Hivi kwenye jukwaa la siasa ni kuzungumzia muda mwingi CCM,CHD na Kupakana matope kwa vyama hivyo,ina maana hoja za msingi kama KATIBA zimesahaulika? Nawasilisha.
Hapana hazijasahaulika ndiyo maana hata wewe umegusia kidogo hapa suala la katiba
CCM Wameuza Tanganyika yetu, Tutazungumzaje katiba bila Tanganyika. Tanganyika ndio platform yetu. Wao CCM wameshajipaka matope mpaka yakawa Gamba. Sisi tunachapia chipping wawe na mkwaruzo, Gamba limegoma kutoka.:evil:
Unajua hapa janvini panya kungura wameingia. Hakuna cha maana kinachojadiliwa hapa siku hizi. Baada ya wale wanachama wa Magamba kusikia kwamba JF inatumika kupaka matope chama chao basi wakaingia kwa nguvu zote sasa hakuna cha maana kinachofanyika hapa. Nimechukia sana na nasikitiswa sana na upuuzi unaoendelea hapa. baada ya mda si mrefu nitaiacha JF maana hakuna ninachogain siku hizi.
Ila naomba moderators watoe thread zinazofuka hapa. Kwa maana wanachama wengi wa chama cha Mangamba hukiri kwamba wao ni serikali na wanaitetea hata kama imefanya madudu. Naamini hii itawagharimu zaidi.
kwa hiyo mkuu unataka serikali ya Tanganyika na kuvunja muungano? Au unataka serikali 3?
Hukuna mtu anayechukia muungano, ila kwanini zanzabari ipo na Tanganyika imeondolewa. Tutaanzia wapi kuzungumzia katiba. Mimi ningependa serikali tatu au moja, lakini sio mimi ndie mwamuzi bali wana wa nchi.:israel:
Kwa ujumla Mimi sioni faida ya Muungano, na nimekuwa nafuatilia mazungumzo ya viongozi mbalimbali wanapo ulizwa wataje faida ya Muungano kwa miaka 50. Kwanza wanakimbilia kusema "zipo nyingi tu" nategemea wataanza kuporomosha moja baada ya nyingine kama tano mpaka kumi hivi. Cha ajabu waataishia kusema "tumeoleana, wapemba wanafanyabiashara Bara!" basi wanaishia hapo!
Najiuliza hizo ndo nyingi? Na ndiyo sababu kuu za Muungano?
Mimi sioni faida za Muungano!
Tunataka ccm wajivue hayo magamba waliyoyakiri kwamba wanayo kitu ambacho sidhani kama wanakiweza manake magamba waliyo ni nayo yanatisha na hayavuliki kirahisi ni tishio na magamba ni wao wenyewe mpaka dr slaa atinge ikulu ndio yatavuka..