CCM na CHADEMA Hamuwezi kututawala milele!

CCM na CHADEMA Hamuwezi kututawala milele!

kunatatizo hapa! na tatizo lenyewe ni kuwa kila mtu sasa amefuzu mbwembwe za uongo. mi nadhani tuwe waungwana tu kwa kuwaachia wanao weza kupanga hoja wapange, na kama unaona mwenzio hakupanga unatakiwa kufahamu kabisa kuwa mtoa mada ametamka kuwa watu tunauwezo tofauti wa kufikiri na akili pia, sasa huu ubabe wa kutusi unatoka wapi?

binafsi nadhani niwakati muafaka wa kutokuwa na chama ililetea maendeleo nchi hii ikiwezekana tutofautiane wakati wa uchaguzi tu na tunapo maliza swala hilo basi tuwe namshkamano wa kitaifa ili kujenga nchi yetu.

ushauri wangu kwa CCM kwa heshima ya walipo tutoa katika nchi ya ASALI NA MAZIWA huku wanapo taka kutupeleka watuache sasa tunaweza kwenda wenyewe kwani tumea sasa na tunaona siwezi kuingia kwenye nchi ya GIZA, HAKUNA MAFUTA, HUDUMA MBOVU ZA HOSPITALI, BORA MAISHA, MIUNDO MBINU MIBOVU, NA KUTHAMINI WAGENI KWA HELA ZAO NA KUTUACHA SISI WAZAWA AMBAO TUMETUNZA ARDHI YETU MAKABWELA, sipo tayari kuingia nchi hii ambyo inawezekana kabisa viongo zi tulio waamini hawaoni haya. NAJUTIA KURA YANGU NAMUOMBA MUNGU ANISAMEHE. Ila naamini sintakufa hadi nitakapo yashuhudia haya mabadiliko ya kweli.
 
(Taifa mbele chama baadaye). Na ndugu zangu tatizo liko kwa viongozi, wana CCM wakawaida hawana matatizo, mbona tupo wote humu mitaani tunashirikiana kwenye harusi na misiba. CCM mambo ya ukabila, udini, ukanda ili mradi tubaki madarakani tuyakatae ni hatari (Bomu baya sana).

Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mlianzisha sera ya soko huru kuwa litaleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho na hivyohivyo waoneni wapinzani kama washindani wenu katika kuboresha maisha ya mtanzania na pale mnapozidiwa kubalini hamkuzaliwa mtawale milele hizo ni akili za watu wasio na upeo. CCM huu ni ushauri wangu bado ninawapenda kama watanzania wenzangu.

Mungu Ibariki Tanzania

Karibu sana kwenye kampeni ya Tanzania Mbele vyama sio lazima viwe dila yetu,kuthibitisha uzawa na uzalendo kwa Mama Taifa Tanzania.Kwnye Red ndio vya kuangalia kwa jicho la tatu.
 
hamjaelewa nini huyu jamaa ni pro wa cdm,nia yake ni kuwahabarisha ccm na kuwatahadharisha chadem.
halafu wengine mnajiita gt wakati vichwa vinachelewa kufungua.
 
Ndugu Chama

Nina mashaka na wewe. Huna akili (Chizi) au uwezo wako wa kufikiri ni mdogo.
 
Karibu safu nzima ya uongozi Chadema ni mizoga ilyotoka ndani ya uozo wa CCM. Chadema haijatawala na wala haitatawala, ukombozi wa kweli wa mtanzania utaletwa na watanzania wenyewe. Siku watanzania wa kawaida watakaposema basi ukombozi utapatikana, AMANI NA NJAA haviendi pamoja.
Chama
Gongo la Mboto DSM
sasa tupe mbadala; umesimamia wapi wewe?! tungoje hadi lini watanzania watakapoAMUA?
nini kinahitajika ili waelewe na wajielewe?! chachu ni ipi hapa?
sitaki statements za mkato wa tamaa!! tunahitaji uchambuzi hapa!
 
Moja ya mambo yanayosikitisha ni pale mtu unayemtegemea kuwa anauwezo au akili fulani au busara lakini unakuja kukuta kinyume chake.

Ndugu zangu watanzania napenda kuanza kwa kusema ule msemo kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na sio mwekezaji, wala mzungu bali ni mtanzania ataamua kujenga au kubomoa. Nayazungumza haya kwa machungu makubwa kwa kuwa naona Watanzania tunaelekea kubaya kwa sababu tuu ya watu wachache wenye uchu wa madaraka. Mtu mwenye akili timamu ni lazima atambue kuwa duniani Mungu ametuumba tofauti kunakuzidiana kiakili,kiuwezo wa hali namali, kuna wakati wa kupanda na kuna wakati wa kushuka, kuna wakati wa kiangazi kwa maana mambo huwa yanabadilika.

Kutokana na hayo mabadiliko kwa mtu mwenye busara huwa anajiandaa na mabadiliko, mtu mjinga ataendelea kushangaa na na kuendelea kupambana akidhani anaweza kuzuia madadiliko.

Nimeyazungumza hayo hapo juu kwa lengo la kuwashauri viongozi wa CCM na CHADEMA kuwa ni vizuri wakaelewa kuwa wao ndio wanaweza kusababisha amani ikawepo au ikatoweka kwa sababu tuu ya uchu wa kutawala wengine. Tutumie akili zetu vizuri kwa kujenga utamaduni wa kukubali pale mwenzio anapokuzidi na tuwe na moyo wa kusema kwa dhati kabisa katika hili, au kipindi hiki au wakati huu, au karne hii wenzetu wamenizidi kiaakili, kiuwezo na kisera pale inapodhihiri.

Nimeyasema haya kwa sababu dalili si nzuri kwa viongozi wa CCM , yenyewe niwaonavyo wanafikiri ndio wenye hati miliki ya kutawala, hata pale dalili za wazi zinapoonyesha kuwa ni wakati wa kulia. Mimi niwashauri kuwa ni vizuri wakacheza siasa za kistarabu na haki kwa maana ya kujenga hoja kwa hoja wakishinda safi, mkishindwa sawa lakini Taifa likabaki na amani na watanzania wakaendelea kuwa wamoja (Taifa mbele chama baadaye). Na ndugu zangu tatizo liko kwa viongozi, wana CCM wakawaida hawana matatizo, mbona tupo wote humu mitaani tunashirikiana kwenye harusi na misiba. CCM mambo ya ukabila, udini, ukanda ili mradi tubaki madarakani tuyakatae ni hatari (Bomu baya sana).

Ndugu zangu ni nyinyi wenyewe mlianzisha sera ya soko huru kuwa litaleta unafuu kwa mtumiaji wa mwisho na hivyohivyo waoneni wapinzani kama washindani wenu katika kuboresha maisha ya mtanzania na pale mnapozidiwa kubalini hamkuzaliwa mtawale milele hizo ni akili za watu wasio na upeo. CCM huu ni ushauri wangu bado ninawapenda kama watanzania wenzangu.

Mungu Ibariki Tanzania
Nikuulize kidogo! Umevitaja vyama viwili katika heading yako lakini maelezo unamsema mmoja huyo mwingine ana kosa gani? Ungesema hivi: CCM HAMUWEZI KUTAWALA MILELE.
 
Mtoa mada unaongea kwa mafumbo unafikiri kila mtu ana muda wa kukaa chini na kutafsiri mafumbo yako? Watu tuna kazi nyinginea za kufanya zaidi ya kutafakari habari zisizoeleweka.
 
Ndugu Chama

Nina mashaka na wewe. Huna akili (Chizi) au uwezo wako wa kufikiri ni mdogo.
Mungu wangu kashfa si mahala pake hapa, tuvumiliane. Uliyetengeneza tatizo huwezi kulitatua tatizo hilo mwenyewe utasaidiwa na wenye uwezo zaidi yako. CCM katengeneza matatizo awaachie wanaomzidi uwezo wamsaidie kulitatua tatizo.
 
hamjaelewa nini huyu jamaa ni pro wa cdm,nia yake ni kuwahabarisha ccm na kuwatahadharisha chadem.
halafu wengine mnajiita gt wakati vichwa vinachelewa kufungua.

Ah Mie hiyo avatar yako mkuu.. ah!! ingekuwa wakati wa swaumu!! do.. afu mie picha ile nilikuwa sijaielewa ki vile.. kumbe ni kwamba Hicho chama kimeweka misahani ya Wali mbele ya wananchi, lakini wameweka walinzi ili wananchi wasifikie mlo.. mlo kwa wakubwa tuu.. aisee fumbo limetulia hili...
 
Ndugu Chama

Nina mashaka na wewe. Huna akili (Chizi) au uwezo wako wa kufikiri ni mdogo.

dguyana,
Nadhani wewe ndiye uliyekurupuka kuongea kama chizi, upeo wako wa kuelewa ni mdogo sana unashabikia siasa kama mpira, Chadema kimefanikiwa kuvuna wanachama si kwasababu wamekubaliana na sera za CDM la hasha! Bali watanzania wamekata tamaa CCM kutokana na hali duni ya maisha, ukirudi ndani ya hiyo mizoga iliyotokana na uozo wa CCM akiwamo Dr. Slaa akili zao zinafanana na viongozi wa CCM wanachojali ni maslahi yao binafsi. Labda nikukumbushe unakumbuka Mh. Zitto alipogomea posho? Je wabunge wangapi wa Chadema waliungana naye? Mh. Zitto alifanya hivyo kwa kuleta changamoto ndani ya bunge, matokeo yake wabunge wenzake wa Chadema walimsaliti sikusikia wabunge wa Chadema waliojitokeza hadharani kuungana naye wengi waliomuona kama msaliti wa matumbo yao, akili zao sawasawa na za wabunge wa CCM wanachojali ni maslahi binafsi.
Chama
Gongo la Mboto DSM
 
sasa tupe mbadala; umesimamia wapi wewe?! tungoje hadi lini watanzania watakapoAMUA?
nini kinahitajika ili waelewe na wajielewe?! chachu ni ipi hapa?
sitaki statements za mkato wa tamaa!! tunahitaji uchambuzi hapa!

Kitu gani ambacho hujaelewa? Chadema ni copy and paste ya CCM, viongozi wengi waliopo Chadema ni makapi yanayotokana na CCM bado kiakili na kimaadili wapo CCM, na hii ndiyo sababu kubwa inaoyoifanya Chadema ikose mbinu mbadala wa kuingusha CCM. Chadema kimekosa uwezo wa kutafuta pesa za kujiendesha inachosubiri ni ruzuku kutoka kwa wapinzani wao CCM (ndiyo inayoendesha serikali) jiulize Dr. Slaa yupo tayari kukosa milion 7 kwa mwezi? Ukweli wa mambo Dr. Slaa na viongozi wenzake hawapo tayari kukosa posho zao, watapiga sana kelele kwenye majukwaa kuisema CCM mwisho wa siku wanachokifanya ni kusubiri pesa kutoka CCM. Ruzuku si haki ya chama chochote kile ni mtego maalum wa kuwatega viongozi dhaifu kama Slaa. CCM wamefanikiwa sana na mtego posho Maalim Seif alikuwa ni mpinzani halisi mpaka siku alipoanza kupokea posho kutoka kwa wapinzani wake serikali ya mapinduzi Zanzibar. Mheshimiwa Odinga (Kenya) amefanikiwa kuwa mpinzani wa kweli alikataa ruzuku na posho kutoka kwa Kibaki, hata baada ya uchaguzi wa Kenya walijaribu kumrubuni kwa pesa na vitisho walishindwa kutokana na upinzani wa kweli. Tanzania tutapata mapinduzi ya kweli siku sisi watanzania wenyewe tutakopoamua kuingia mitaani kupinga dhuluma zinazoendelea na si kutegemea huu utitiri wa vyama vya siasa ambavyo viongozi wake wapo kutetea matumbo yao.
Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Back
Top Bottom