CCM na Rais Magufuli wanatumia ajali ya moto Mororgoro kama mtaji wa kisiasa na wakiwatukuza wahalifu kama mashujaa


KWANI WAO WALIKUWA SIYO WALIPA KODI? WANANCHI KARIBU WOTE WANALIPA KODI. WAO VILEVILE WALIKUWA WANALIPA KODI. KWA HIYO HELA ILIYOTUMIKA NI KODI YAO AMBAYO NI HAKI YAO KUITUMIA. MIMI SIONI HAJA YA KULALAMIKA ETI KODI INAPOTEA BURE. HAWA NI BINADAMU LAZIMA WAZIKWE KWA HESHIMA ZAO, LICHA YA AINA YA TUKIO LENYEWE. NA UMESHAAMBIWA WENGINE WALIKUWA NI WAPITA NJIA. HATA KAMA WOTE WALIKUWA WANACHOTA MAFUTA. HIYO PESA ILIYOTUMIKA NI HAKI YAO. KWANI HELA NI KITU GANI JAMANI. TUWAACHE WAPUMZIKE KWA AMANI.
 
Wewe ulitakaje????
Hujasoma hapo juu?
Sio nilichotaka tu, bali ni kilichostahili kufanywa.

Raisi angetoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kwapa pole wafiwa. Angetamka kwamba serikali itagharamia mazishi ya waliokufa ikiwa hawatatambuliwa na ndugu zao, na kugharamia gharama za matibabu kwa majeruhi.

Na pia angekumbusha Watanzania kwa ujumla kwamba wajiepushe na kujichukulia mali pale ambapo ajali zinatokea, kwa kuwa sio tu sio ubinadamu bali pia ni kitendo cha uhalifu na wakikamatwa watachukuliwa hatua.

Basi, hiyo ingetosha kabisa. Hakuna kutembelea hospitali na kutangaza "nakugawia laki tano ukanunue juice", hakuna kutangaza kujenga mnara wa kumbukumbu.
 
Soma tena uelewe. Hata kibaka aliye gerezani anatumia kodi yangu japo sipendi.
 
Hayo ni maoni yako tu ila kwa wale ambao ndugu zao ni wahanga [wengine walikuwa wala hawahusiki na kugema mafuta] wamefarijika sana. Kwa upande mwingine jee mlitaka serikali isifanye hayo iliyoyafanya ili muilaumu kwa kutofanya hicho walichokifanya?????
 
Sasa hapo ndicho usichoelewa! Sio wamefarijika, bali wameshanunuliwa kisiasa, na ndicho Magufuli alichaotaka! Suala halikuwa kufariji bali kununua watu kisiasa!

Ona hata wewe umeshanunulika, sasa huelewi husikii juu ya Magufuli na CCM yake.

Yaani Watanzania mnanunulika kisiasa kwa pesa ndogo sana na wala hamuoni!
 
Hayo yanabakia kuwa maoni yako. Jee pale alipokuwa anahudhuria maziko ya watu wengine ambao hata siyo wanasiasa, kutembelea wagonjwa hospitalini alikuwa anafanya kampeni???
 
Hayo yanabakia kuwa maoni yako. Jee pale alipokuwa anahudhuria maziko ya watu wengine ambao hata siyo wanasiasa, kutembelea wagonjwa hospitalini alikuwa anafanya kampeni???
Inawezekana kwa kiasi fulani, lakini kama ni kawaida yake kufanya hivyo basi sio kampeni.

Lakini ona kwamba tukio hili la moto ni tofauti, kwa kuwa wahanga wengi ni wahalifu wa mitaani, na ndio wapiga kura walio wengi. Ndio maana nikasema, amelivumisha kuliko inavyostahili kwa kuliona kama fursa ya kisisa. Sisemi aose utu,. la hasha, bali katumia tukio lisilostahili.Utu ulipaswa uonyeshwe kwa salamu za rambirambi na kugharamia matibabu, basi. Lakini kaenda mbali sana katika kuteka mioyo ya vibaka waliobaki.
 
Siasa zimekukolea kiasi kwamba haufikirii sawa sawa na uwezo wako mkubwa wa akili.
Huo mnara unaweza kuwa na majina ya watu waliofahamika wamefariki lakini ndugu zao hawajapatikana.
Ipo siku ndugu wanaweza kujitokeza na kukuta jina kwenye mnara wakathibitisha ndugu yao alikuwamo ktk ajali kisha kuhani walipolazwa ndugu zao.
Siasa za namna hii ni hasara kwa jamii yako.
 
ujue hawa waliopata ajali ya kuungua wanapewa huduma na attention kuliko mtu aliyepata ajali akiwa kataika kazi yake halali.
Japo sio wote walikuwa wakiiba mafuta,
 
Hawawezi kutumia km mtaji hakuna mtaji hapo wa kisiasa. wewe ulitaka watu wasihudumiwe hilo lilikuwa ni janga la Taifa na huo ndio wajibu wa serikali zote duniani
 
Majina ya vibaka wengi waliokufa wakiiba mafuta huku wakimwacha bila msaada dereva wa lori lililopata ajali
 
Hawawezi kutumia km mtaji hakuna mtaji hapo wa kisiasa. wewe ulitaka watu wasihudumiwe hilo lilikuwa ni janga la Taifa na huo ndio wajibu wa serikali zote duniani
Sijasema popote nilitaka wasihudumiwe. Nimesema tukio linatumiwa kisiasa. Hivi nyie CCM mmenda shule lakini? Kwa nini mnashindwa kuelewa insha fupi namna hii?
 
Kaka watu hao kwa sasa ni marehemu na sisi tumekatazwa kuwahukumu wakiwa kwenye hali hiyo kwani hakimu mkuu ndiye watakaekutana naye siku ya mwisho.
Jukumu letu sisi ni kuwastiri kwa kuwazika kwa heshima ambayo kila binadamu anastahili kufanyiwa akifariki.
 
Yaani ukisoma kwa makini nilichaoandika, utaona nakubalina na uliyosema hapa kwa 100%. Lakini utakaposoma kwa umakini zaidi, utaona ninachokataa.
 
Yaani hii mada ya huyu mpumbavu tangu jana badomnaisumbukia na alaaniwe huyumtoa mada hafai na siyo raia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…