Ccm na chadema jiandaeni kupokea matokeo matamu au machungu ya uchaguzi arumeru mashariki

MCHUMA MBOGA

Member
Mar 29, 2012
18
10
Kesho siku ya jumamosi tarehe 31. 03. 2012 ndiyo siku ambayo vyama mbalimbali vilivyojitokeza kuwania ridhaa ya wana Arumeru kuongoza jimbo hilo vitahitimisha kampeni zao. Mpaka sasa ni jambo la kumshukuru Mungu kwamba hatujasikia maafa makubwa ya mali kuharibiwa au mtu/watu kupoteza maisha. Pongezi kubwa kwa wana Arumeru Mashariki, vyombo vya ulinzi na usalama hasa Jeshi la Polisi na wanasiasa wote waliohubiri amani na maelewano na sio matusi na kashfa. Ieleweke wazi kwamba mwisho wa siku sisi wote ni Watanzania.

Katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika siku ya jumapili tarehe 01. 04. 2012 kitu cha msingi kabisa ni kwa wana Arumeru Mashariki kujitokeza kwa wingi wao na kwenda ktk vituo vya kupigia kura mapema na kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kumchagua mwakilishi wao bungeni. Mengi sana yameelezwa na wagombea na wapambe wao ktk majukwaa ya kampeni. Mambo ya kweli, mambo ya uongo, wengine wamemwaga sera, wengine wamemwaga matusi, kashfa dhidi ya wenzao. Lakini tar 1.4.2012 wana Arumeru Mashariki ndio mtachagua pumba na mchele. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Atakayejaribu kwa namna yeyote kuibadili sauti ya wana Arumeru Mungu amlaani hapa duniani na hata mbinguni.

Hata hivyo tumeshuhudia ktk baadhi ya chaguzi ambazo vyama upinzani vimeshinda basi wasimamizi wa uchaguzi wanapata kigugumizi cha kutangaza matokeo. Chondechonde msimamizi wa Uchaguzi huu wa Arumeru Mashariki usithubutu kukubali shinikizo lolote kuhusu kumtangza mshindi. Wewe tangaza mgombea yeyote atakayeibuka kidedea tena kwa haraka bila kuchelewa. Hata ukihamishwa kituo cha kazi (maana imetokea kama hujui uliza) lakini utakumbukwa kwa kutenda haki na hiyo legacy itaishi hata pale wewe utakapoondoka na Mungu atakubariki.

Kadhalika kumekuwa na tabia ya vyama vyama vya ushindani kulalama kila mara wanaposhindwa uchaguzi kwamba 'tumechakachuliwa'. Mnazidiwaje akili na hao wenzenu wakati na nyie ktk kila kituo mna mawakala? Anyway, kwa hili siwezi nikawalaumu sana kwani mbinu zinazoweza kutumiwa na mwenye fedha na vyombo vya dola ni nyingi kuliko zenu kwani baadhi ya mawakala wenu sio waaminifu- wanunuliwa na wenye fedha na kuwasaliti. Arusha ni ngome yenu kubwa, itumieni kulinda kura zenu!

Kuhusu wasimamizi wa amani hasa polisi. Hilo ni jukumu (law enforcement) ambalo mmepewa kisheria. Tekelezeni majukumu yenu kwa haki kama ambavyo mmekuwa mkifanya tangu kuanza kwa kampeni. Ukweli lazima usemwe siogopi kukosolewa kwa kile ninachokiamini.

Polisi wamejitahidi sana kuwa wavumilivu na kutekeleza majukumu yao kwa haki na usawa ktk uchaguzi huu mdogo wa Arumeru Mashariki kuanzia kipindi chote cha kampeni hadi sasa. Nimedokezwa kwamba wengi wa hawa vijana ni wapenzi wa CDM.(naomba usiniulize source ila kama hujui fuatilia utapata ukweli kwani yametokea) Kitu cha msingi ni kujipanga kutekeleza changamoto kubwa sana iliyoko mbele yenu- kusimamia haki siku ya uchaguzi 1.4.2012 na hatimaye kutangazwa kwa matokeo. Hiki ni nafasi yenu ya kujijengea heshima kitaifa na kimataifa. Msikubali kutumiwa, heshima yenu na imani ya wananchi juu yenu itazidi kuporomoka sana na jamii itawanyima ushirikiano ktk ulinzi ambao mnawaomba kila kukicha.

Kubwa zaidi, na hakika msingi wa uzi huu kuhusu utayari wa vyama vikuu vya ushindani ktk uchaguzi huu mdogo yaani CCM na CHADEMA (samahani sana kwa vyama vingine) ktk kupokea matokeo ya uchaguzi huu. Viongozi wa vyama hivi viwili mnayo dhamana kubwa sana juu ya hili kwani mnaongoza watu wengi ambao ni waaminifu kwenu na wanawasikiliza kiasi kwamba wako tayari hata kufa kwa nia ya kutekeleza maagizo yenu (imetokea kama hujui uliza), halafu wengine wana vyombo vya dola. Tutumieni madaraka mliyopewa kwa haki. Kumbukeni, Mungu yupo. Shauri yenu.

Mwisho, kwa atakayeshinda atekeleze ahadi alizotoa kuhusu suala la ardhi, umeme, maji, elimu, afya, huduma zingine za jamii kama soko, stendi nk nk. Kama ilikuwa ni changa la macho basi mtakarudi kutoa shkrani kwa kuchaguliwa waambieni wana Arumeru Mashariki kwamba ahadi hii na ile ilikuwa ni fiksi na muwaombe radhi.

Kazi kwenu wana Arumeru, kila la kheri na Mungu Ibariki Tanzania.

MCHUMA MBOGA.
 
Back
Top Bottom