Yaani mambo ya kimaendeleo yanayofanywa kwa wananchi wanayaona kama zawadi au fadhila. Siku ya uzinduzi waandishi watajazwa;hotuba za tambo zitatolewa na kadhalika. Mambo ya ajabu kabisa!
Hoja ni hizi. Mosi,kama chama tawala chenye Serikali yenye dhamana zote za mapato ya kiinchi,kuleta maendeleo ni wajibu wao wa lazima. Wananchi wapatiwe maji,umeme,shule,vivuko,barabara,hospitali na huduma nyinginezo kama haki yao na si fadhila.
Pili,hakuna uwiano mzuri kati ya rasilimali tulizonazo kama taifa;pato la taifa na maendeleo yanayopatikana. Wananchi hawaoni matumizi sahihi na ya kimaendeleo ya utajiri wa nchi hii. Hadi leo,baada ya miaka hamsini na mbili ya Uhuru,CCM na serikali yake inazindua shule ya sekondari au kisima halafu wanajitamba!?