CCM na Rais Magufuli wanatumia ajali ya moto Mororgoro kama mtaji wa kisiasa na wakiwatukuza wahalifu kama mashujaa

stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
17,688
Points
2,000
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
17,688 2,000
Mkuu ukumbuke tu kuwa walioumia ni binadamu kama wewe na hakuna kosa kuwapa msaada unaotakiwa.
 
B

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
4,569
Points
2,000
B

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2012
4,569 2,000
Sijasema popote nilitaka wasihudumiwe. Nimesema tukio linatumiwa kisiasa. Hivi nyie CCM mmenda shule lakini? Kwa nini mnashindwa kuelewa insha fupi namna hii?
If you do not know where you are going any road will take you there
 
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Messages
5,456
Points
2,000
Mwanamageuko

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2010
5,456 2,000
Acha spedi tuiite spedi mara nyingine. Tusipoangalia katika kutafuta mitaji ya kisiasa kuna wakati tutawatukuza majangiri wa pembe za ndovu.
Huo ndio ukweli mchungu...na hili ndio linapelekea kuthibitisha kwamba CCM ni kichaka cha uhalifu... pango la walanguzi na majambazi... shamba la bibi...
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Mkuu ukumbuke tu kuwa walioumia ni binadamu kama wewe na hakuna kosa kuwapa msaada unaotakiwa.
Hakuna jambazi au kibaka au mbakaji wa watoto ambaye sio binadamu kama mimi. Lakini namna wanavyotendewa lazima ionyeshe kuna tofauti kati yangu nisiye kibaka, au jambazi au mbakaji wa watoto kama wao. Labda siku ukibakiwa mwanao, au kuibiwa badala ya kusaidiwa ukipata ajali, ndio uje uniambie aliyembaka au kukuibia ni binadamu kama wewe hakuna kosa kumpa msaada unaotakiwa. Lakini hapa hatuongelei kutowapa msaada, tunaongelea kuwapa msaada kwa namna ya kulitumia tukio kama fursa ya kisiasa, hata kwenda mbali zaidi ya hapo. Someni muelewe ndugu zangu.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Yaani hii mada ya huyu mpumbavu tangu jana badomnaisumbukia na alaaniwe huyumtoa mada hafai na siyo raia
Kibaka mwingine wewe, unaiba kwenye magari ya ajali na unaibia watu waliopata ajali badala ya kuwasaidia. Bado 40 zako.
 
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
5,972
Points
2,000
Titicomb

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
5,972 2,000
Majina ya vibaka wengi waliokufa wakiiba mafuta huku wakimwacha bila msaada dereva wa lori lililopata ajali
Two wrongs don't make it right!
Kama baadhi yao walikosea kutomsaidia dereva na kuiba mafuta basi unataka na serikali ikosee kwa kuwahukumu marehemu wote hata wale waliokufa wakitoa msaada au wapita njia au watu ambao pale lilikuwa eneo lao la kazi na hawakushiriki kuchota mafuta?
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
45,522
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
45,522 2,000
Ukweli ndio huo, labda kwa mtu asiye na uwezo wa kufikiri ndio hataona kwamba CCM na Magufuli wanataumia ajali ya moto Morogoro kama mtaji wa kisiasa.

Hatukatai kwamba wakati wa hili janga na msiba, labda si vema kuanza kuhukumiana, kama alivyosema Rais Magufuli, japo haina maana baada ya msiba kusiwepo kabisa kuhukumiana. Lakini sasa Rais Magufuli mwenyewe na CCM si kwamba tu hawahukumu, bali wanaenda mbali zaidi kwa kutumia tukio hili kama mtaji wa kisiasa, kujiuza kwa wananchi kisiasa.

Hawa watu waliokufa wakiiba mafuta kwenye ajali wote tunajua ni wahalilifu, vibaka. Tunachoona sasa ni kwamba wamegeuzwa kuwa mashujaa wa namna fulani. Majushaa wa kuiba kwenye tukio la ajali?

Zaidi ya zawadi za maelfu ya pesa yakitangazwa live na vyombo vya habari, kuambiwa serikali itagharamia matibabu (yaani mimi mlipa kodi nigharamie matibabu ya vibaka wa mafuta) sasa tunaambiwa wajajengewa mnara wa kumbukumbu!

MImi kama mlipa kodi wa Tanzania, sitaki hela yangu ya kodi itolewe kama zawadi kwa mhalifu, wala imjengee mhalifu mnara wa kumbukumbu. Labda kwa huruma inaweza kugharamia mazishi, kwa kuwa mhalifu aliyekufa hawezi kujizika.

Hivi tangu lini mhalifu amekuwa akitukuzwa kiasi hicho? Tangu lini Tanzania limewkuwa taifa la kutukuza uhalifu? Hivi CCM wamekuwa desparate kujiuza hadi kufikia kiasi hiki? Au CCM na Raisi Magufuli wanaona kuwa wao ndio kisababishi cha hali mbaya ya mzunguko wa fedha nchini kiasi kuwafanya watu kufanya chochote kujipatia fedha kidogo?

Binafsi wala hata sikuona haja ya raisi Magufuli kuwatembelea hawa watu hospitali na kufanya matangazo mengi ya kutoa msaaada wa fedha huku akitaja kiasi wanachopewa. Na wala sioni haja ya kuwajengea mnara wa kumbukumbu. Na kama ikibidi kujenga huo mnara, basi tuandike maandishi "hapa wamezikwa watu waliokuwa wakiiba mafuta baada ya ajali ya lori. Tujifunze ili tukio kama hili lisije tokea tena.

Sikatai kutoa maneno ya pole kwa wafiwa, lakini jambo la ajabu ni kuona Magufuli na CCM yake wakienda mbali zaidi na kulifanya tukio hili kuwa mtaji wa kisiasa. Hili ni tukio la kihalifu, kwa kiyo serikali na Raisi Magufuli walipaswa watende kwa umakini wakijua hilo, sio kulitumia kujijengea umaarufu wa kisiasa. Hivi mmefikia kuwa desparate kiasi hicho katika kujaribu kufanywa mpendwe na wananchi? CCM kimekuwa chama kibaya cha kujitembeza?

Ajali nyingi sana zimetokea nchini na kuua watu wasio na hatia. Ni mara ngapi umesikia Raisi Magufuli akitembelea majeruhi wa ajali hizo na kuwapa maelefu ya fedha au kuwajengea mnara wa kumbukumbu au ajali hizo kufanywa tukio la kitaifa? Kwa nini hii ya wahalifu hawa ionwe tofauti - au kwa kuwa inakuja tukielekea uchaguzi Mkuu kukiwa na tetesi kwamba serikali ya Magufuli inazidi kuporomoka katika umaarufu na kuwa katika uchaguzi wa haki hataweza kushinda?

NB: Kwa tukio kama hili Raisi Magufuli alipaswa kufanya yafuatayo badala ya kulitumia tukio kisiasa

Raisi angetoa salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kuwapa pole wafiwa. Angetamka kwamba serikali itagharamia mazishi ya waliokufa ikiwa hawatatambuliwa na ndugu zao, na kugharamia matibabu kwa majeruhi.

Na pia angekumbusha Watanzania kwa ujumla kwamba wajiepushe na kujichukulia mali pale ambapo ajali zinapotokea, iwe gari binafsi au ya mizigo, kwa kuwa kufanya hivyo sio tu sio ubinadamu bali pia ni kitendo cha uhalifu na wanaofanya hivyo wakikamatwa watachukuliwa hatua kali.

Basi, hiyo ingetosha kabisa. Hakuna kutembelea hospitali na kutangaza "nakugawia laki tano ukanunue juice", hakuna kutangaza kujenga mnara wa kumbukumbu, hakuna la zaidi. Kwa kuwa wengi waliopatwa na janga hili kimsingi ni wahalifu.

La sivyo tutarajie siku moja Raisi Magufuli akitembelea majambazi waliojeruhiwa na polisi kwa risasi wakiwa wamelazwa hospitali na kuwapa pole na zawadi za fedha, kwa kuwa anajali sana utu.
1. Mimi si mtetezi wa Magufuli, Magufuli ana makosa mengi, na hata anapofanya mazuri huwa anayafanya kwa njia mbaya, nimemsema mara nyingi hapa na wanaonifuatilia wanajua hilo.

2. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Katiba ya nchi inasema kwamba watu wote watachukuliwa kama hawana hatia mpaka mahakama itakapowapata na hatia. Hizi habari z akusema watu ni wahalifu bila kipimo wala kituo ni kuweka mtego wa panya unaonasa mpaka nzi.

3. Magufuli ana lawama nyingi katika mizizi ya watu kukosa uchumi wa kueleweka na elimu kulikowafanya waishie kuungua moto. Lakini kuanza kumlaumu kwa kuwa "waliofariki ni wahalifu" ni kufuja fursa ya kumlaumu vizuri Magufuli na kuitumia vibaya sana fursa hii kiasi cha kwamba wengine wanaosema kuna watu furaha yao ni kumlaumu Magufuli tu wanaweza kupata mtaji wa kusikilizwa katika lawama hizi.

4. Hata mimi sifurahii rais anavyogawa pesa kama vile pesa ndiyo ufumbuzi wa matatizo yote.Tumekuzwa katika siasa za "Utu wa mtu ni kazi, pesa ni matokeo". Lakini zama zimebadilika, na hakuna kinachomzuia rais kisheria kugawa pesa. Hivyo ndivyo anavyotaka urais wake uwe. Hakuna sheria inayomkataza. Kama hupendi hilo, gombea urais umshinde na wewe uoneshe mfano wa urais bora wa kutatua matatizo ya watu bila kuwagawia pesa.Mimi nitakuwa mtu wa kwanza kusifia uongozi huo na kusema "uongozi huu ni bora kuliko Magufuli alivyokuwa anagawia pesa mtu mmoja mmoja".

5. Unajichanganya unaposema rais anakosea kusaidia wahalifu, halafu hapo hapo unasema angetoa rambirambi na kusaidia gharama za mazishi ya wasiotambuliwa. Ni kama unamlaumu rais kwa kusaidia wahalifu, halafu unasema rais angesaidia wahalifu.
 
Z

zigg

Member
Joined
Aug 4, 2018
Messages
39
Points
95
Z

zigg

Member
Joined Aug 4, 2018
39 95
Ubaya upo wp? Si kweli walikuwa wanachota mafuta ambayo si yao? Na kila aliegusa mafuta aliungua ukweli uliotamkwa umekuwa mchungu kwa sababu wakubwa waliingilia na kweli sisi sote lazima tuwe na majonzi kwa vifo hivyo na tuonyeshe majonzi na huruma kwa kila janga tusibagui siku ingine gari ya hela itaanguka watu watavamia watapigwa risasi ja na hao wataitwa mashujaa? Watajengewa mnara? Sina maana kuwa serekali imefanya vibaya ila ajali zisibaguliwe pole sana kwa wafiwa
Yaani ndiyo maana siwapendi wapinzani kwaajili ya akiliyao mbovu kama mtoa mada hivi wewe ni binaadamu wa kawaida kweli au hiyo CHADEMA yako ndiyo inakufundisha uwe na roho mbaya kiasi hicho halafu mnakuja kutuomba muongoze nchi watu wenye rohombaya kama yako wewe?

Maneno hayo kamwambie tundu lissu wenu huko siyo mnatuletea huku sisi tuko kwenye majonzi ya msiba huna huruma kabisa
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
1. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Katiba ya nchi inasema kwamba watu wote watachukuliwa kama hawana hatia mpaka mahakama itakapowapata na hatia. Hizi habari z akusema watu ni wahalifu bila kipimo wala kituo ni kuweka mtego wa panya unaonasa mpaka nzi.

5. Unajichanganya unaposema rais anakosea kusaidia wahalifu, halafu hapo hapo unasema angetoa rambirambi na kusaidia gharama za mazishi ya wasiotambuliwa. Ni kama unamlaumu rais kwa kusaidia wahalifu, halafu unasema rais angesaidia wahalifu.
Mkuu, hakuna popote tumesema anakosea kuwasaidia wahalifu. Tumesema anatumia kuwasaidia wahalifu kama mtaji wa kisiasa. Kwa mfano, tueleze ni wahanga wangapi wa ajali za kusikitisha Magufuli kawatembelea hospitali akitangaza hewani nakupa hii laki tano ununue juice? Na ni mara ngapi ajali zimetokea nchini watu wakafa wakajengewa mnara wa kumbukumbu?

Tunasema kama hii ajali isingehusu wengi wa wahalifu, tungemwelewa. Lakini tunachoona ni bidii kubwa ya kujitangaza kupitia hii ajali - zawadi laki tano kutangazwa live, mnara wa kumbukumbu nk. Tunajua lengo sio huruma bali kutumia janga lililowakumba watu wasio na uwezo kimaisha kujionyesha yuko pamoja nao ili tu kupata kura zao.

Sasa hata kujitangaza kwa kutumia tukio la ajali inaweza isiwe sio tatizo. Lakini sasa, kujitangaza kwa kufunika kombe la mhalifu ili kupata ujiko wa kisiasa is very pathetic
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
45,522
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
45,522 2,000
Mkuu, hakuna popote tumesema anakosea kuwasaidia wahalifu. Tumesema anatumia kuwasaidia wahalifu kama mtaji wa kisiasa. Kwa mfano, tueleze ni wahanga wangapi wa ajali za kusikitisha Magufuli kawatembelea hospitali akitangaza hewani nakupa hii laki tano ununue juice? Na ni mara ngapi ajali zimetokea nchini watu wakafa wakajengewa mnara wa kumbukumbu?

Tunasema kama hii ajali isingehusu wengi wa wahalifu, tungemwelewa. Lakini tunachoona ni bidii kubwa ya kujitangaza kupitia hii ajali - zawadi laki tano kutangazwa live, mnara wa kumbukumbu nk. Tunajua lengo sio huruma bali kutumia janga lililowakumba watu wasio na uwezo kimaisha kujionyesha yuko pamoja nao ili tu kupata kura zao.

Sasa hata kujitangaza kwa kutumia tukio la ajali inaweza isiwe sio tatizo. Lakini sasa, kujitangaza kwa kufunika kombe la mhalifu ili kupata ujiko wa kisiasa is very pathetic
Katiba inasema ni kazi ya mahakama kusema nani ni muhalifu na nani si muhalifu, na mtu yeyote ambaye mahakama haijamsema kuwa ni muhalifu, achukuliwe kama si muhalifu.

Hii inaitwa "presumption of innocence".

Ni msingi wa kisheria unaoeleweka na kuheshimiwa dunia nzima, si Tanzania tu.

Unaelewa hilo?
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Two wrongs don't make it right!
Kama baadhi yao walikosea kutomsaidia dereva na kuiba mafuta basi unataka na serikali ikosee kwa kuwahukumu marehemu wote hata wale waliokufa wakitoa msaada au wapita njia au watu ambao pale lilikuwa eneo lao la kazi na hawakushiriki kuchota mafuta?
Hatuongelei kuwahukumu Mkuu, tunaongelea vikolombwezo vya ki-plomotion ambavyo Magufuli na serikali wanavitumia hapa kupitia tukio la kihalifu lililotokea, kwa mfano, kutembelea wagonjwa na kutangaza zawadi, kujenga mnara nk. Kama ingekuwa tukio halihusiani na uhalifu huenda tusingesema, lakini kufanya hii promotion kupitia tukio la kihalifu ni kama kubariki uhalifu.

Fikiria kwa mfano. majangiri ishirini wameingia Serengeti kuua tembo, na ikatokea wengi wao wakauwawa na tembo na wengine kujeruhiwa wakalazwa. Itakuwa sahihi Magufuli, kwa matangazo mengi live, kuwatembelea majangiri majeruhi hospitali na kuwapa zawadi ya laki tano, na kusema tusiwahukumu, na hata serikali kusema itagharamia mazishi ya waliouwawa na kuwajengea mnara wa kumbukumbu pale Serengeti?

Serikali inaweza kusaidia, lakini kwa uhalifu wa tukio, haipaswi kulifanya kama hao majangiri ni mashujaa kwa kelele na matangazo mengi. Na itawafanya mashujaa ikiwa tu inajua kuna watu kama wao ambao wataiwezesha kushinda uchaguzi kirahisi.
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Katiba inasema ni kazi ya mahakama kusema nani ni muhalifu na nani si muhalifu, na mtu yeyote ambaye mahakama haijamsema kuwa ni muhalifu, achukuliwe kama si muhalifu.

Hii inaitwa "presumption of innocence".

Ni msingi wa kisheria unaoeleweka na kuheshimiwa dunia nzima, si Tanzania tu.

Unaelewa hilo?
Huelewi maana ya hicho kipengele cha sheria. Presumption of innocence umekufa unaiba mafuta? Kwamba inawezekana walikufa wakitaka kuliinua lori lililopata ajali sivyo?
 
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2009
Messages
45,522
Points
2,000
Kiranga

Kiranga

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2009
45,522 2,000
Huelewi maana ya hicho kipengele cha sheria. Presumption of innocence umekufa unaiba mafuta? Kwamba inawezekana walikufa wakitaka kuliinua lori lililopata ajali sivyo?
Presumption of innocence inasema kila mtu atachukuliwa hana hatia mpaka mahakama impate na hatia.

Sasa hao unaosema wahalifu, mahakama iliwapata na hatia lini?

Unajuaje nani kafa anaiba mafuta, nani kafa anaenda kusaidia ajalini, nani kafa wakati kaenda kuwatahadharisha watu waondoke kwenye eneo la ajali, nani kafa kwa utashi na ujinga tu wa kutaka kuangalia gari lililopata ajali bila wizi wowote kuwapo akilini mwake?
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Presumption of innocence inasema kila mtu atachukuliwa hana hatia mpaka mahakama impate na hatia.

Sasa hao unaosema wahalifu, mahakama iliwapata na hatia lini?
Niambie kama unaona uhalifu wowote ukiendelea hapa chini. Na kama unauona, wewe ni mahakama? Kama huuoni kakojoe ulale.

1565791414665-png.1181264
 
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2010
Messages
7,116
Points
2,000
Synthesizer

Synthesizer

JF-Expert Member
Joined Feb 15, 2010
7,116 2,000
Hiyo picha hata sijui ya wapi kwanza.
Mkuu, hiyo ni picha ya watu wakishughulika kuchota mafuta baada ya kufungua mfuniko wa petroli kwenye lori lililoanguka, sekunde kadhaa kabla ya moto kulipuka. Wengi wa hao watu unaowaona hapo, kama sio wote, walikufa!
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
83,364
Points
2,000
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
83,364 2,000
Presumption of innocence inasema kila mtu atachukuliwa hana hatia mpaka mahakama impate na hatia.
Kiutaratibu rasmi wa kisheria, sawa.

Lakini, ikitokea umefua nguo zako na kuzianika uani kwako [line drying] halafu unaona mtu ambaye humjui anakuja kwa kunyata halafu anaanua mashati mawili matatu, hapo vipi?

Huyo hatakuwa mwizi mpaka mahakama impate na hatia ya kukuibia nguo?
 

Forum statistics

Threads 1,326,235
Members 509,448
Posts 32,215,479
Top