Mkuu heshima. Mimi naamini hata kama tungekuwa na wimbo wa taifa mzuri na mtamu kushinda zile za Gabriel na timu yake waimbazo wakizunguka kile Kiti cha Enzi; ambazo imenenwa kwamba sauti zao ni tamu kushinda vinanda na vinubi vyote vilivyopata kuwepo; bila HESHIMA, HAKI, na KUMJALI MNYONGE, wimbo huo ni ubatili tena wafanana na sauti za waombolezao.
UZALENDO kwa taifa ni kitu ambacho hakihitaji kuchochewa kwa ghiliba kama za kutunga nyimbo mpya, kugawa vibendera, au kuvaa mavazi fulani waliyobuni watawala. Badala yake, ni kitu ambacho huja au hutoweka chenyewe kutegemea na jinsi tabaka la walio wengi linavyotendewa. Ukisikia kwa mfano vijana wanaamini ni heri kuwa mbwa Ulaya kuliko binadamu Tanzania ujue uzalendo umekwisha na uzalendo huu haurudishwi kwa kutunga nyimbo mpya.