Ccm ni ile ile..sasa inaleta maana.

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,146
2,000
Nimetafakari kwa kina baada ya kuurudia huu wimbo kichwani kwangu mara kadhaa
Ccm ni ile ile, hata atokee kiongozi mwenye maono mazuri kiasi gani bado Ccm ni ileile baada ya muda itarudi kulekukule..
Nimemuona Polepole kule Monduli akimpokea Lowasa mwili ulikuwa pale lakini ninaamini kabisa nafsi yake yamkini haikuwa pale, bila shaka ilikua umbali mrefu sana ikibebwa na tafakuri.kadhaa ndani yake,
Nimejaribu kuvuta picha ya Mh Balozi W Slaa huko aliko nikawaza picha aliyo nayo kichwani kwake kwa wakati huu.
Nikavuta taswira Ya Watanzania waliokuaa wameanza kuiamini Ccm na kujivunia ubora wake hisia zao baada ya ugeni ule wa monduli na mbwembwe zake.!

Nikajikuta taratiibu ninaanza hatua za kujisogeza kando na chama hiki kikongwe barani Afrika, taratiibu mapenzi yaliyo anza kuchipua kwa chama hiki naona yanaanza kufifia na kuvunjika moyo naamini hali hii itawakuta vijana wengi sana walio amua kuiunga mkono Ccm wakiamini ni safi
Sitashangaa harakati za akina.
Kafulila, Machali, Kisandu, na wengine wengi zikizaliwa upya ndani ya Ccm na hii itakuwa ni CCM B au CCM academia..

Zao la vijana wanaoitakia Mema Nchi hii bila shaka kutakuwa na Vuguvugu fulani jipya ndani ya CCM, Muda ni hakimu mzuri..


Sent using Jamii Forums mobile app
 

mikedean

JF-Expert Member
Mar 15, 2018
2,636
2,000
ccm ni mzizi uliojichimbia chini sana.kuucjimbua ni mpaka ufanye mapinduzi/mageuzi.aJiwe na ujanja wake ameshindwa.ko tuhesabu hasara kwa taifa ukicheki Rostam karudi,Lowassa mzee wa madili na saiz kuna vilaza wèngi akina bashite,pole2,katibu mkuu na wengineo.sio enzi za kina kinana na mangula

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,411
2,000
Enzi za mwalimu tulikua na si si em, na nyakati hizi tuna fis em. Hapo lazima kuwe na tofauti. Siku hizi muhimu mkono uende kinywani. Sasa kwa nini usiwe mnafiki na kujiondoa ufahamu? Kuna mtu nyakati hizi anapenda kula kwa jasho!
 

Rhz4567

JF-Expert Member
Mar 16, 2018
2,783
2,000
Waliipenda wenyewe waliijenga wenyewe wataiachaje kirahisirahisi hivyo
Capten Komba hajakosea kwenye mwimbo wake wa CCM ni ileile
 

getrusa

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
2,146
2,000
ccm ni mzizi uliojichimbia chini sana.kuucjimbua ni mpaka ufanye mapinduzi/mageuzi.aJiwe na ujanja wake ameshindwa.ko tuhesabu hasara kwa taifa ukicheki Rostam karudi,Lowassa mzee wa madili na saiz kuna vilaza wèngi akina bashite,pole2,katibu mkuu na wengineo.sio enzi za kina kinana na mangula

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndipo ninapopata shaka! Mwanzo Jpm alisema Ccm imeoza kila mahali akajitahidi kuanza kusafisha ghafla bin vuu uchafu unarudishwa na kasi ya kimbunga safari hii unaingia machoni, puani masikion..! Mdomoni..
Unakutia upofu huoni mbele..!
Unakuziba pua husikii tena harufu ya uchafu.!
Unakuziba masikio husikii tena kelele za wananchi na wanyonge wanaolitakia mema Taifa hili..
Unakuingia mdomoni unajikuta huwezi tena kufunua kinywa chako kukemea.

Na huu bila shaka ndio Mwisho.!
Katu, sitarajii wafaidika wa Mtandao wa Lowasa na Rostam Aziz watakaa kimya, maslahi yao yakiguswa kwa namna yoyote ile.!
Ninauona upande wa akina H.Mwakyembe, Dr W. Slaa, H. Polepole na bila shaka JPM mwenyewe wanavyopata tabu..


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom