Mbunge wa CCM
JF-Expert Member
- Nov 13, 2009
- 475
- 25
Wewe unaonekana kujua mengi kuhusu uingizaji wa magari haya. Hebu weka wazi na siyo kuwashutumu watu wadaku wakati wewe mwenyewe unaonekana pia mdakaji. Kama si mdakaji mkuu hebu eleza ilikuwaje hasa kuhusu ununuzi huu wa magari, vinginevyo na wewe huna unalolijua kaa kimya watu waeleze wanachofahamu. Au ndiyo kampeni zimeanza?
Kuwa mkuu wa fedha na mipango wa ccm si lazima uambiwe kila kitu kinachotoka hazina ya taifa kwenda ccm. mambo mengine hayahitaji msululu wa watu kujua wao watakabidhiwa magari na fadha tu, vimetoka wapi sio kazi yao, kazi yao itakuwa ni kupanga jinsi gani watumie.
Namuomba Mungu na miungu yoote habari hii iendelee kuwaa tetesi hivyohivyo kani kama tumefikia hapo mwenyekiti anafanya jambo kubwa kama hilo na KM wake hajui, Mungu apishe mbali kwani itakuwa ni hitimisho kwamba SASA TUMEKWISHA!!
Wala usishangae ukijasikia kuwa pesa za kununulia magari zimetoka kwa 'Wafanyabiashara fulani'.
In return, wanapata nafuu ya kodi, tenda zenye akili, kuwa karibu na 'mzee' etc...
Nimezisikia habari kuwa siri aliyotoboa Dr.Slaa juu ya CCM kuagiza magari 200 imemuhuzunisha sana Makamba maana hakuwa na tip juu ya kuwepo kwa mpango kama ule. Ni JK tu ndiye aliyekuwa katikati ya mpango mzima. Muhabarishaji anathibitisha zaidi kuwa ndo maana hata majibu ya Makamba yalikuwa dhaifu sana wakati ya Chiligati na Makalla yamekuwa rojorojo.
Je, kuna uongo au ukweli wowote ndani ya tetesi hii? Na
Je, kwa nini JK amenza kumficha hata Katibu Mkuu wake wa Chama?
Pesa hizi ni za walipa kodi wa Tanzania zilizofisadiwa katika EPA, Meremeta, Mwananchi, Kagoda n.k.
UR dead right.
Add IPTL, Richmond/Dowans, BoT Twin Towers, Pension Funds...