Jana nimeshudia tambo za wapambe pale Dodoma na makada wa ccm kiasi kwamba zimezidi kupita kiasi. Inaelekea sasa ccm inashindwa kutofautisha kati ya serikali na chama cha siasa.
Kilicho nistua zaidi ni kuambiwa kuwa sasa sisi sote ni watumwa hapa nchini na mabosi wetu ni ccm. Hizi ni tambo za hali ya juu Sana kuwahi kutolewa duniani na chama chochote cha siasa.
Nacho jua Mimi CCM ilitukuta watanganyika tukiishi maisha yetu kwa Amani kabisa. Ikaomba tuishi wote tukaikubalia Leo ndo imekuwa mabosi na kututaka tuisujudie ili hali iliomba urai kwetu tukaipa?
Mkumbuke kiburi cha chama cha KANU kule Kenya na matokeo yake sasa yamekifikisha wapi. Jina la Rais wa Kenya kwa sisi tulio ishi zamani tunakumbuka lilikuwa linatanguliwa na neno Mtukufu halafu ndio unataja jina lake.
Msisahau msemo wa wahenga usemao sikio huwa halizidi kichwa jamani.