa ccm
 
Huyu mtuleteee wapinzani ndoo tutashinda uchaguzi saa 4 asbhi. Tuna ushahidi wa wizi wake sio Richmond. tunaongelea Pre Meremeta aka Alivyoua kiwanda cha Nyumba. Mtabaki midomo wazi.
 
*Kwannini lowasa alitajwa list of shem?


*Kwanini lowasa alitakawa kuvuliwa gamba ndani ya siku 90 ??

Nikipata haya majibu kwa ufasaha naweza kubadili msimamo wangu

Labda nikuelimishe kidogo na kwa faida ya wengi pia. Lowassa kuhusishwa na richmond na kupelekea kujiuzulu sio kwa kuhusika na ufisadi bali nia iliyochukuliwa ovu ya kutekeleza uovu. Haupo ushahidi wowote wa serikali kumlipa richmond fedha yoyote ya kufua umeme hivyo Lowassa asingeweza kufaidika na mtu/kampuni ambayo haikulipwa kwani nayo haikutoa huduma yoyote.Richmond baada ya kusaini mikataba ya kulipatia taifa umeme ilikuja gundulika kuwa hawakuwa na mtaji, utaalamu na hata ofisi. Baada ya Lowassa kama waziri mkuu kugundua hilo alimjulisha mkuu wa nchi aliyekuwa safarini ulaya kuwa anatengua mkataba kati ya serikali na richmond na raisi aliporejea nchini mkataba ulivunjwa na kuingia mkataba na kampuni iliyokuwa na uwezo wa kuzaliaha umeme.Hivyo sio kweli kuwa Lowassa alifaidika na richmond kwani serikali haikupoteza hata senti tano kwa kampuni hii.Ile nia ya Lowassa kutekeleza ule mkataba ndio ulioifanya kamati ya bunge kumwambia apime yeye mwenyewe kubakia na nafasi yake kama waziri mkuu au kuwajibika kisiasa. Uelewe kwa miaka ile ufisadi ulikuwa nadra sana kwa viongozi na watendaji serikalini. Hakika ile kamati ingegundua jinai katika uchunguzi wao wasingesita kumfikiaha mahakamani haswa takukuru kwani nao walihusishwa pia. Hilo zoezi la ccm kuvuana magamba nalo lilimlenga Lowassa kwani waliukosa ushahidi wa kumhusisha kwa kosa lolote.Wapo wengi haswa viongozi wa juu wanaomhofia Lowassa akiwa raisi wa nchi kuwa mali zao walizoliibia taifa zitakamatwa na wao kushtakiwa na ndio mizengwe unayoishuhudia na kusahau kuwa chqguo la wengi ndilo chaguo la mungu pia. Wanaweza kushindana na wasishinde. Sasa kwa ugumu wa miyo yao na roho mbaya zao wamkate Lowassa Slaa aapishwe. Sasa maamuzi ni yako ya kumuunga mkono au kuacha na ukumbuke mafisadi ni kama waliofungwa jana wewe hukupata habari?
 
Wana Jamii Forum nauona mwisho wa CCM ndio umefikia tamati.CCM hawakujua kuwa kila,chenye mwanzo kina mwisho wake.Kama,ambavyo JK amehitimisha bunge jana hivyohivyo anakwenda na chama chake.Ishara moja ya dhahiri ni,hii ukimpitisha Lowasa chama kinagawanyika.Usipompitisha vilevile chama,kimegawanyika.Kwahiyo sioni nafuu yoyote.CCM ilianza kama mtoto hatimaye ikawa kijana na baadaye imezeeka kinachofuata,nini.Nukuu Jaji Warioba,Jaji Manento,Butiku,Polepole na Waraka wa Kakobe kwa JK
 
Wana Jamii Forum nauona mwisho wa CCM ndio umefikia tamati.CCM hawakujua kuwa kila,chenye mwanzo kina mwisho wake.Kama,ambavyo JK amehitimisha bunge jana hivyohivyo anakwenda na chama chake.Ishara moja ya dhahiri ni,hii ukimpitisha Lowasa chama kinagawanyika.Usipompitisha vilevile chama,kimegawanyika.Kwahiyo sioni nafuu yoyote.CCM ilianza kama mtoto hatimaye ikawa kijana na baadaye imezeeka kinachofuata,nini.Nukuu Jaji Warioba,Jaji Manento,Butiku,Polepole na Waraka wa Kakobe kwa JK

Mkuu hapa ni PAGUMU. Maana ninashindwa kuelewa wanaosema EL ni fisadi wakati wengine siyo MAFISADI! Na ndiyo maana factor FISADI haiwezi kutumika kumkata EL. Hivyo linatafutwa ZENGWE jingine kwani UFISADI unawagusa wote!
 
Back
Top Bottom