CCM na somo la Ushirika wa Vyama

Nduka

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
8,552
2,359
Wanasema hata saa mbovu kuna muda katika siku huwa inakuwa sahihi, nadhani upinzani hasa CHADEMA wanapaswa kujifunza kwa CCM somo la kushirikiana na vyama vingine.

CCM pamoja na kushika dola, kuwa na rasilimali na uwezo wa kifedha, kuwa na mtandao ulioenea kila kona ya nchi lakini bado wamekuwa wakiheshimu ushirika na vyama vingine.

Bila kujali ukubwa wala udogo wa vyama, CCM wameendelea kuvishikilia vyama rafiki kwao bila kuviacha. Angalia namna TADEA, NRA, CCK na vingine kama hivyo vinavyonyenyekewa na CCM kama vinaweza kuwa tishio kwao.

Viongozi wa vyama hivi wanaheshimiwa na kuthaminiwa na CCM na hata pale panatokea kutokusikilizana basi CCM huwa ndio mstari wa mbele kurudisha mahusiano na hutu tuvyama. Kuna la kujifunza hapa.
 
CCM hata siku moja hawataki uwanja sawa wa kisiasa, wanataka vyombo vyote vya nchi hii viwapendelee. Dawa ni kudai katiba mpya kwa nguvu zote.
 
Magufuli hakukosea kumpangia chalamila kuwa mkuu wa mkoa wa mbeya.

Mikoa yenge idadi kubwa ya wapinzani inahitaji kuongozwa na wanywa bia, wanajua kujichanganya na makundi yote.

Chalamila angekuwa bado mkuu wa mkoa wa Mwanza asingehangaika na kumkamata Mbowe na kumletea mama mkwamo wa kisiasa.
 
CCM hata siku moja hawataki uwanja sawa wa kisiasa, wanataka vyombo vyote vya nchi hii viwapendelee. Dawa ni kudai katiba mpya kwa nguvu zote.
Hata hiyo katiba mpya bila kushirikiana, unawezaje kupata matokeo?
 
Back
Top Bottom