bibikuku
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 832
- 495
Usiku huu timu ya kampeni ya CCM na ile ya CHADEMA wamejikuta wakipambana kwa dakika kadhaa katika eneo la Meru Garden wilayani Arumeru ambapo ilidaiwa kuwa CCM walikuwa pale kutoa hongo kwa watu kadhaa na kisha Chadema kugundua mchezo huo na kuvamia kwa lengo la kuwakamata na kuwasambaratisha.
Ugomvi huo unadaiwa kusababisha gari la Violet kuvunjwa vioo kwa mawe na kisha CCM wakaenda kuripoti jambo hilo polisi na kudai kuwa wamevamiwa wakati wakiwa katika starehe zao Bar.
Taarifa zaidi juu ya tukio hili tutazipata asubuhi na maendeleo yake. Lakini kwa ufupi hivyo ndivyo mambo yalivyotokea usiku huu