Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Ni kawaida watu kufurika ili kuwaona "wezi".
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.
Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.
watu wa mkoani ni wapenzi wa sikukuu, na sikukuu ya kuzaliwa kwa ccm nayo ni same kama sikukuu zingine, kwa hiyo kwa upande mwingine ni nafasi ya kupata mtoko na mapumziko kwenda kuona ngoma n.k
haimaanishi kuwa wanaipenda sana ccm, kwanza hapo wengi pia wametoka nje ya kgm
CCM walisoma alama za nyakati. Waliona wakifanya maadhimisho yao zaidi ya jumapili watakosa wale watu waliowatoa Kasulu, Manyovu na Uvinza (na uswekeni-yaani nje ya mji wa Kgm wenyewe) kwani tarehe 5 ilikuwa inaangukia siku ya kazi! Si mnaona jinsi walivyocheza karata zao za magamba na ufisadi? Ila nyakati za kutema karanga kwa bigijii za kuonjeshwa zimeshapitwa na wakati, Linex mwanamuziki maarufu wa Kigoma ameimba hivyo! au vipi jamani.
Toka lini sikukuu ya kuzaliwa CCM ikawa kama sikukuu zingine. Mimi nilikuwa nafikiri baada ya nchi kuingia multiparty, hii kitu ilifutiliwa mbali. Mimi nadhani ilikuwa ni normal Sunday.
Kwa maelezo yako inaonyesha unasimama na hii dhana ya kwamba uwingi wa watu kwenye mikutano ya kisiasa siyo kigezo cha chama kukubalika. Kitu ambacho hata mimi nilikuwa nafikiri hivyo.
Mkuu hiyo ni hela imetumika kujaza watu hapo kuna Rafiki yangu wa Karibu mhasibu wa ccm amendokezea hii kitu imekula zaidi ya milioni 500
nimezungumzia mtizamo wa watu wa mkoani, wewe mzaliwa wa mjini nini! watu wanavaa wanaenda kusherehekea sabasaba, sikukuu ya wakulima n.k huku dar umeshaona watu wanamind kivile?