CCM nasi hakuna kulala

CCM nasi hakuna kulala

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tutalinda kura zetu katika Kata zote 26 (tukiiacha Mtae ya kule Lushoto). Tunaamini kuwa tutashinda kwa ushindi wa kimbunga katika Kata fulanifulani.Si zote.Zote haiwezekani.Lakini,tutashinda Kata nyingi-hasa za mkoa wa Pwani na Kusini.Na zile za vijijini mno.

Kule ambapo bado tunapendwa.Kule ambapo bado wananchi ni 'wetu'. Kule ambapo wananchi wanaamini kuwa Wajumbe wa Nyumba Kumi wana mamlaka kiserikali. Kule ambapo chopa za CHADEMA hazijafika au hazijafika mara nyingi.Kule ambapo tunaweza kusema na wanachi wakafanya bila kuhoji. Mahali pale ambapo kura zahesabiwa na pande nyingi zikiwa na lengo la mshindi yule yule.

Nasi leo hatulali.Tumepewa kazi ya kulinda kura zetu. Zisiibwe. Mimi naelekea Kata ya Magomeni Bagamoyo kwa shughuli za ulinzi. Nitakaa mita mia moja toka mlango wa kituo cha kuhesabia kura.Leo hatulali wala kusinzia. Tunataka ushindi.Tunataka kuendelea kuendelea kushika hatamu. Madaraka matamu jamani. Si rahisi kuyaachia.

Twende kazi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Unahangaika kweli.. Njaa mbaya mno. Nashauri tusitumie vichwa kufuga tu nywele
 
Hangaika sana kujishebedua ila ccm ni kama katapila, itazoa kata zote 27. Mtalia na kusaga meno mchana kweupe
 
Ndugu ifweero hauko sawa Kada mwenzangu. Si wewe uliyeweka bandiko muda si mrefu unadai CCM tutashinda kata 25? Mbona hapa wasema 27 tena? Hauko sawa Mkuu.Nyinyi ndiyo mnaofanya chama kidharaulike. Kuweni makini bwana

Mzee Tupatupa wa Lumumba

Last edited by a moderator:
Toka lini wewe ukawa ni mwanaCCM?.

Mambo ya ngoswe mwachie ngoswe kinyume cha hivyo ni kuzidi kuonyesha unafiki na ufitini kwa kuwaaminisha wanaJf wasiokufahamu kuwa wewe ni CCM.

Hivi watu kama wewe huwa mnafaidika nini na kuwalaghai wanaJfi kila siku hapa kwenye jukwaa la siasa.

Huu mwendekezo wako wa kuwadharau wanaJf usidhani hauna malipo huko mbeleni. Kuna siku the law of karma will take its course.
 
Mzee Tupatupa ndiye gamba mwenye akili timamu pekee humu Jf wengine wote ni mizigo tu kama Sam Luhanga.
 
Tutalinda kura zetu katika Kata zote 26 (tukiiacha Mtae ya kule Lushoto). Tunaamini kuwa tutashinda kwa ushindi wa kimbunga katika Kata fulanifulani.Si zote.Zote haiwezekani.Lakini,tutashinda Kata nyingi-hasa za mkoa wa Pwani na Kusini.Na zile za vijijini mno.

Kule ambapo bado tunapendwa.Kule ambapo bado wananchi ni 'wetu'. Kule ambapo wananchi wanaamini kuwa Wajumbe wa Nyumba Kumi wana mamlaka kiserikali. Kule ambapo chopa za CHADEMA hazijafika au hazijafika mara nyingi.Kule ambapo tunaweza kusema na wanachi wakafanya bila kuhoji. Mahali pale ambapo kura zahesabiwa na pande nyingi zikiwa na lengo la mshindi yule yule.

Nasi leo hatulali.Tumepewa kazi ya kulinda kura zetu. Zisiibwe. Mimi naelekea Kata ya Magomeni Bagamoyo kwa shughuli za ulinzi. Nitakaa mita mia moja toka mlango wa kituo cha kuhesabia kura.Leo hatulali wala kusinzia. Tunataka ushindi.Tunataka kuendelea kuendelea kushika hatamu. Madaraka matamu jamani. Si rahisi kuyaachia.

Twende kazi

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Acha ushamba wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom