CCM na kandambili

CCM na kandambili

Naweza kukusifu kuwa wewe sio mnafiki siku utakapo jitokeza kwenye mkutano wa hadhara na kutamka hayo maneno hapo nitakusifu wewe haswa mkweli! Lakini upo kwenye PC unaijisfu huko ni unafiki
kuumia kwako hakuwezi kunifunga
mimi na kunifanya nisiandike kile ninachoona mimi kinafaa, wala siwezi kukuogopa wewe uta react vipi
hiyo hainipi shida, ninacho weza kukuambia ni ndiyo kikwete ni afadhali ya kandambili za msalani zitakusitiri kwa uchafu, na huo ndiyo mtazamo wangu juu yake, nikishauri jambo moja wewe mtafute na umpe hii taarifa, then anaweza kujiboresha na kuwa hatua ya pili kutoka kwenye kandambili na kuwa japo yebo yebo
 
Yap! Tupingane kwa hoja lakini sio kwa lugha za kejeli na dharau
ukiogopa kuesema ukweli jinsi
mtazamo wako na hatma ya viongozi wetu, kuliongoza taifa, kizandiki, kifisadi, kibabe
lazima utaleta hoja kuwatetea wezi wa rasilimali za umma, huku wakitudanganya kuwa tutapata,
maisha bora ya kutafuna boflo na maziwa, ongeza umakini ili mawazo na mtazamo wa mtu mwingine juu ya ufirauni usiyaite kejeri na dharau
 
Ila hakuna atakaye kuunga mkono kwa lugha zako za kejeli zisizo na staha wala adabu!
sitafuti kuungwa mkono na wafuasi wa mafisadi na mamluki wa viongozi wezi wasiokuwa watekelezaji wa majukumu juu ya utawala wao, wewe ni mmoja wa wanaokula upenuni mwa kikwete tena vyakula vya kunyongwa, vyenye manung'uniko, tena visivyokuwa na baraka za Mungu

so hilo halinipi shida sana nategemea kupingwa na wengi wa watoto wa viongozi magogoi wasojua majukumu yao vizuri zaidi ya uzandiki na ughafidhuna
 
Uhuru mwingine usivuke mipaka, we sema ccm na si raisi wetu! yaani unamfananisha raisi na kandambili!
alokwambia kuwa mimi ni raia wa Msumbiji nani?
toafauti yangu mimi na wewe ni kwamba siwezi kuliremba jalala,
ati lifanane na ukumbi wa harusi,
 
utatamani kuona na hautaona, utatamani kusikia na hautasikia
kuchagua ccm na kikwete ni uthibitisho tosha wa akili ilivyo 'shake well before use'
 
Uhuru mwingine usivuke mipaka, we sema ccm na si raisi wetu! yaani unamfananisha raisi na kandambili!
Hee, usipandishe munkali anatumia fasihi! Ni kwamba kikwete kwake is not a cup of tea, hata asipokuwa rais bado mambo yatakwenda! Kwa maana nyingine, kandambili kwake zina msaada zaidi ya kikwete na sisi emu, si ndivyo Anyisile?
 
afadhari ulikwepo mkuu,
tatizo wengi wetu tunakurupuka kujibu post tu bila kujua mwandishi amesimama juu ya nini, na nini hoja yake ya msingi
 
Mimi wala sikulaumu kwa lolote anyisile kwa kuwa unajaribu kuteta japo kiduchu hisia za watanzania wanaochakachuliwa keki yao ya taifa na mafisadi! Huku mtaa mambo yanakuwa afadhali ya jana hii ni kutokana na kutokuwepo kwa umakini ktk uongozi wa ccm!
 
ni kweli mkuu Msikonge,
kwa mwenye akili na kujali sana afya yake hata kama ni malafi kiasi gani, keki ikidondokea juu ya kinyesi hawezi
kuisafisha, maana itakuwa si keki tena bali uchafu, sasa ni heri achukue hata mhogo wa kuchoma, tena bahati nzuri
ni kwamba mhogo ni heavy kuliko keki, japo thamani yake vikiwa dukani havifanani
 
afadhari ulikwepo mkuu,
tatizo wengi wetu tunakurupuka kujibu post tu bila kujua mwandishi amesimama juu ya nini, na nini hoja yake ya msingi
Kwa hili mkuu Anyisile inabidi kuwavumilia kwani uwezo wa kuelewa tunatofautiana. Dawa ya jipu ni lazima likamuliwe japokuwa linauma! Kikwete aliingia akibeba matumaini ya watanzania, na kama nilivyotarajia, amewaangusha kinoma, kama vile nilijua sikumpa kura yangu, nikiami ni msanii!
lazima tufikie uozo tuite uozo na manukato tuyaite hivyo, tutoe unafiki hata kama unafaidika na ufidhuli unaoendelea! kwani angefanya mema hata tu kujitoa muhanga kukemea kwa vitendo ufisadi kwa manufaa ya watanzania waliomuamini, isipokuwa mimi, tusingemsifu na kusema anatufaa, mbona mpaka leo japokuwa mwalimu alikuwa na mapungufu yake hatusiti kumsifu kuwa nu mfano wa kuigwa. Rais wa Rwanda, pia pamoja na mapungufu yake lakini kwa muda huu tu amekuwa ni kiongozi wa kupigiwa mfano! sasa kulikoni kwa rais wetu!
 
Hii kali!! Nafikiri ni vizuri mkazionyesha hizo hasira zenu kwenye uchaguzi mwezi wa kumi. Maana si ajabu wewe unayetuandikia haya hapa jamvini mwezi wa kumi ukifika utanunuliwa na fedha za kifisadi ukawa kwenye misafara ya Kiikwete au meneja wa kampeni za CCM unasaidia kuipigia debe CCM ishike nafasi kwa mara nyingine.

Hakika wakati muafaka ni huu wa kuonyesha hisia zetu kwa matendo, yaani kuwa radhi kwenda kujipanga kwenye mstari na kutimiza wajibu wa kiraia wa kumchagua yule unayeona atashirikiana nawe kuleta maendeleo. Viongozi wabovu, wauza sura ndani ya bara la Afrika, waloshindwa kusoma alama za nyakati na kushirikiana na wananhchi walowapa nyadhifa walizonazo wamewekwa madarakani na raia wao wema kabisa waloshindwa kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Zoezi la kupiga kura mara nyingi limeachiwa watu wachache, wanaofikiria kuwa hawana kazi za msingi za kufanya, ndo maana wako radhi kusimama juani kwa zaidi ya masaa kadha; ili hali wanaofikiri wanamajukumu ya 'kitaifa au kimataifa' wakikwepa jukumu hilo halali kabisa, hivyo wakishiriki kuwaweka viongozi wabovu madaraka.
 
Kwa hili mkuu Anyisile inabidi kuwavumilia kwani uwezo wa kuelewa tunatofautiana. Dawa ya jipu ni lazima likamuliwe japokuwa linauma! Kikwete aliingia akibeba matumaini ya watanzania, na kama nilivyotarajia, amewaangusha kinoma, kama vile nilijua sikumpa kura yangu, nikiami ni msanii!
lazima tufikie uozo tuite uozo na manukato tuyaite hivyo, tutoe unafiki hata kama unafaidika na ufidhuli unaoendelea! kwani angefanya mema hata tu kujitoa muhanga kukemea kwa vitendo ufisadi kwa manufaa ya watanzania waliomuamini, isipokuwa mimi, tusingemsifu na kusema anatufaa, mbona mpaka leo japokuwa mwalimu alikuwa na mapungufu yake hatusiti kumsifu kuwa nu mfano wa kuigwa. Rais wa Rwanda, pia pamoja na mapungufu yake lakini kwa muda huu tu amekuwa ni kiongozi wa kupigiwa mfano! sasa kulikoni kwa rais wetu!
mkuu uko sahihi, hakika harufu ya msalani haiwezi kuwa manukato hata siku moja tatizo ninaloliona hapa kwetu, tunapenda kumsifia mtu si kwa uwezo bali mapenzi ya umaarufu wake na anapokuja mtu akakosoa jambo juu ya mtu huyu basi wale wafki wa ufuasi kwa mtu huyo watakuja juu,
mimi hata ningekuwa na mapungufu kiasi gani lakini sijaliona zuri la kikwete kwa uongozi wake yeye kama mkuu wa nchi lenye manufaa kwa taifa zaidi ya safari nyingi za nje, inaniuma sana ninapoona hata vile tulivyo na uwezo navyo tunashindwa kuvifanya kwa kujikowezesha wenyewe, sasa huyo raisi wetu yupo kwa ajili ya nini? kama kivuli?
 
mwalimu alisema "Umasikini wa fikra ni mbaya zaidi.....!" Ni vizuri angalau watu wakitoa japo kwa kiasi machungu walionayo, kwani ni kwa njia hii wanawesa ku'diffuse tension'! Viongozi wetu wanatupeleka wapi sasa, imefikia watu badala ya kug'wag'wania fani zao, wanakimbilia politics, kwa nini, kuna masilahi! Mbunge akidai posho anapewa haraka sana, mfanyakazi akiomba ongezeko la kijimshahara ambacho kalibu chote kinaishia kukatwa kodi anazomewa na kukejeliwa bila kujali ni yeye ndie anatewalipa wanasiasa, na kwamba kimsingi yeye ndie kaiajili serikali na politiciani wote kupitia kodi!
haya yote ni kutokana na mfumo mbove usiojali maslahi ya wananchi waliowengi ya ccm kinachohakikicha kinawakumbatia mafisadi hata kama in expense ya wananchi!
huwezi kujiuliza hivi kwa nini viongozi wetu wanapenyeza watoto wao kwenye siasa (ili kulinda na kuendeleza maslahi yao)??? Watoto hawa hawajuishida wanazopata watanzania! Na viongozi wetu wala haiwasumbui kuona upanuzi wa totauti ya kipato kati ya wasionacho wa walioneemeka unavyozidi. siku moja hawa walalahoi wakisema 'enough is enough' hakuna atakayekuwa salama.
 
mkuu Anyisile, Naamini ktk ungwe ya kwanza rais huwa anajitahidi sana kuonyesha kwamba kweli anaweza na anastahili kupewa ngwe nyingine na waajiri wake (walala hoi), hii ni kutokana na kuwepo kwa check-point (uchaguzi baada ya miaka hiyo 5). kwa utendaji kazi alioonyesha kipindi cha kwanza, mheshimiwa huyu, akichaguliwa tena tutegemee nini ktk kipindi hiki cha lala salama wakati traffic hawapo tena na basi ndio limefunguliwa 'speed gorvernor', usalama upo hapo! Mungu ibariki Tz, Mungu bariki watz!
 
kweli kabisa kwa maana ukamilifu wa mwanadamu na kwenye hatua ya kuwa mtu ni uwezo wake mwenyewe wa kuweza kujitawala fikra zake,
na kujitambua yeye ni nani katika jamii inayomzunguka, kama atakosa hayo na kujidhurumu nafsi yake kwa sababu ya kundi ama mtu flani,
huyo hana tofauti na kiumbe. maana ni utashi pekee wenye kuweza kukuamusha akili yako ama kwakubadirishana mawazo na jamii nyingine
hasa ukisimamia kujifunza zaidi kwa yale yanayofaa hata kama huna elimu ya kufafana nao.
sifa hizo ndizo zenye kuweza kukufanya utoke kwenye kundi la kuwa kiumbe na kuwa mwanadamu harafu uitwe mtu kamili, maana unaweza ukaitwa mwanadamu lakini usiwe mtu kwa kuwa huna sifa za kukufanya kuwa mtu, kwa vile huna utu, na utu ni hekima, busara na ujasiri
hivi vyote vinapatikana kwa yule mwenye kujitambua na kujitawala kifikra
 
mkuu Anyisile, Naamini ktk ungwe ya kwanza rais huwa anajitahidi sana kuonyesha kwamba kweli anaweza na anastahili kupewa ngwe nyingine na waajiri wake (walala hoi), hii ni kutokana na kuwepo kwa check-point (uchaguzi baada ya miaka hiyo 5). kwa utendaji kazi alioonyesha kipindi cha kwanza, mheshimiwa huyu, akichaguliwa tena tutegemee nini ktk kipindi hiki cha lala salama wakati traffic hawapo tena na basi ndio limefunguliwa 'speed gorvernor', usalama upo hapo! Mungu ibariki Tz, Mungu bariki watz!

hapo ndipo nilipo na wasi wasi wangu maana hicho kitakuwa ni kipindi cha kujitengeza zaidi, kinyumbani,
huu ni wakati wa kuicha biskuti na kujaribu kula mihogo.

Mungu jaaria uwamshe watu wako kutoka upumbavuni.
 
Back
Top Bottom