CCM Na Zuzuka La 'Umati' Kigoma

CCM Na Zuzuka La 'Umati' Kigoma

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
sherehe za miaka 36 ya CCM zafana sana mjini Kigoma leo

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia uwanja wa Lake Tanganyika kuhitimisha sherehe za miaka 36 ya chama hicho mjini Kigoma leo

Ngoma za utamaduni zamfurahisha Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Akipungia kwa furaha maelfu ya wananchi wa Kigoma wanaomshangilia kwa nguvu

Licha ya vyombo kukorofisha msanii Diamond nma kundi lake walitumbuiza kwa ustadi

Diamond akipagawisha

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliohudhuria Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Mkoani Kigoma jioni hii.​

Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akisema machache,muda mfupi kabla ya kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani} kuwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii.

Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Harisson Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kigoma jioni hii na kuwahakikishia kuwa sasa hivi mkoa wa Kigoma mambo yako vyema kabisa na treni itaendelea kufanyaka kazi kama zamani.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akiongoza shughuli hiyo.

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Kigoma,wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,kuongoza Maadhimisho ya 36 ya kuzaliwa kwa CCM,Mkoani Kigoma leo.

Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia burudani ya ngoma.

Chipukizi wa CCM Mkoa wa Kigoma wakifanya Gwaride la heshima kwa Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM,yaliyofanyika jioni hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma.

Mtangazaji mkongwe wa TBC Taifa Swedi Mwinyi akiwa hai hewani na wenzie
Katibu Mkuu wa CCM akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Omar Chambo na Maafisa waandamizi wa wakala wa usafiri wa anga
Washindi wa kombe la CCM 2013
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea banda la Uhuru na Mzalendo
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mang'ula akipitia magazeti ya zamani kwenye banda la Uhuru na Mzalendo
Ankal akiwa na wanahabari wa Kigoma
Ngoma toka mkoa wa Makamba nchini Burundi
Wanahabari waliorekodi sherehe hizo kutoka vyombo mbalimbali
Mablogger wakirekebisha mitambo wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia. Kutoka shoto ni Ahmad, Othman, Bukuku, Nkoromo na Mroki

MUHIDIN MICHUZI at Sunday, February 03, 2013

Angalizo:
Nini hasa kigezo kwa chama kukubalika katika jamii ya Kitanzania kama hata chama 'kilichochoka' kuongoza nchi kinapata UMATI wa watu hata kwenye ngome ya vyama pinzani kisiasa.

Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.

Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.
 
Naweza kushangaa kama Ccm hawajaenda na kundi lolote la burudani uwanjani af bado wakajaza watu, huwa sielewi mtu anaposhangaa watu wakiwa wamejaa na ilhali mahali hapo kuna kila aina ya burudani na wasanii maarufu nchini ambao kwa wengi asipotumia hiyo fursa anaweza asiwaone kabisa ktk maisha yake!
Hebu tujiulize wangapi wamekuja kuwaona akina Nape na wangapi wanataka muziki wa akina diamond? Tuache kujifanya akili zimekataa kufikiri! Utashangaaje watu kujaa mahali penye kila aina ya burudani na usafiri wa bure??
 
Zitto alipoenda Kigoma kuzindua Leka dutikite alijaza uwanja mara mbili ya hapo na idadi ya watu waliokaa nje ilikuwa ni mara mbili ya waliopata nafasi ya kuingia ndani, ikumbukwe wote unaowaona hapo sio kwamba wamefuata sherehe hizo kuna walienda kmwona Diamond wakidhani ataimba Leka dutikite na zaidi na zaidi unaambiwa mshiko na mabasi vimetembea balaaaa.
 
Ningetarajia diamond awe kambi ya zitto akitumbuiza kasulu lakini njaa ndo imemfanya kuwa kwa kambi ya magamba
 
Mkuu hiyo ni hela imetumika kujaza watu hapo kuna Rafiki yangu wa Karibu mhasibu wa ccm amendokezea hii kitu imekula zaidi ya milioni 500
 
Ningetarajia diamond awe kambi ya zitto akitumbuiza kasulu lakini njaa ndo imemfanya kuwa kwa kambi ya magamba
Mkuu diamond akiwa kambi ya zitto ataimba nyimbo gani? Au hizo nyimbo zake za kubembelezea uroda?
 
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.

Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.

Jibu kila mmoja wetu analo maana waliojaza uwanjwa wana sare za chama
 
Zitto kaandika ktk twitter kuwa wakati anakwenda Kasulu amekutana na mabasi yamejaza magamba yanakwenda Kigoma, sasa hayo ni sehem tu, je, mangapi ambayo yamesafirishwa?
 
Jibu kila mmoja wetu analo maana waliojaza uwanjwa wana sare za chama

Safi sana!! Jamaa wanalia,, wako tayari kuita nyekundu wakati wanaona kabisa ni kijani. Jamaa wanakimbia kivuli chao! Wao wakijaza mikutano hawakawii kuleta picha hapa,, leo CCM wamejaza Kigoma nongwa! hawa watu hawa! ni wa kuogopa kama ukoma
 
Mbona mambo yapo wazi diamond alishangiliwa kuliko yeyote
 
Wameenda kutazama wasanii na zaidi mpira kwani kulikua kuna final, wakigoma kwa soka ndo wenyewe!
 
Kwa Watanzania wengi, picha ni ujumbe kisiasa, na ujumbe chanya au hasi una shadadiwa na UMATI wa watu shiriki katika mikutano ya kisiasa. Hii ya CCM sijui katika fikra hizo inatoa ujumbe gani, hasa ikizingatiwa hiyo ni "ngome" ya vyama vingine vya kisiasa huku kikiwa 'kimelemewa' na zigo la kiuongozi na kiutawala nchini.

Sina budi kukubaliana na wale wanaopatwa na sindiko la moyo pale matokeo ya chaguzi yanapokuwa vinginevyo kwa kutumia dhana ya UMATI katika siasa za Tanzania.

nashangaa unashindwa kufikiria kuwa watu wale walijaa kwa sababu ya Diamond, na sio CCM, tulishawahi kufanya sherehe ya siku ya UKIMWI Duniani Kigoma na tulitangaza Comedy watakuwepo, uwanja ulifurika mno mpaka watu wakazuiliwa getini, ina maana walijaa kwa sababu ya mgeni rasmi?
 
Hivi CCM ilizaliwa lini? Kwa nini hizi sherehe zimefanyika jana? Mimi nafikiri CCM ilizaliwa tarehe 5 February? Au wameamua kufanya mapema kwa kuwa ilikuwa ni Jumapili?

Tiba
 
Naweza kushangaa kama Ccm hawajaenda na kundi lolote la burudani uwanjani af bado wakajaza watu, huwa sielewi mtu anaposhangaa watu wakiwa wamejaa na ilhali mahali hapo kuna kila aina ya burudani na wasanii maarufu nchini ambao kwa wengi asipotumia hiyo fursa anaweza asiwaone kabisa ktk maisha yake!
Hebu tujiulize wangapi wamekuja kuwaona akina Nape na wangapi wanataka muziki wa akina diamond? Tuache kujifanya akili zimekataa kufikiri! Utashangaaje watu kujaa mahali penye kila aina ya burudani na usafiri wa bure??

Mimi binafsi ningeenda kuangalia ngoma ya Kirundi kutoka makamba kwani sijawahi kuiona na sina mpango wa kwenda Burundi hivi karibuni.
 
Tiba, sasa unatarajia wangewapataje wafanyakazi wa serikali wakati sikukuu ya kuzakiwa CCM si ya kiserikali?

Hivi CCM ilizaliwa lini? Kwa nini hizi sherehe zimefanyika jana? Mimi nafikiri CCM ilizaliwa tarehe 5 February? Au wameamua kufanya mapema kwa kuwa ilikuwa ni Jumapili?

Tiba
 
Ogopa sana watu wanaojaa kufata burudani na sio ujumbe utakaotoa. Hapo ukiwauliza JK katoa ujumbe gani watakuambia sikumbuki ila Diamond kaimba nyimbo zipi.
Hiyo siku zote ndiyo hasara wanayoipata CCM. Nimewahi kuona mkutano mmoja wa Slaa watu wanasikiliza wameshika tama na kelele unazisikia akisema peoples! Na mkutano haukuwa hata msoma shairi.
Ujumbe ndio muhimu
 
Safi sana!! Jamaa wanalia,, wako tayari kuita nyekundu wakati wanaona kabisa ni kijani. Jamaa wanakimbia kivuli chao! Wao wakijaza mikutano hawakawii kuleta picha hapa,, leo CCM wamejaza Kigoma nongwa! hawa watu hawa! ni wa kuogopa kama ukoma

Pia ukumbuke maandalizi ya mkutano huo yamegharimu mwaka mzima!!!!
 
hakuna free will hapa! Kuna motisha za aina nyingi zimehusika kuwaleta watu hapa uwanjani! Unaweza kuona tu ni wangapi walikuwa wanaitikia vibwagizo vya CCM au Nape nilikuwa nasikiliza kila wakisema CCM Hoyee sauti na shamrashamra zilizokuwa zinatoka uwanjani hazilingani na Umati uliokuwepo. Tofauti siku ya uzinduzi wa leka tutigite ambapo akina Zitto na Nassari walikuwa wakishangiliwa kupita wasanii waliokuja kutumbuiza!
 
Back
Top Bottom