CCM na CHADEMA tuna cha kujifunza kwenye uchaguzi wa Zambia

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,221
22,297
CCM na Upinzani tuna cha kujifunza kwenye uchaguzi wa ZAMBIA

Nawasalimu kwa jina la demokrasia.

Leo nimeona nije na uzi mfupi kwa nilichojifunza kutokana na uchaguzi mkuu wa Zambia tarehe 12 Agosti 2021. Hakika ni uchaguzi ulioweka alama za kipekee hapa Afrika. Binafsi naweza sema Zambia ni Marekani ya Afrika linapokuja suala la uchaguzi mkuu wa rais, wabunge, madiwani, mameya ya wenyeviti wa halmashauri. Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Tume yao ya uchaguzi ilifanya kazi kwa weledi wa kipekee. Haikuwa na dosari yoyote. Hadi ninapoandika huu uzi tayari Rais mteule Hakainde Hichilema kashatangazwa huku Rais anayemaliza muda wake Edgar Lungu akitoa hotuba ya shukrani na kukubali matokeo.

Mimi kama mtu mwenye akili nyingi sana kuna mambo nimejifunza ambayo vyama vyetu vina vya kujifunza. Yaani CCM na upinzani hasa CHADEMA wanatakiwa wachukue darasa la kutosha.

CCM wajifunze nini? Chama tawala kina mengi ya kujifunza kutoka kwa chama kilichoshindwa uchaguzi chini ya Rais Edgar Lungu. Kwenye huu uchaguzi kuna mambo mawili tu yangesaidia Lungu kuendelea kubaki madarakani, jambo la kwanza ni utayari wa wazambia kumchagua tena kama angekuwa amekidhi mahitaji yao na jambo la pili ni kutumia vyombo vya dola kulazimisha kubaki madarakani. Kwenye jambo la kwanza ilikuwa ngumu kwasababu ni kama Lungu hakuwa na vision nzuri kama rais hali iliyotokana na kuupata urais kama bahati pale mwanzoni baada ya kifo cha Rais Sata. Lungu naweza kusema hakuwa dikteta ila alikuwa ni "bora liende" hali iliyowafanya makada wa chama chake kuwa na nguvu mno.

Wananchi wa kawaida walikuwa hawafurukuti mbele ya makada. Hawa makada wanalaumiwa mno kwa kufanya upuuzi mwingi. Kwahiyo wananchi walikuwa tayari wameshachoka vitimbi vya chama cha PF. Uwezekano wa Lungu kushinda ulikuwa mdogo. Mbinu ya kucheza rafu kwenye uchaguzi ilikuwa ni poa... ila angewezaje mbele ya tume huru ya uchaguzi? Angeweza vipi mbele ya polisi ambao nao pia walionyesha kuchoshwa na hawa makada?

CCM inatakiwa ipambane kutimiza ahadi zake na kulinda haki za kila mwananchi. Isiruhusu makada wake wakawa na haki kuliko raia wengine kisa ni wapinzani. Wananchi wote wawe na haki sawa bila kujali itikadi. Chama kiisimamie serikali kutekeleza ilani inavyotakiwa. Hakuna haja ya kusubiri hadi wananchi wachoke kabisa na kuamua kuyaleta mabadiliko kinguvu. Bado wananchi wa Tanzania wana matumaini na CCM hivyo hakuna haja ya kuwatibua.

Wapinzani (CHADEMA) wana mengi sana ya kujifunza kupitia huu uchaguzi wa majirani. Chama kilichoshinda cha UPND ni chama ambacho kinafanya siasa za kisomi mno. Chama kilijikita kwenye kufafanua mambo mengi ya kitaifa na sio kujikita kwenye matukio kwa kutafuta kiki za kijinga. Siasa za rais mteule Hakainde Hichilema ni za kisayansi na za kisomi mno. Jamaa ni mjenga hoja ambazo ukizisikiliza unaona kabisa huyu ni mwanasiasa mwenye kipaji. Hoja zake zilijikita kufafanua malengo ya chama chake huku akigusa maisha ya mwananchi wa chini. Kwa mfano kipindi cha kampeni alizungumzia suala la bei ya unga wa mahindi kupaa, bei ya mbolea na kwacha kushuka thamani. Na hakuishia kulaumu tu bali alitoa mwelekeo wa chama chake kutatua hayo huku akitaja kabisa na muda (deadlines).

Hizi siasa za CHADEMA za kutukana ovyo na kujikita kwenye matukio ya kujitafutia kiki ni siasa za kipuuzi zitakazozidi kuwachelewesha kuingia ikulu. Watu kama Mdude ndani ya CHADEMA ni wa kunyimwa nafasi ya kuongea mbele ya watu. CHADEMA ijikite kwenye masuala ya kitaifa huku ikitoa mbinu mbadala badala ya kujihusisha na mambo yasiyo na tija kwa chama. Kwa mfano viongozi waandamizi ndani ya CHADEMA kujihusisha na mambo ya Diamond Platnumz ilikuwa ni kukishushia chama thamani kwa kiwango kikubwa mno.

Mheshimiwa Zitto Kabwe ndo naona ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kufafanua jambo kama Hakainde Hichilema ila tatizo tayari chama chake kimefunga ndoa na Chama Tawala kwahiyo hoja zake hata akizisema ni kupoteza muda kwasababu tayari yeye ni sehemu ya serikali. Upande wa CHADEMA alikuwepo Dr Slaa kama mjenga hoja za kisomi ila kwasasa chama hakina mwenye uwezo huo. Waliopo ndo hao kina Mdude, Lema, Sugu, na Msigwa. Ni huzuni kubwa sana kwa upinzani wa Tanzania
 
Mpaka hapa nilipo sijawahi kuona upinzani wanafanya uwasi ! Maaana pale Zanzibar ccm walifanya mambo ya hovyo sana.
 
Hebu niambie mwanasiasa gani wa CCM analingana na lema, sugu au msigwa kujenga hoja?
 
Hebu niambie mwanasiasa gani wa CCM analingana na lema, sugu au msigwa kujenga hoja?
Basi una tatizo kubwa sana kama Lema, Sugu na Msigwa ndo unawaona wajenga hoja wazuri. Msigwa juzi kasema tusitoe sadaka kwa wachungaji wasiounga mkono CHADEMA ana tofauti gani na waliochochea mauaji ya kimbari huko Rwanda?
 
Back
Top Bottom