CCM Na Zuzuka La 'Umati' Kigoma

CCM Na Zuzuka La 'Umati' Kigoma

Kinana: Sasa tutulie tumsikilize mwenyekiti wa taifa
Watu: Tunataka Diamondddddddddddddddddddddddddddddddddddddddddddd
M/kiti: Acha tupige maneno kwanza ,tutaselebuka baadaye
 
Hivi siku zote alizokaa kinana kigoma tembo wetu wako salama kweli???? WATU WALIKUJA KUMWONA DIAMOND PLATINUM KITU CHA M4C NI KAZI TU HAKUNA KIDUKU WA SEGERE YA MSOGA!!!!!!!!1
 
Zitto alipoenda Kigoma kuzindua Leka dutikite alijaza uwanja mara mbili ya hapo na idadi ya watu waliokaa nje ilikuwa ni mara mbili ya waliopata nafasi ya kuingia ndani, ikumbukwe wote unaowaona hapo sio kwamba wamefuata sherehe hizo kuna walienda kmwona Diamond wakidhani ataimba Leka dutikite na zaidi na zaidi unaambiwa mshiko na mabasi vimetembea balaaaa.

Nilikuwepo,wengi walikuwa niwatoto wadogo nawengine walifuata mziki lakini zaidi kabisa niwale walioletwa kwamabasi kwa kukusanywa toka wilaya zote za mkoa pamoja na nchi jirani na mikoa jilani
 
Zitto kaandika ktk twitter kuwa wakati anakwenda Kasulu amekutana na mabasi yamejaza magamba yanakwenda Kigoma, sasa hayo ni sehem tu, je, mangapi ambayo yamesafirishwa?

Kwani ile treni iliyobeba Magamba mengine toka Dar mmeshaisahau! Kama yaliweza kubeba watu kwa treni toka Dar, je kwa mikoa na wilaya za jirani si yatakuwa yamebeba mpaka Mbwa!
 
Hapa ndo napochoka na siasa ya nchi yetu... Utakuta malofa wenzetu wakipewa Pilau, kofia,vitenge na mashati wanasahau kila kitu.

Kwa hali hii naona itakua ngumu CCM kung'olewa 2015

Sent via EyePhone
 
ili ujue huu ni umati uliokusanywa kwa kutumia gharama kubwa, angalia uwanja mzima wamevaa nguo za kijani, ikiwa tu watanzania kununua nguo za kawaida ni tatizo, hayo magamba ya CCM wangeyanunua kwa pesa gani?
 
Pamoja na kuweza kukusanya umati huo fedha iliyotumika ni ile inayotolewa na walipa kodi na ktafunwa na hao magamba. Imekula kwetu tunaolala hoi na kulipa kodi left, right and centre.
 
Umati hii umefuata burudani, full stop. kuna jambo jingine ambalo linanikera sana. Huu utamaduni wa vyama wa kuendekeza sana "sare za chama' unakera sana, na ndio unaotugawa na kufanya siasa iwe kama vita. Magamba unakuta yapo mbele kwenye kijani njano, magwanda na wengineo na sare zao. Napendekeza CDM mkishika madaraka ya nchi hii mpige ban huu utaratibu, unatumia fedha nyingi sana ambazo zingetumika kwenye shughuli za maendeleo kwa ajili ya sare! Mbona siijui sare ya Republican au Democrat vya Marekani?!
 
sherehe za miaka 36 ya CCM zafana sana mjini Kigoma leo

Ndugu yangu Do not read too much katika hadhara hiyo kubwa!! Hakuna kitu kinachoweza kupendwa au kuchukiwa na watu wote; kwa wakati wote! na wala hadhara hiyo haiwakilishi asilimia 100 ya wakazi wa Kigoma; la hasha!!!

CCM ina die hards wake; wazee na walalahoi waliokata tamaa; na Vyama mbadala (Sio Upinzani!) vina watu wake hasa kizazi kipya na wasomi.

Sasa basi ukizingatia kwamba life is so boring in Kigoma; hiyo shughuli ilikuwa ni outing of the decade, Kigoma hakuna mpira wa daraja la kwanza, bendi kubwa kubwa haziendi Kigoma mpaka Zitto ahamasishe matamasha! watu wa Kigoma hawajamuona Raisi wao tangu 2010 wakati wa uchaguzi wa kampeni na isitoshe matarajio ya umma kwa JK kumwaga ahadi zisizotekelezeka lukuki ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwafanya wanakigoma kufurika uwanja wa tanganyika pasipo manufaa ya kisiasa kwa CCM.

Wakumbuke kuwarudisha kwao watu waliosafirishwa toka mbali,wasijewatelekeza kama mwaka jana hapa Mwanza.Watu walitolewa Geita na Shinyanga,wakalishwa nyama ili kujaza uwanja kisha wakatelekezwa.Najua wengi walienda kuona ngoma ya kirundi ndo maana hata mnaoleta taarifa hamtuambii ni masuala gani yalizungumzwa zaidi ya kutuambia JK ameburudika na ngoma za asili huku vyombo vikimgomea Diamond.Kama ni reli bado safari siyo kila siku kama zamani,isitoshe mliua wenyewe sasa hapo habari ni ipi?
 
Safi sana!! Jamaa wanalia,, wako tayari kuita nyekundu wakati wanaona kabisa ni kijani. Jamaa wanakimbia kivuli chao! Wao wakijaza mikutano hawakawii kuleta picha hapa,, leo CCM wamejaza Kigoma nongwa! hawa watu hawa! ni wa kuogopa kama ukoma

Cdm hawajawahi na hawako tayari kujaza watu kwa kuwafata lusesa,uvinza,kasulu,kibondo nakwingine kwa kuwapelekea pesa na usafiri na kuwaleta sehemu yamkutano nadhani unalijua hilo,pia kwa ushahidi kuna mke wa uncle wangu katolewa kijijini kuja kgm mjini kwa bus na kapewa elfu 15 akaona aibu kufikia kwangu akaenda kulala nawenzie kwenye vi guest vyauswahilini.Kaniambia mwenyewe baada yakuja kunisalimia home!
 
Kwani ile treni iliyobeba Magamba mengine toka Dar mmeshaisahau! Kama yaliweza kubeba watu kwa treni toka Dar, je kwa mikoa na wilaya za jirani si yatakuwa yamebeba mpaka Mbwa!

Nikweli kamanda uwanja jana 78% walikuwa niwageni toka sehemu mbalimbali,guest zimejaa nawengine wamekosa pakulala kiasi cha kulala kwa watu kwa kulipa kama lodge!
 
nashangaa unashindwa kufikiria kuwa watu wale walijaa kwa sababu ya Diamond, na sio CCM, tulishawahi kufanya sherehe ya siku ya UKIMWI Duniani Kigoma na tulitangaza Comedy watakuwepo, uwanja ulifurika mno mpaka watu wakazuiliwa getini, ina maana walijaa kwa sababu ya mgeni rasmi?

Kwa nini Diamond alipomaliza kutumbuiza hawakuondoka kama hiyo ndiyo sababu maridadi. Siasa za Tanzania ni zaidi ya tumbuizo la wanamusiki kwenye mikutano ya kisiasa. Nitashangaa kama kigezo cha kuwa na 'UMATI' wa watu katika mikutano ushindi.
 
Ndugu yangu Do not read too much katika hadhara hiyo kubwa!! Hakuna kitu kinachoweza kupendwa au kuchukiwa na watu wote; kwa wakati wote! na wala hadhara hiyo haiwakilishi asilimia 100 ya wakazi wa Kigoma; la hasha!!!

CCM ina die hards wake; wazee na walalahoi waliokata tamaa; na Vyama mbadala (Sio Upinzani!) vina watu wake hasa kizazi kipya na wasomi.

Sasa basi ukizingatia kwamba life is so boring in Kigoma; hiyo shughuli ilikuwa ni outing of the decade, Kigoma hakuna mpira wa daraja la kwanza, bendi kubwa kubwa haziendi Kigoma mpaka Zitto ahamasishe matamasha! watu wa Kigoma hawajamuona Raisi wao tangu 2010 wakati wa uchaguzi wa kampeni na isitoshe matarajio ya umma kwa JK kumwaga ahadi zisizotekelezeka lukuki ni baadhi ya mambo yanayoweza kuwafanya wanakigoma kufurika uwanja wa tanganyika pasipo manufaa ya kisiasa kwa CCM.

Mimi ninakubaliana na maneno yako haya, lakini kitu kinachonishangaza ni hii dhana ya watu kuwa na zuzuka la kuona UMATI katika mikutano yote ya kisiasa bila kujali kama ina impact kwenye ujumbe wake. Kila mara hapa janvini utasikia wanajanvi wanaomba picha kwa kile yule anayeleta habari za mikutano ya kisiasa.

Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.

Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.

Kama MAGAMBA walialika Mpaka ngoma kutoka Burundi na huyo Diamond ulitegemea watu wasije kuburudika?? Hawakuja kushabikia CCM ila kuburudika na kuwashangaaa Mafisadi
 
Kama MAGAMBA walialika Mpaka ngoma kutoka Burundi na huyo Diamond ulitegemea watu wasije kuburudika?? Hawakuja kushabikia CCM ila kuburudika na kuwashangaaa Mafisadi

Kwa nini kama watu huwa wanakuja kwa ajiri ya burudani na wengi wanajua hivyo, mbona watu wengi hapa huwa na zuzuka la kuomba picha za UMATI wa watu waliohudhuria mikutano ya kisiasa. Inaonekana kama kipimo cha siasa ni UMATI na siyo ujumbe kwa jamii.
 
Maazimisho ya mwaka jana ya CCM (36) katika viwanja CCM Kirumba, Mwanza, pamoja na CCM kusomba wanachama wake kutoka katika wilaya zote za Mwanza. Pia walikwenda Serengeti National Park kuwinda nyumbu kwaajili ya kitoweo cha halaiki ya watu waliowasomba mawilayani.

Lakini kikubwa waliwinda nyumbu bila kupata kibali, huo ulikuwa UFISADI mwingine ambao umezimwa kimya kimya na ofisa wanyamapori wa MZA
 
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.

Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.

huo umati walikuja kwa ridhaa yao au waliweshwa?
 
huo umati walikuja kwa ridhaa yao au waliweshwa?

Katika Tanzania, watu ambao hupelekwa sehemu bila ridhaa yao ni wafungwa peke yake. Kama hao walikuwa ni wafungwa basi ninasema hawakuja kwa ridhaa yao.

Napata shida kuelewa maana ya kuwa na UMATI katika mikutano ya kisiasa kwa Tanzania kama watu wengi wanavyopenda kuona na mpaka kufikia hatua ya kusukuma magari ya wanasiasa.
 
Back
Top Bottom