Ccm na chadema, nani atatuangamiza katika hili?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm na chadema, nani atatuangamiza katika hili??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MWANALUGALI, Feb 13, 2011.

 1. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tuache propaganda katika mambo makubwa yanayoweza kuangamiza Taifa, tujadili issues kwa makini tuone nani kati ya vyama hivi viwili anayetupeleka kusiko ili tuonye na kutoa ushauri kwa kuweka mbele mstakabali wa nchi yetu. Baada ya kuangalia mwenendo wa uchaguzi uliopita, tukaangalia mapokeo ya uchaguzi na mwenendo wa vyama hivi viwili baada baada ya uchaguzi, sasa tunaweza kujadili na kujiuliza Kati ya CHADEMA na CCM:-
  • Nani anahatarisha usalama wa taifa letu?
  • Nani mwenye uroho na uchu wa madaraka?
  • Nani mwenye kutumia udini katika siasa zake?
  • nani asiyekuwa na sera?
   
 2. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 813
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  ccm ndo mwenye vyote ulivyotaja hapo
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umeleta hoja ambayo haijadiliki, namaanisha ni hoja ambayo hiko obvious na kila mtu anaujua ukweli,
   
 4. M

  Mkorosai Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM watatuangamiza, wana uroho na uchu wa madaraka. Wakati wa uchaguzi mkuu hawakukubali kushindwa hasa kwenye nafasi ya urais, walichakachua wakang'ang'ania Ikulu hadi kikaeleweka kuwa wana uchu wa madaraka. Kwenye chaguzi za Mameya huko Arusha, Mwanza na Mbeya ndiko hasa walikodhihirisha uroho wao wa madaraka!!

  CCM ni hatari sana kwa usalama wa taifa letu maana wanatengeneza na kukalia mabomu ambaye mlipuko wake utawafanya vijana kuleta mabadiliko kwa njia ambayo haitaratibiwa na yeyote kama ilivyotokea Misri na Tunisia.
   
 5. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu hoja inajadilika, kama sijakosea CCM ambacho ni chama kilichoko madarakani kimekuwa kikishutumu vyama vya upinzani kuwa vina uroho wa madaraka ikiwemo chadema. Siyo mara moja au mara mbili, viongozi na wanaCCM kuipachika CHADEMA kuwa ni chama chenye udini na kwamba ni chama cha vurugu!! je haya hayawezi kujadiliwa? Humu JF hakuna watu wa kukisafisha CHADEMA au kuisafisha CCM kwa hoja? Nadhani kuwa tunaweza kuruhusu vichwa vyetu vikaanza kufikiri na kuonesha nani kati ya vyama hivi anacheza mchezo mchafu wa kuangamiza taifa letu!
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,000
  Trophy Points: 280
  Mkuu ninasema hii mada inamajibu tayari, ukiangalia hapo kwenye Nyekundu, Chadema si wa kwanza kupewa hizo sifa na cCM pamoja na serikali yake
  CUF walipokuwa wapinzani wa kweli waliambiwa pia kuwa ni chama cha kidini, cha wapemba na pia ni chama cha vurugu, ilifikia mpaka IGP wa polisi (Mahita) kusimama mbele ya vyombo vya habari na kusema wamekamata Contena la CUF la zana kuulia (Majambia)

  Ndio maana nasema majibu ya hii mada yapo open mno sioni cha kujadili
   
 7. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo twaweza kuanzia mjadala wetu hapo ulipogusa! Kwa nini CCM inavituhumu vyama vinavyoonekana kuwa vyama mbadala kuwa ni vyama vya kidini na vyenye vurugu? je hilo laweza kuwa ndilo jibu la kutokuwa na sera kwa CCM? au kwa nini sehemu ambazo CCM haikubaliki ndiko kunakotokea fujo mara zote? ( angalia Pemba, Tarime, Mwanza, Arusha nk.) Kwa hiyo twaweza kukubaliana kuwa CCM ndiyo chama cha vurugu?
  Nadhani wana CCM wanapashwa kukitetea chama chao hapa kwa hoja yakinifu kama zipo
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,860
  Trophy Points: 280
  Hawawezi kuwa na utetezi CCM,wanacho weza wao ni mipasho na majibu ya jumlajumla Kama tunavyo jionea Bungeni sasa hivi kwa hoja za msingi kutolewa majibu ya hovyo na maelezo ambayo hata watoto hawawezi kutoa
   
 9. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kwa wengi wetu kuangamia siyo tena suala la wakati ujao, ni hali inayotukabili hivi sasa; siku nenda siku rudi sisi na watoto wetu tunashinda njaa, tukibahatika kupata muhogo kidogo na maharage ya kutowezea alhamdu lillah. Kwa upande wa shule kwa wototo wetu hilo husiseme, kwani mfumo uliopo ni wakuwahesabia vyumba vya darasa na wala siyo kuwapa elimu. Kwa mtindo huo huduni wa maisha tulio nao sisi tuna hakika kuhuridhisha kwa watoto wetu. Yote hayoni matokeo ya CCm kugangania madarakani
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  wa kujiangamiza ni sisi wenyewe
   
 11. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunajiangamiza kwa kuchagua chama kisichokuwa na sera nzuri za kutuondoa hapa tulipo au tunajiangamiza kwa kutokuwaiga Watunisia na Wamisri??
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Mwanalugali mbona watanzania tunaangamia tayari au wewe upo nje ya nchi.
  Maswali yako yanafaa ajibu Makamba.
   
 13. U

  Ulimali Member

  #13
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hapana nakataa wale wote wenye akili na ufahamu hawakuchagua ccm ila wamechakachua
   
 14. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #14
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  niko hapa hapa bongo, lakini nataka tutumie bongo zetu na kuwasaidia wenzetu walio wavivu wa kutumia bongo zao ili ijulikane nani anataka kuliangamiza Taifa na kwa namna gani. Tanzania ni nchi yetu wote na washika dau wakuu ni sisi wananchi, lakini kuna kikundi cha watu wadhani wao ndio wenye haki kuliko wengine kwa kila jambo!! Sasa ifike mahali kila kitu kijadiliwe kwa mapana na wananchi wanyonge wajue mbivu na mbichi!!
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Feb 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  chadema waache kufuata waraka wa kikatoliki ni hayo tu.
   
 16. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #16
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  LAITI NINGALIKUA RAIS KIKWETE NISINGEKAA HATA ZAIDI YA LISAA MOJA
  BAADA YA RIPOTI YA JUMUIYA YA NCHI ZA ULAYA KUWEKA WAZI
  KWAMBA NIKO MADARAKANI KIMABAVU KWA WIZI KURA:


  Kwa kweli wananchi inabidi tufike mahala tujiulize kwamba hizi nafasi za kuchaguliwa mtu, kwa mantiki kabisa kidemokrasia, ni (a) nafasi za AJIRA BINAFSI KWA YEYOTE ANAYEJIMEGEA KAKIPANDE au (b) ni fursa tu yenye dhamana kubwa na ridhaa ya wananchi ukawatumikie??

  Kama jibu sahihi ni bee hapo juu sasa iweje mtu uwe umeuchubua tu ofisini hata baada ya RIPOTI YENYE UJUMBE NZITO NA NYETI kama ule uliowashilishwa na Jumuia ya Nchi za Ulaya?? Na unapoendelea tu kujing'ang'aniza hivo hivo wapiga kura wapende wasipende, ilmradi tu kuna wazo liliwahi kutoka kwamba rais huongoza kwa awamu mbili, ndio tuseme kwamba uso wa aibu ulishakutoka siku nyingi au ndio kusema kwamba nawe unajaribu kuwapima Wa-Tanzania kwamba watakufanya kitu gani sio??

  Laiti ningalikua rais Kikwete wala nisingejiruhusu nafsi yangu kuendelea kukaa hata kwa lisaa moja zaidi tangu Jumuiya ya Nchi Ulaya itoe ripoti yake inayobaini wazi madai yetu ya muda mrefu kwamba CCM IMEIBA SANA KURA KOTE TANZANIA BARA NA VISIWANI; katika ngazi zote za uchaguzi.

  Nasema hivyo kwa sababu kwa binadamu ambaye bado angependa kujitunzia heshima yako hauwezi kuendelea tu kuchapa usingizi huko kwenye ikulu ya watu kana kwamba hakuna chochote kibaya kilichotokea wakati tayari ni kwamba hauko madarakani kwa ridhaa wananchi. Cha zaidi, hao wenzetu waliotoa ripoti yao pindi wanapoendelea kukuona madarakani wanashindwa tu kukuambia kwamba KWA NINI UGEUZE NAFASI ZA UTUMISHI KWA UMMA KUWA AJIRA BINAFSI kwako kama alivyofanya Mubara??

  Pengine ndio maana Marais walipokutana Africa Union na kuhoji kwa nini watu waondolewe madarakani kwa njia ya maandamano zaidi badala ya kwa njia ya SANDUKU LA KURA, nikasoma habari kwenye internet inayowakejeli marais hawa ile mbaya juu ya madai yao hayo. Mwandishi huyo alikua akisema kwamba katika mataifa mengi sana wananchi hawajawahi kuchagua viongozi wa kuwaongoza kwa zaidi ya miaka ishirini au salasini huko.

  Kwa kuangalia kwa haraka haraka kauli hii mtu utadhani ni upuuzi mtupu tu ndio unaoongelewa hapa lakini ukizama zaidi kwenye kufiki utakuta kwamba kuna ukweli mzito mno nyuma ya hayo madai ya mwandishi huyo. Kwa mfano, itakua vipi mtu aliyeshinda kwa kishindo kama Hosni Mubarak (Asilimia 93 % kwenye uchaguzi wa mara ya mwisho) aliyekataliwa tu na Wa-Misri kiduchu asilimia 7 % akafikia mahala akatimuliwa na 'Nguvu ya Umma' madarakani hata kabla ya kufikia nusu ya awamu yake hiyo nyingine??

  Na tukirudi hapa nyumbani ni lazima tukajiuliza kwamba mbali huu wizi wa kura wa hivi majuzi wazi wazi kabisa kwa Rais Kikwete, je huko mwaka wa 2005 pamoja na ushindi kwake hivi ni kweli huyu ndugu KWELI KABISA alipata huo ushindi wa kishindo kwa asilimia hiyo hiyo 87 % au ndio haya haya tulioyaona mwaka jana??

  Kwa kweli ni kero, chukizo na udhia wa kila aina ambayo ni sharti lisawazishwe haraka mno ili heshima ya mwananchi KUJICHAGULIA KIONGOZI anayependezwa naye iweze kurejae nchini.
   
 17. msadapadasi

  msadapadasi JF-Expert Member

  #17
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  it is obvious, ccm wamepoteza mwelekeo na ushawishi kwa wananchi wake pamoja na uwezo wa kufkiria na ndo maana wamekosa hoja sera kwa mwenendo huu ccm italiangamiza taifa hili...
   
 18. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii ndo propaganda ambayo hatupashwi kuipa nafasi wakati tunapojadili mambo mazito yenye mustakabali wa Taifa.

  CHADEMA hawana sababu ya kufuata waraka wa wakatoliki wakati wana wafuasi wengi kwenye dini tofauti tofauti. Nadhani wakatoliki wa CHADEMA ni wachache ukilinganisha na Wapagani, Walokole, Waanglikani, Waislam, Wamorovian, Walutheran, Wapentekosti, Wasabato, nk walioko kwenye chama hicho!! Sasa CHADEMA watakuwa wajinga kiasi gani kufuata wachache na kuwaacha umma mkubwa ulioko nyuma yao?
   
 19. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kile chama kinachoamuru polisi kutumia risasi za moto kuzima maandamano.

  Ni kile chama kinachohonga sukari, chumvi hadi chupi kwenye chaguzi.

  Ni kile chama kinachohuribi kuna udini lakini hakichukui hatua yoyote.

  Chama chenye sera zisizotekelezeka naamini kinafahamika.
   
 20. GATS

  GATS JF-Expert Member

  #20
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 240
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unajua ndugu yangu hilo libambikiziwa na CCM ili kuweza kushinda ukweli sio huo. We angalia haohao wakatoliki mwaka 2005 walisema kikwete ni chaguo la mungu kwa vile leo wamewapinga CCM basi wanaiunga mkono CDM. Uwe na fikira nzuri ndugu yangu. Mbona 2005 walisema ni chama cha wachaga hilo leo halisemwi wewe huoni ni propaganda ?
   
Loading...