CCM ndiyo inayopingwa na siyo Serikali.

Huwezi ukaitenganisha CCM na serekali,serekali ni ya CCM wananchi tunapakaziwa,ndio maana CCM wanasikilizwa na serekali kuliko wananchi tunavyosikilizwa,wananchi tunasikilizwa pale wanapotaka kututumia kwa manufaa yao.
 
Kwani Serikali na CCM kilianza nini?
Serikali ilikuwepo hata wakati wa Mkoloni TANU wakaomba ridhaa UNO kwa niaba yetu. kuiongoza serikali.

Hivi Vyama vya Uhuru vimejisahau kabisa na vinafikiri hawa Wananchi ni wa wale wale wa 60s.

CCM, ZANU PF, ANC, FRELIMO, vitafuata mwendo wa UNIP KANU na UPC nk.
 
Tunapoizungumzia CCM ni kumaanisha mkutano mkuu wa CCM ambao ndio kikao cha juu zaidi cha kupitisha maamuzi,,,kikao hiki wajumbe wake wengi sio sehemu ya serikali...hata hivyo mara nyingi kama sio mara zote maamuzi ya wajumbe hawa hutegemea zaidi kupisha yale yaliyopitishwa na halmashauri kuu ya CCM ambayo wajumbe wake wengi ni sehemu ya serikali...

Kwa kumalizia tu ni kwamba CCM na serikali ni sawa na familia nyumani ambayo baba na mama ndio halmashauri kuu na mkutano mkuu ni pale kikao kikijumuisha na watoto.
 
...hata hivyo mara nyingi kama sio mara zote maamuzi ya wajumbe hawa hutegemea zaidi kupisha yale yaliyopitishwa na halmashauri kuu ya CCM ambayo wajumbe wake wengi ni sehemu ya serikali..
Serikali siyo CCM na Wala CCM siyo Serikali.

Huo ndiyo ukweli.
 
Serikali siyo CCM na Wala CCM siyo Serikali.

Huo ndiyo ukweli.
Ni kweli katika maandiko ndivyo ilivyo ila kiuhalisia haiko hivyo..

Mwenyekiti wa CCM ndio kiongozi mkuu na msemaji mkuu wa vikao vya juu vya CCM na ndiye rais wa nchi.

wabunge na mwaziri ni mojawapo ya wajumbe kwenye vikao vya juu vya CCM.

kwahiyo sio tu CCM ndio serikali lakini pia ndio bunge kama tu wabunge wengi watakua wanatoka CCM.
 
Back
Top Bottom