CCM ni wa ajabu sana

CCM ni wa ajabu sana

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Yaani mambo ya kimaendeleo yanayofanywa kwa wananchi wanayaona kama zawadi au fadhila. Siku ya uzinduzi waandishi watajazwa;hotuba za tambo zitatolewa na kadhalika. Mambo ya ajabu kabisa!

Hoja ni hizi. Mosi,kama chama tawala chenye Serikali yenye dhamana zote za mapato ya kiinchi,kuleta maendeleo ni wajibu wao wa lazima. Wananchi wapatiwe maji,umeme,shule,vivuko,barabara,hospitali na huduma nyinginezo kama haki yao na si fadhila.

Pili,hakuna uwiano mzuri kati ya rasilimali tulizonazo kama taifa;pato la taifa na maendeleo yanayopatikana. Wananchi hawaoni matumizi sahihi na ya kimaendeleo ya utajiri wa nchi hii. Hadi leo,baada ya miaka hamsini na mbili ya Uhuru,CCM na serikali yake inazindua shule ya sekondari au kisima halafu wanajitamba!?
 
Tarifa mbovu haina uthibitisho imebeba umbea mtupu bila hata chenga lakini ndiyo kazi mliyopewa bavicha na dj wenu endeleeni.
 
CHADEMA mbona mnaanza kuweweseka? Serikali inafanya maendeleo halafu matumizi sahihi hayaonekani ndiyo umesema nini?
 
Tarifa mbovu haina uthibitisho imebeba umbea mtupu bila hata chenga lakini ndiyo kazi mliyopewa bavicha na dj wenu endeleeni.

Mkuu huyu mleta mada atakuwa na faili MIREMBE. Anasema ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo hakuna sabau ya kutamba. Kwa akili ya kawaida sidhani kama kuna mtu anamuelewa anachokisema ni nini
 
Yaani mambo ya kimaendeleo yanayofanywa kwa wananchi wanayaona kama zawadi au fadhila. Siku ya uzinduzi waandishi watajazwa;hotuba za tambo zitatolewa na kadhalika. Mambo ya ajabu kabisa!

Hoja ni hizi. Mosi,kama chama tawala chenye Serikali yenye dhamana zote za mapato ya kiinchi,kuleta maendeleo ni wajibu wao wa lazima. Wananchi wapatiwe maji,umeme,shule,vivuko,barabara,hospitali na huduma nyinginezo kama haki yao na si fadhila.

Pili,hakuna uwiano mzuri kati ya rasilimali tulizonazo kama taifa;pato la taifa na maendeleo yanayopatikana. Wananchi hawaoni matumizi sahihi na ya kimaendeleo ya utajiri wa nchi hii. Hadi leo,baada ya miaka hamsini na mbili ya Uhuru,CCM na serikali yake inazindua shule ya sekondari au kisima halafu wanajitamba!?

Visima na shule za sekondari ndiyo huduma zenyewe za jamii, wewe ulitaka wazindue sayari ya watanzania nini?
 
Umri wa uhuru hatukupaswa kuzindua visima na shule zakata kwa mbwembwe,uzinduzi wa mbwembwe kwa vitu hivyo ulipaswa ufanyike miaka ya 69,Leo tulipaswa kuzindua viwanda vikubwa vya kutengeneza Magari nk.Ccm yaleo mnazindua hata vijiwe vya kahawa,vijiwe vyakuzibia puncture na car wash.Hakiks ukiwa Ccm hauoni nadhani ni laana
 
CCM ni chama kinachowaletea maendeleo wananchi. Si hawa ambao hata fedha za walipa kodi wanazopata kama ruzuku haijulikani zinaenda wapi.
 
Mpira uchezwe uwanjani huko Brazili wengine wanaonesha hasira zao kwa serikali. Huu ni upuuzi wa hali ya juu sana
 
Ulitakiwa kujaza mazuri ya chama chako hapa sio kubinua midomo tu!!!!!
 
Mpira uchezwe uwanjani huko Brazili wengine wanaonesha hasira zao kwa serikali. Huu ni upuuzi wa hali ya juu sana

Mpuuzi ni wewe unayedhani kuwa kila mtu ni shabiki wa Brazil. Karibu leo Argenina wanaposhuka dimbani. Hoja hapa ni kuwa CCM inatambia vitu vya lazima kuvifanya kwa wananchi.Ni kama mazazi kutamba kumlisha na kumvisha mwanane
 
Mkuu huyu mleta mada atakuwa na faili MIREMBE. Anasema ni wajibu wa serikali kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo hakuna sabau ya kutamba. Kwa akili ya kawaida sidhani kama kuna mtu anamuelewa anachokisema ni nini

Huwezi kuelewa kwakuwa wewe Mkuu thatha ni kilaza
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom