CCM na Rais Magufuli wanatumia ajali ya moto Mororgoro kama mtaji wa kisiasa na wakiwatukuza wahalifu kama mashujaa

Yaani kama CHADEMA wamekutuma uchafue hali ya hewa umeshindwa huna huruma hata kidogo hivi chadema huwa mnachamaana kweli? akikaa kimya mnaongea vibaya akisaidia pia mnaongea vibaya mnataka afanye nini kilakitu nyie mnaona kibaya hamna sera bora mjikalie kimya kuliko kuendelea kuropoka kama yule mpumbavu wenu lissu anaeropoka mhovyo huko aliko hamna huruma mbwa nyie
Kabla ya awamu ya 5 nilikua sitaki hata kusikia CCM. Lakini Magu akabadilisha hali ya hewa sijui nisema CCM au uongozi wa serikali, nikadhani wapinzani watakuja na sera nzuri zaidi, yani zaidi ya sera waliokua nao hapo awali lakini imekua kinyume hatimae tunaona, tuna sikia na tunasoma kila siku maneno yao yasio kua na kichwa wala miguu, yaani maneno ya chuki na chuki. Mleta mada anaonyesha chuki yake kupitia hao waliokufa na waliojeruhiwa. Amewaweka wote kwenye kundi la uhalifu, ebufikiria atajisikiaje yule alienda kukimbilia pale ili asaidie na leo yuko mahtuti hospitali au yule aliempoteza ndugu yake ambaye alikua mpita njia.
Alicho andika huyu mtu kinatia kichefuchefu.
Mungu awerehemu wote waliopoteza maisha na awape awape unfuu waliokua kitandani na maumivu. Na mungu Pia atuepushie ajali Kama hizi.
 
Kiutaratibu rasmi wa kisheria, sawa.

Lakini, ikitokea umefua nguo zako na kuzianika uani kwako [line drying] halafu unaona mtu ambaye humjui anakuja kwa kunyata halafu anaanua mashati mawili matatu, hapo vipi?

Huyo hatakuwa mwizi mpaka mahakama impate na hatia ya kukuibia nguo?
Ndiyo maana niliepuka mambo ya kuanika nguo, basement kuna washing machine na dryer. Haahaa.

On the real, unatakiwa kuchukulia kwamba anything is possible, pengine ni kichaa.

Unamkamata na kumripoti vyombo vya sheria vimfanyie utaratibu wa kisheria.

Unaweza kukuta ni muathirika wa madawa ya kulevya, madawa yamemuathiri akili, ni muhanga, si muhalifu.

Kuna movie moja classic, inaitwa "12 Angry Men", ilitoka mwaka 1957 na inachukuliwa kwamba ni moja ya movie kali kabisa katika movies za sheria, inahusu jury ambayo ilianza deliberations ikiwa ina uhakika kwamba case ni slam dunk conviction, juror mmoja akaanza kuonesha doubt, hatimaye akapindua maoni ya jurors wote.

Ukiangalia movie ile utaona umuhimu wa "presumption of innocence".

 
Ndiyo maana niliepuka mambo ya kuanika nguo, basement kuna washing machine na dryer. Haahaa.

On the real, unatakiwa kuchukulia kwamba anything is possible, pengine ni kichaa.

Unamkamata na kumripoti vyombo vya sheria vimfanyie utaratibu wa kisheria.

Unaweza kukuta ni muathirika wa madawa ya kulevya, madawa yamemuathiri akili, ni muhanga, si muhalifu.

Hahahaaa. Mimi nikimkamata ni kibano tu.

Sina muda wa kuanza kuwaza kama ni kichaa au la.

Vipi jambazi atayevunja mlango wa nyumba yako akiwa na silaha kwa lengo la kupora mali zako?

Naye utamchukulia hana hatia hadi mahakama impate na hatia?
 
Ukitizama kwa haraka unaweza kuona uhalifu, lakini ukiwa makini zaidi utaona umasikini. Umasikini wa Tanzania ni zao la CCM. Ni mtaji wa kisiasa. Kwa hivyo, kwa serikali kufanya hicho inachofanya sasa, ni namna ya ku accept responsibility yao (chanzo cha umasikini ni wao).....mimi nawaunga mkono, kiroho safi tu.
 
Kufa kufaana, yaliyotokea tumuachie Mungu yeye ndo atajua, sisi hatuna tuliwezalo, lolote na wakati wowote laweza kukuta yeyote na popote pale, si wote walio poteza maisha pale walikuwa na nia ya kupata mafuta na hata kama walikuwa na nia hiyo ila sisi sote hatuna utimilifu kwani kila jambo linapotokea kwetu huwa tunaona ni fursa,maofisini na sehemu zingine,
 
Hahahaaa. Mimi nikimkamata ni kibano tu.

Sina muda wa kuanza kuwaza kama ni kichaa au la.

Vipi jambazi atayevunja mlango wa nyumba yako akiwa na silaha kwa lengo la kupora mali zako?

Naye utamchukulia hana hatia hadi mahakama impate na hatia?
Kuna tofauti kati ya mfumo wa nchi nzima na matendo ya taasisi ya urais, na mambo ya mtu mmoja.

Mimi naweza kumchukulia jambazi kwamba jambazi, nikamuua, nikatetewa na sheria kwamba nimemuua wakati nimeingiliwa nyumbani kwangu, kwa self defense.

Magufuli anapoongelea watu kibao waliofariki katika moto, kisiasa, kiutu na kisheria ni sawa kuwachukulia watu waliokufa hawana hatia.

Kisiasa katika msiba kuanza kusema hawa watu waliokufa ni wezi its very awkward, unaonekana unsympathetic, na zaidi, inawezekana kuonekana yeye rais ndiye katengeneza mfumo unaofanywa watu wawe wezi wa mafuta kiasi cha kuhatarisha maisha yao, tena wezi na wajinga.

Kisiasa na kiutu inabidi akubali tu kwamba hapo wamechanganyika watu wengi, wezi na wengine wengi tu wasio wezi, na kwa sababu hiyo, kuanza ku distinguish nani mwizi na nani mdadisi au mjinga tu, ni kazi ngumu, tuwachukulie kama si wezi tu, kwanza ushahidi wote ushaunguzwa moto na hauna chain of custody ya kueleweka, sasa utaanzaje kusema nani mwizi na nani mdadisi na nani mjinga na nani alikuwa anahimiza watu waondoke sehemu hiyo?

Kisheria, mahakama ndiyo ina jukumu la kutuambia nani mhalifu, na kama rais kakataa kuwaita watu wahalifu kabla ya mahakama - rais mwenye kimbelembele sana cha kusema ovyo- mimi namshukuru na kumpongeza kwa hilo. Ningemtaka afanye hivyo zaidi na zaidi.
 
Inaudhi sana kusoma ujinga kama huu moderators naninyi mjipange,ndomana watu hutekwa na kutandikwa vizuri huwezi kumkashifu rais kiasi hiki kwa akili za kipuuzi. Waliokufa walilidondosha wao hilo Lori? Tumetoka maombolezo kama taifa sikutatu kuwaombea waliotutangulia wajinga kadhaa wanajitokeza kukashifu vibaya wanaotenda ubinaadam. Hivi nduguyo/mtoto wako yangemkuta usingemzika? Poor stupid little brain...
 
Kuna tofauti kati ya mfumo wa nchi nzima na matendo ya taasisi ya urais, na mambo ya mtu mmoja.

Mimi naweza kumchukulia jambazi kwamba jambazi, nikamuua, nikatetewa na sheria kwamba nimemuua wakati nimeingiliwa nyumbani kwangu, kwa self defense.

Magufuli anapoongelea watu kibao waliofariki katika moto, kisiasa, kiutu na kisheria ni sawa kuwachukulia watu waliokufa hawana hatia.

Kisiasa katika msiba kuanza kusema hawa watu waliokufa ni wezi its very awkward, unaonekana unsympathetic, na zaidi, inawezekana kuonekana yeye rais ndiye katengeneza mfumo unaofanywa watu wawe wezi wa mafuta kiasi cha kuhatarisha maisha yao, tena wezi na wajinga.

Kisiasa na kiutu inabidi akubali tu kwamba hapo wamechanganyika watu wengi, wezi na wengine wengi tu wasio wezi, na kwa sababu hiyo, kuanza ku distinguish nani mwizi na nani mdadisi au mjinga tu, ni kazi ngumu, tuwachukulie kama si wezi tu, kwanza ushahidi wote ushaunguzwa moto na hauna chain of custody ya kueleweka, sasa utaanzaje kusema nani mwizi na nani mdadisi na nani mjinga na nani alikuwa anahimiza watu waondoke sehemu hiyo?

Kisheria, mahakama ndiyo ina jukumu la kutuambia nani mhalifu, na kama rais kakataa kuwaita watu wahalifu kabla ya mahakama - rais mwenye kimbelembele sana cha kusema ovyo- mimi namshukuru na kumpongeza kwa hilo. Ningemtaka afanye hivyo zaidi na zaidi.

Kuhusu wahanga wa ile ajali, Rais Magufuli yupo sahihi.

Hilo mimi nililisema majuzi.

Na kwa mtu yeyote mwenye busara tu za kawaida [common sense] hawezi kuhitimisha kuwa wote waliokumbwa na huo mkasa kuwa ni walikuwa wezi wa mafuta.

Na katika mazingira yale, ni vigumu kujua nani alikuwa mwizi, nani alikuwa mpita njia, nani alikuwa innocent bystander, nani alienda kwa lengo la kusaidia, na kadhalika.

Mazingira ya ile ajali hayaruhusu kutoa mahitimisho ya jumla jumla bila kufanya uchunguzi yakinifu.

Hilo sina ubishi nalo kabisa.
 
Yaani ndiyo maana siwapendi wapinzani kwaajili ya akiliyao mbovu kama mtoa mada hivi wewe ni binaadamu wa kawaida kweli au hiyo CHADEMA yako ndiyo inakufundisha uwe na roho mbaya kiasi hicho halafu mnakuja kutuomba muongoze nchi watu wenye rohombaya kama yako wewe?

Maneno hayo kamwambie tundu lissu wenu huko siyo mnatuletea huku sisi tuko kwenye majonzi ya msiba huna huruma kabisa
Nimehuzunika sana unapokwepa point na kwenda kwenye hoja mufilisi. Jitahidi kuyakumbauka majanga yaliyoipata nchi tangu 2015. Je mh alienda huko hata kuwaona?? Tetemeko la Bukoba, Boti la kule Ukerewe, Boti za Zenj?? Mbona mna kawaida ya kufunika mambo?? Kinachoombwa hapo ni; Mzee asiwe na double standards tu si kingine. Atawaumiza wengi sana. Michango ilitolewa kwenda Bkb na kwingineko ila ikapangiwa mambo mengine ya ujumla. Sasa hili limekaaje??
 
Mimi nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa kwa kuwaambia ukweli....

Kwenye ishu ya Rais kugawa pesa, mimi hapo ndipo nilipoona anafanya fyongo kuliko kawaida.....

Ulichoshauri mwishoni, ndiyo hasa sahihi alichopaswa kufanya Rais siyo namna ile ya kugawa fedha kama yule msanii alivyotupia waandishi wa habari minoti na wao kuanza kugombania kama watoto wadogo....

Na nadhani kuna kitu hakiko sawa kwa Rais Magufuli na mtazamo wake kuhusu fedha na namna njema anavyoweza kuzitumia kama kiongozi mkuu wa nchi......

Katika awamu zote ya 1, 2, 3 na 4, huyu jamaa kwenye fedha nadhani ana tatizo fulani....

Anazitukuza, kuziabudu na kudhani zinaweza kumpa na kumfanyia chochote akitakacho such as to boost up his self - pride, egoism, popularity and so forth....

Huyu bwana ukimchunguza, utagundua kuwa, he's even ready to kill just for money, power and political popularity!!

Wanaodhani kuwa Magufuli kupita anagawa pesa kama njugu barabarani kwa kigezo cha "kuonesha utu/kujali", inaonesha ni kiongozi wa kipekee, wameliwa kifikra na kiufahamu, hawajui kilicho nyuma ya matendo hayo....!!

Huko ni kujikweza, misaada haitolewi kwa namna anavyofanya hususani kwa kiongozi wa nafasi yake.....

Na tusidhani kuwa maRais waliopita Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete hawakuwa na moyo wa kusaidia watu....

They were, lakini hawakuwa wanafanya kwa ajili ya show - off kuonesha self-pride...

Afanyavyo Magifuli, ni copyright tabia za viongozi wa dizaini ya IDD Amin Dada, Mobotu Seseseko, Adolf Hitler, Benito Mussolini na wengine wafananao na hao....

Walivaa ngozi za kondoo nje, lakini ndani walibeba roho halisi ya fisi na mbwa mwitu wakali.....!!
 
Ukisema hivyo unakosea sana...

Sababu pesa yako hiyo hiyo ya kodi pia inalisha wafungwa magerezani tena wengine wenye kesi za kubaka na mauaji, hujaliona hilo...

Hao sii wahalifu na wala hawakusimama barabarani na kupora, bali walikua wanazoa kilochokua kinamwagika baada ya ajali...


Cc: mahondaw
 
Mkuu umeandika maneno mengi sana, na nakiri nakubaliana na mengi ya uliyosema. Hata hivyo, umeenda nje sana ya mada yangu.

Mimi sijasema ni vibaya kuwa na utu kwa mtu aliyekufa, bila kujali sababu. Sheria za duniani zinataka kuwa na utu hata kwa majeruhi au maiti ya askari adui wakati wa vita, sembuse kibaka wa kuba mafuta ya gari lililopata ajali?

Na pia ni vema ukumbuke kwamba hawa vibaka waliokufa Morogoro kwanza wao pia hawakuwa na utu. Kumbuka hawakujali kutoa msaada kwa dereva wa gari aliyekwama ndani ya hilo lori bali walikimbilia kujipatia mafuta. Kuna mtu mmoja tu ndie alienda kutoa msaada japo na yeye pia alikufa. Kwa hiyo basi, najua kuna innocent victims kama huyu aliyekufa akijaribu kumwokoa dereva.

Lakini sasa, asilimia zaidi ya 90 ya waliokufa ni vibaka tu. Na kuwa mhalifu hakuna kisingizio cha kutojua kwamba unachofanya ni kosa. Kwanza niambie nani katika hawa vibaka wa kuiba mafuta hakujua kwamba kuiba mafuta toka gari iliyopinduka ni kosa? Sasa kusema ilikuwa mara yao ya kwanza isiwe kisingizio.

Angalia hii picha hapa chini ya tukio kitambo kifupi kabla ya moto

View attachment 1181061

Karibu 80% ya unaoona hapo pichani walikufa. Sasa niambie, unaona innocent victims hapo? Unaona watu ambao hawajui wafanyalo?

Pamoja na hayo, mie nilichosema ni kwamba tujali utu kwa wau waliokufa, lakini tusiwatukuze. Hata nilisema wazi, ningeelwa kabisa kwa Raisi Magufuli kutoa rambirambi kwa waliokufa kwa Mkuu wa Mkoa Morogoro, na pengine hata serikali kuwazika victims katika kaburi la pamoja kwa gharama za serikali. Nilisema basi iishie hapo. Lakini kitendo cha raisi kwenda hospitali na kufanya matangazo makubwa juu ya fedha anazowakabidhi majeruhi, na pia matangazo juu ya mnara wa kumbukumbu - hayo nayaona waziwazi kwamba ni Raisi Magufuli na CCM yake kulitumia tukio hili kama fursa ya kisiasa, sio suala la huruma.

Kwani mara ngapi tumeona ajali kubwa zikitokea Tanzania na kuua na kujeruhi watu wengi na hatuoni Raisi Magufuli au CCM wakiifanya tukio kuwa kubwa hadi mnara wa kumbukumbu? Ndio maana nikauliza, je, jinsi serikali inavyoliimbia tukio hili mapambio, ni kwa kuwa liko karibu na uchaguzi ili wamfanye Magufuli yuko karibu sana na wananchi?

Hivi kweli katika utawala wa Raisi Magufuli ni ajali ngapi zimetokea na kuua watu wengi kwa namna ya kusikitisha, watu ambao hawakuwa katika tukio la uhalifu, je alifanya yote haya? Tetemeko la ardhi kule Kagera? Ajali ya wandishi wa habari Azam? Niambie kwa mfano, ni nini hasa kinachofanya majeruhi wa ajali ya moto wastahili zawadi kubwa ya fedha tofauti na majeruhi wa ajali nyingine za kusikitisha zilizotokea wakati wa utawala wa Magufuli?

Yaani hawa vibaka waliokufa katika tukio hili wanauma zaidi ya kina Akwilipo waliouwawa kama innocent victims ulisikia Raisi akitoa hata neno moja la kufariji familia yake? Na kwani ni huyo Akwilipo tu? Wahanga wa tetemeko Kagera waliishiwa kukashifiwa. Basi kama mnajali sana utu wa wahalifu, kila tunaposikia Polisi wameua washukiwa wa ujambazi "katika mapambano makali" basi Raisi Magufuli atoe salamu za rambirambi kwa familia zao!

Nakupata vizuri sana, ila nilijibu kwa kukusaidia kuwa, serikali kama baba wa wote haina jinsi, na nilikuchambulia watu wanaoweza kuangamia kwa jambo kama hili, hakika kama waijua nchi hii, la uwe mgeni, si wote walioenda hapo wameshiba roho ya wizi, no, no, no, hapo kuna ujinga na tafsiri ya zali la mentari kwa tafsiri yao, na nikakukumbusha kwamba kama hawa wasisikitikiwe kwa sababu tu ni wezi, basi kuna wezi wengi sana, tofauti ni wavaa suti na wanaonekana wastaarabu.

Kuhusu kwenda nje ya maadaaa, hilo sitajadiliana sana, maana sijajua una uwezo gani katika kuelewa.`
 
Back
Top Bottom