CCM ni Doa Nyeusi Katika Mifumo ya Utawala wa Nchi

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,579
41,141
Kipingamizi kikubwa cha mifumo mizuri ya utawala maeneo mbalimbali ni CCM. Na hakika, nchi hii kamwe hatutakuja kuwa na mifumo bora ya kiutawala mpaka CCM itakapokuwa nje ya utawala.

Kikwazo kikubwa cha kuwa na Bunge huru, ni CCM. CCM inataka kulidhibiti Bunge kwa mlango wa nyuma, ndiyo sababu ya kuweka kanuni kuwa mgombea wa nafasi ya Uspika ni lazima apendekezwa na chama. Ndiyo sababu ya kuweka sheria kuwa mgombea wa Ubunge ni lazima adhaminiwe na chama, na akihama chama, ubunge wake upotee. Mfumo mzima wa kuwapata wabunge na spika umelenga dhamira chafu ya kulidhibiti Bunge. Kwa mfumo uliopo sasa, Bunge na Mahaka ni kama idara za Serikali na chama.

Kikwazo kikubwa cha kushindwa kuwa na mahakama huru ni CCM. Wameweka sheria eti Jaji mkuu, jaji kiongozi, msajili wa mahakama, na majaji wote ni lazima wateuliwe na Rais ambaye, tunajua ni Mwenyekiti wa CCM. Kwa sababu ya kutetea uroho wa madaraka, majaji wengi ni wanaCCM wa siri. Hilo limedhihirika mara nyingi. Mara kadhaa, tumepata wagombea wa nafasi za kisiasa ambao walikuwa majaji kupitia CCM, huku haieleweki walianza kuwa wanachama wa CCM tangu lini.

Ni nani ambaye hawezi kumpendelea aliyemteua? Ni nani anaweza kumteua mtu ambaye anafahamu ana mlengo tofauti na wa kwake? Kwa hiyo, ukiangalia kiuhalisia, kusema kuwa Bunge na mahakama, ni mihimili huru, ni lugha za kisanii, za kuwapumbaza watu.

Nampongeza marehemu Magufuli kwa kuwa mkweli. Yeye alitamka, japo siyo kwa uwazi, kuwa hiyo mahakama na Bunge si chochote, pale alipotamka kuwa kuna mhimili uliojichimbia zaidi.

CCM ndiyo mvurugaji mkubwa wa itendaji wenye weledi kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Wamevifanya vyombo hivi, kwa mlango wa nyuma, kuwa vyombo vya chama. Mara ngapi tumeshuhudia makamanda wa Polisi, wanapostaafu wanaenda kugombea ubunge kupitia CCM au hata kugombea nafasi za umwenyekiti wa CCM Wilaya au mikoa? Hawa walikuwa wanachama wa CCM kuanzia lini hata waaminiwe kuwa viongozi wa chama?

Nafasi karibia zote, kama vile CAG, DPP, mashirika ya umma na taasisi nyingine ambazo watendaji wake wanateuliwa na Rais, ukifuatilia, utagundua kuwa ni wanachama au wamethibitisha utiifu wao kwa CCM. Utiifu kwa CCM ni sifa mojawapo kubwa iliyojificha. Hii ni sababu mojawapo kubwa, taasisi nyingi za umma kushindwa kuendeshwa kwa weledi kwa sababu vigezo vya weledi huwa vinapewa nafasi ndogo.

Leo hii vyuo vyetu vikuu vimepoteza heshima kwa kugawa PhD kwa baadhi ya viongozi wenye mafungamano na CCM, huku kukiwa na mashaka makubwa kama PhD hizo zimezingatia vigezo. Lakini vyuo vitafanya nini ikiwa viongozi wa vyuo hivi indirectly ni wateule wa CCM? Taasisi hizi zitakuwa na nguvu gani ya kumkatalia kiongozi wa serikali/CCM anayetaka kupata PhD kwa njia ya mkato au kwa kuchakachua?

Ifahamike wazi kuwa utafiti wa TWAWEZA uliwahi kutamka wazi kuwa:

1) CCM inaungwa mkono zaidi na watu wasio na elimu na wazee (japo hapa naamini ni wale wazee wenye uelewa na upeo mdogo au wale wanafiki na watafuta vyeo)

2) Vyama vya upinzani, vinaungwa mkono zaidi na wasomi na vijana (Wakimaanisha wasomi wa kweli, siyo hawa wasomi michongo wa sasa wanaogawana PhD kama njugu za sokoni).

Kwa sababu ya kuendekeza uCCM kila mahali, leo hii maeneo mengi yaliyohitaji watu wenye weledi, wamewekwa watu ambao hawana uwezo unaohitajika kwenye nafasi hizi, lakini kwa sababu ni waimbaji wazuri wa sifa kwa CCM, wapo kwenye hizo nafasi, huku Taifa likiteketea kwa kukosa ufanisi unaohitajika. Hii ndiyo sababu kuu ya kila mwaka ATCL kupata hasara, TANESCO kupata hasara, NDC kupotea, UDA kufilisika, TTCL kuchechemea, n.k.

Hakuna Mtanzania yeyote, mzalendo wa kweli, anayeipenda nchi yetu anayeweza kufurahia Chama chochote, au Serikali au Rais kudhibiti taasisi zilizostahili kuwa huru. Rais ni mtu, Serikali ni kikundi kidogo, CCM ni kikundi kidogo cha watu, hawa wote wanaweza kukosea au kwa bahati mbaya, au kutokana na weledi mdogo au kwa makusudi, tusipokuwa na vyombo au taasisi nyingine huru, ina maana CCM ikikosea, Serikali ikikosea au Rais akikosea, nchi nzima inatumbukia shimoni kwa sababu hakuna wa kuhoji wala kuzuia.

Watanzania wenye dhamira njema na Taifa letu, waiweke nchi mbele ya vyama vyao, japo jambo hilo halionekani kutokea hivi karibuni kwa sababu wengi, hasa waliopo madarakani wamejaa ubinafsi na tamaa ya madaraka. Na Rais juzi ametamka kuwa tatizo ndani ya Serikali yake ni uchaguzi wa 2025. Rais anawaza 2025, mawaziri wanawaza 2025, wabunge wanawaza 2025, n.k. Wote wanawaza madaraka, wanawaza vyeo, wamejaa ubinafsi wa kuamini kuwa wao ni lazima wawe na vyeo.

Japo viongozi wetu wamefumba macho na masikio, lakini ni muhimu tuendelee kupiga kelele.

Mod - Tafadhali isomeke CCM ni Doa Jeusi ...
 
Hakika CCM ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu, kuanzia uchumi, demokrasia na haki za watu. Hakuna wanachojali zaidi ya ubinafsi wa madaraka.
 
Kwa ujumla, CCM kwa sasa, mambo mengine yote ni ziada. Kikubwa wanachoangalia ni kuendelea kushika madaraka, iwe kwa haki au dhuluma.

Na hali hiyo inatokana na aina ya watu ilio nao. Rais, yupo tayari kufanya chochote ili kuendelea kuwa Rais. Waziri yupo tayari kufanya chochote alimradi abakie kuwa waziri. Mbunge/diwani yupo tayari kufanya uchafu wa aina yoyote kuhakikisha anaendelea kuwa mbunge/diwani.

Una kundi kubwa ndani ya CCM, ambao wapo tayari kufanya uchafu wa kila aina ili kuwa madarakani. Hili kundi katika level ya juu, ndiyo chama chenyewe. Kama chama kina watu ambao maslahi yao binafsi yapo mbele ya kitu chochote, itawezekana vipi chama kiweke maslahi ya nchi au maslahi ya umma mbele ya maslahi binafsi? Kwa vyovyote haiwezekani.
 
CCM ni takataka!Angalia hapa huyu anaeutaka usipika wa Bunge👇😁😁😁
 
Back
Top Bottom