CCM na CHADEMA Hamuwezi kututawala milele! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM na CHADEMA Hamuwezi kututawala milele!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Joblube, Sep 14, 2011.

 1. J

  Joblube JF-Expert Member

  #1
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 367
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Moja ya mambo yanayosikitisha ni pale mtu unayemtegemea kuwa anauwezo au akili fulani au busara lakini unakuja kukuta kinyume chake.

  Ndugu zangu watanzania napenda kuanza kwa kusema ule msemo kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na sio mwekezaji, wala mzungu bali ni mtanzania ataamua kujenga au kubomoa. Nayazungumza haya kwa machungu makubwa kwa kuwa naona Watanzania tunaelekea kubaya kwa sababu tuu ya watu wachache wenye uchu wa madaraka. Mtu mwenye akili timamu ni lazima atambue kuwa duniani Mungu ametuumba tofauti kunakuzidiana kiakili,kiuwezo wa hali namali, kuna wakati wa kupanda na kuna wakati wa kushuka, kuna wakati wa kiangazi kwa maana mambo huwa yanabadilika.

  Kutokana na hayo mabadiliko kwa mtu mwenye busara huwa anajiandaa na mabadiliko, mtu mjinga ataendelea kushangaa na na kuendelea kupambana akidhani anaweza kuzuia madadiliko.

  Nimeyazungumza hayo hapo juu kwa lengo la kuwashauri viongozi wa CCM na CHADEMA kuwa ni vizuri wakaelewa kuwa wao ndio wanaweza kusababisha amani ikawepo au ikatoweka kwa sababu tuu ya uchu wa kutawala wengine. Tutumie akili zetu vizuri kwa kujenga utamaduni wa kukubali pale mwenzio anapokuzidi na tuwe na moyo wa kusema kwa dhati kabisa katika hili, au kipindi hiki au wakati huu, au karne hii wenzetu wamenizidi kiaakili, kiuwezo na kisera pale inapodhihiri.

  Nimeyasema haya kwa sababu dalili si nzuri kwa viongozi wa CCM , yenyewe niwaonavyo wanafikiri ndio wenye hati miliki ya kutawala, hata pale dalili za wazi zinapoonyesha kuwa ni wakati wa kulia. Mimi niwashauri kuwa ni vizuri wakacheza siasa za kistarabu na haki kwa maana ya kujenga hoja kwa hoja wakishinda safi, mkishindwa sawa lakini Taifa likabaki na amani na watanzania wakaendelea kuwa wamoja (Taifa mbele chama baadaye). Na ndugu zangu tatizo liko kwa viongozi, wana CCM wakawaida hawana matatizo, mbona tupo wote humu mitaani tunashirikiana kwenye harusi na misiba. CCM mambo ya ukabila, udini, ukanda ili mradi tubaki madarakani tuyakatae ni hatari (Bomu baya sana).

  Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mlianzisha sera ya soko huru kuwa litaleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho na hivyohivyo waoneni wapinzani kama washindani wenu katika kuboresha maisha ya mtanzania na pale mnapozidiwa kubalini hamkuzaliwa mtawale milele hizo ni akili za watu wasio na upeo. CCM huu ni ushauri wangu bado ninawapenda kama watanzania wenzangu.

  Mungu Ibariki Tanzania
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ?..!!!!!! sijaelewa muelekeo.. nipangie hoja isiyo na mafumbo.. elezea kipi ni nini na kiweje.. Una mawazo kichwani basi uwe na uwezo wa kuyatandaza yakasomeka.. usiogope..
   
 3. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hujaelewa nini wewe? kama hata kiswahili kinakupa tabu,heb tupishe hapa
   
 4. M

  Mfwatiliaji JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,325
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  ..great thinker!! nadhani--kwa tafsiri yangu--ujumbe ni kuwa huu ni mwanzo wa mwisho
   
 5. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Bwana kweli haeleweki huyu katika kichwa cha habari anaonekana kulaumu CCM na CDM ukimfuatilia ni kama analaumu CCM peke yake kama haja onesha ubaya CDM mi nadhani hakupaswa kuweka kichwa cha thread namna hii,kwa aliyandika ni kweli ya kuwa CCM inajichukulia kama ina hati miliki katika kutawala hii nchi kuna mwisho.
  kwani miaka ya GHADAFI ni zaidi ya miaka ya CCM madarakani lakini akafika mwisho, kuna HUSSEN MUBARAK akatawala miaka mingi lakini mwisho ukamfikia na ndio maana ni nasema nina afiki kuwa CCM haitatawala milele,Na akitaka mwisho mbaya basi iendeleze haya inayoyafanya lakini kwa mwisho mwemana amani basi ni lazima wakafuta umma unataka nini.
   
 6. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hata wewe Pia hujaelewa Mada Unakurupuka kutukana tu..Sasa wewe una tofauti gani na hao Jamaa anaowaomba Wawe wastahimilivu??..Kwani kama Hoja ya Mwenzio Imekukera Ndio Utukane?..Si na wewe umjibu kwa Hoja??..Inaonyesha Jinsi Gani Usivyo Mstaarabu!!
   
 7. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu, muanzisha thread baada ya kutambaa ni hiyo mistari yako mwisho naomba uniambie wewe unasimama wapi kwenye ili jambo?
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  acha haki itawale milele na siyo ccm wala chadema..
   
 9. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #9
  Sep 14, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  kandambili inaweza kuwa kiatu.. na hasa kwa mtoko!! ila ni mkosi kuwa na kinywa chenye matusi ndani ya JF... usijal.. nakusamehe.. you are welcome
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  mi mwenyewe sijamwelewa nimerudia mara 3 ili nione kosa la CHAMEMA kwa wa TZ sijailiona ila kwenye heading kawashutumu, pia aeleze sbb za kutaja CCM na CDM wkt ht CUF kina wabunge wengibara na visiwani?hapo ndo nahtaji maelezo kdg ili niamue kuunga mkono hoja au kutemana nayo.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Sep 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu nakuona unamung'unya maneno na umeshindwa kusema ukweli sijui kwa sababu ya mapenzi yako au ulitaka kuwalaumu CCM pekee wakati umewataja na CDM. Labda mimi nikusaidie ktk hili na hawa viongozi wetu wa vyama vyote vya kisiasa wapate kutuelewa kwamba wananchi tumechoka na hizi siasa za majitaka. Tumechoka na unafiki wa siasa ambao unatazama kwanza maslahi binafsi na kwa mafanikio yao wao hali wananchi wanazidi kuangamia.

  Maafa mengi yametokea na tukianza na lile la kuzama kwa meli ya Mv. Bukoba, Treni liyoharibika na kurudi nyuma huko Dodoma, maafa ya Same na Manyara, njaa na ukosefu wa huduma muhimu kama maji na Umeme. Kisha hii meli ya Zanzibar ilozama majuzi, vitu vyote hivi vimetokana na uzembe mkubwa unafanywa na viongozi wetu ktk nafasi zao lakini katu hatujawahi kuona wala kusikia shinikizo la wahusika kuchukuliwa hatua toka upande wowote zaidi ya hizi siasa za kumtaka JK, Waziri mkuu Pinda au waziri yeyote ajiuzulu kwa sababu za kisiasa zaidi.


  Kinachotuchosha zaidi ni pale hawa viongozi wetu wa upinzani tuliowachagua wanapotugeuka pindi wanapopewa wadhifa ktk serikali hii ili hali wao walikuja na nguvu kubwa ya kupinga sera na ilani za chama tawala. Leo hii wengine wamechaguliwa kushika wadhifa ktk kamati za Bunge wamebalisha kabisa kauli na matumaini yao na kufikiria kwamba sera za CCM zinaweza kuboresha maisha ya wananchi. Mtazame Maalim Seif, Mrema, Cheyo na hata Shibuda ni watu ambao walikuwa machachari sana ktk upinzani leo hii wameshikwa nakuwa watetezi wazuri wa mfumo mfu wa maendeleo wa CCM. Leo hii wamejiunga na chama wakiendesha siasa za majitaka bila kutazama wananchi tunaathirika vipi..

  Kwa mpinzani yeyote ambaye leo hii anaweka matumaini ktk maendeleo ya nchi yetu hali akijua fika kwamba sababu ya uongozi mbovu nchini sio WATU bali ni mfumo mbaya ambayo umetokana na kutokuwa na DIRA ya kitaifa, aidha dira hiyo tumeipoteza. Tanzania ya leo ni nchi inayokwenda kama jahazi la kutumia nyota na hakika hatufahamu tuendako wala hali ya hewa isipokuwa kwa baraka zake Mola, tunaomba kila siku tufikishwe ufukoni mahala popote penye uhai kutunusuru na dhoruba za maafa. Tumeshindwa kujiandaa ktk maafa na zaidi ya hapo tunashindwa hata kukidhi mahitaji yetu hivyo SHIDA zinazidi kupandiana..

  Leo hii serikali yetu inahudumia DHIKI na mipango ya kuokoa kama vile tupo Somalia kwenye vita na ukame. Matumaini yetu ni misaada kutoka taasisi za wahisani ambao tunashindwa kuwapa masharti ya kibiashara kutokana na adha tulizonazo. Na ni katika mfano huu tunawapata viongozi ambao siasa zao zinatazama zaidi mgao wa misaada badala ya kutafuta mbinu za kuondokana na shida zetu. Inakuwaje, mbunge anapopewa wadhifa ktk serikali au kamati za bunge huanza kutetea bajeti ya serikali ambayo UFISADI ndio umeiweka madarakani? ni kitu gani kinachowapa tumaini viongozi hawa ikiwa sera za chama tawala ni zile zile walizokuwa wakizipiga vita miaka ya nyuma.

  Je, kuongezwa fedha ktk bajeti ya wizara ya nishati na madini kunaweza kuondoa adha ya umeme nchini ikiwa fedha hizi zimetawaliwa na mfumo mfu wa kiutawala?.. Hivi kweli tunapoendelea kukodisha wazalishaji wa umeme wenye kutumia mafuta (Petrol) yenye gharama kubwa badala ya kuimarisha na kuboresha usambazaji na matumizi ya gas na Upepo kweli tunaweza kuondoa tatizo la umeme nchini ktk nchi maskini..Je hivi kweli matumizi ya makaa ya mawe yanaweza kuzalisha umeme mkubwa zaidi na salama kuliko nguvu za upepo na jua?..

  Halafu tutazame swala la Posho! vyama vya Upinzani vimechukua hatua gani kuhakikisha posho zao zinarudi kwa wananchi hata kama serikali imekataa kuziondoa?..Pamoja na upinzani wa posho hizi wabunge wetu wameshindwa kuendeleza Upinzani wa Mh, Dr. Slaa ambaye aliweka madai ya hata mishahara ya wabunge ipunguzwe, leo hii serikali imeongeza majimbo, vikao vya bunge na kamati zake, ongezeko la tume za bunge na rais ktk kuchunguza maswala ambayo hayapati ufumbuzi wala kubadilisha sheria. Na bado tunatumikia Azimio la Zanzibar ambalo limeondoa kabisa miiko na maadili ya viongozi na kibaya zaidi tunakusudia kuunda Jumuiya ya nchi za Mashariki ambayo viongozi wake wanapokea mishahara mikubwa kuliko hata nchi tajiri kama Marekani na Uingereza. Hivi kweli maskini wanapounganisha nguvu kuongeza sahani za biriani hupunguza njaa au ndio ktk kugawana umaskini maanake ujazo wa biriani yenyewe haukuongezeka wala hautoshelezi sehemu zote toka mwanzo.

  Itafika wakati wananchi watachoka na hizi siasa za vyama vingi na wao wenyewe watachukua jukumu la kutafuta mabadiliko ya kweli. Kusema kweli kwa jinsi tunavyojisuasua na kuubeba kwa mbeleko UFISADI mkubwa unaofanyika nchini ni hatari zaidi kwa vyama vyote na itafikia wakati wananchi watashindwa kuwaamini viongozi wao. Kama wewe mwanasiasa na umeamua kujiingiza ktk siasa basi la kwanza ni kutazama maslahi ya Umma na kuzitafisiri sera za chama chako kama dira ya kuwaletea maendeleo na sii kufuata nafasi yako mwenyewe ktk utawala kwa sababu huwezi kufanya mabadiliko yeyote ikiwa hujakabidhiwa nyenzo za kufanya mabadiliko hayo.

  Nawasilisha..
   
 12. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  CDM wanaingiaje kwenye lawama zako maana sijaona sehemu umeelezea matatizo ya kutawaliwa na nao, Rekebisha hiyo heading
   
 13. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh sijaelewa kabisa hapa..................hbu edit na uweke flo nzuri
   
 14. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  hivi CHADEMA wameanza kutawala nchi hii ???????????
   
 15. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #15
  Sep 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Tatizo si kwa Chadema ni Ccm kutokutaka mabadiliko mahali chadema wanakubalika watawatumia Polisi Usalama wa Taifa na hata Tume ya uchaguzi kuiba kura , Amani itapotea wananchi kutokukubali dhuluma, na Nchi hihi damu imeshamwagika na itamwagika Kama CCM hawatakubali mabadiliko
   
 16. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #16
  Sep 15, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu hoja yako ha&#305;na mash&#305;ko
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu vipi ? Huu ujumbe una maana gani ? Unawasema Chadema au CCM maana uyasemayo na kichwa chako cha habari ni mkanganyiko .
   
 18. c

  chama JF-Expert Member

  #18
  Sep 15, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Karibu safu nzima ya uongozi Chadema ni mizoga ilyotoka ndani ya uozo wa CCM. Chadema haijatawala na wala haitatawala, ukombozi wa kweli wa mtanzania utaletwa na watanzania wenyewe. Siku watanzania wa kawaida watakaposema basi ukombozi utapatikana, AMANI NA NJAA haviendi pamoja.
  Chama
  Gongo la Mboto DSM
   
 19. C

  Chief Ken Lo Member

  #19
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwenye red umenena mkuu...
   
 20. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #20
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,319
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Hii Thread ni sawa na chakula kilichoandaliwa wageni waliokaa sitting room na mwaandaaji akakiacha jikoni na kuifuatilia huko ni ngumu kwa sababu ugeni.

  Edit habari halafu uilete tena, uwe muwazi nani anafanya nini na wapi then we can participate?????????????
   
Loading...