CCM muwe mnaacha na maneno ya akiba

CCM muwe mnaacha na maneno ya akiba

Lituye

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
1,864
Reaction score
5,697
Jana nimeshudia tambo za wapambe pale Dodoma na makada wa ccm kiasi kwamba zimezidi kupita kiasi. Inaelekea sasa ccm inashindwa kutofautisha kati ya serikali na chama cha siasa.

Kilicho nistua zaidi ni kuambiwa kuwa sasa sisi sote ni watumwa hapa nchini na mabosi wetu ni ccm. Hizi ni tambo za hali ya juu Sana kuwahi kutolewa duniani na chama chochote cha siasa.

Nacho jua Mimi CCM ilitukuta watanganyika tukiishi maisha yetu kwa Amani kabisa. Ikaomba tuishi wote tukaikubalia Leo ndo imekuwa mabosi na kututaka tuisujudie ili hali iliomba urai kwetu tukaipa?

Mkumbuke kiburi cha chama cha KANU kule Kenya na matokeo yake sasa yamekifikisha wapi. Jina la Rais wa Kenya kwa sisi tulio ishi zamani tunakumbuka lilikuwa linatanguliwa na neno Mtukufu halafu ndio unataja jina lake.

Msisahau msemo wa wahenga usemao sikio huwa halizidi kichwa jamani.
 
Hawajiulizi mwaka huu wamepokea wanachama wawili tu ambao mmoja angalau kakaa upinzani miaka zaidi ya mitano na mwingine hata mwaka hajamaliza, last time kipindi cha kina Shonza walikuwa kadhaa hii ni dalili ya increasing at diminishing rate kwa wachumi
 
Kaka uminifurahisha sn na kweli wwe mchambuzi wa political analysis,kwa kauli ya jn kwamba sisi ni wanyapara wa wanasiasa nadhani huu ni upotoshwaji mkubwa,sisi ni watumishi wa umma tusilazimishwe kujiunga na vyama vya kisiasa au kuwa makada tukifanya ivo tunakosea sn na tutaanza kubaguana sisi wenyewe!,mambo ya siasa hazichangamani na issues za utumishi wa umma!
 
kiujumla katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi kauli ile ya rais haikuwa nzuri kwa kweli....
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm, kwa hiyo wafanyakazi wote wanatakiwa kutekeleza ilani ya ccm
 
Umma ni pamoja na CCM!
 
Ilani iliyoshinda uchaguzi ni ya ccm, kwa hiyo wafanyakazi wote wanatakiwa kutekeleza ilani ya ccm
Mmemtia doa na dhambi kuu mzee Lubuva wa watu.
Hilo liilani lenu kalitekelezeeni SUKITA!!!
 
Nadhani hukusikia vizuri. Ilani inayoenda kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano ni ya CCM!Serikali iliyoko madarkani ni ya CCM!So wana ccm wanahaki ya kuhakikisha ilani ya chama chao inatekelezwa, na wanahaki ya kuhoji kama mambo hayaendi kama walivyoyaandika kwenye ilani yao!Hii ni kwa sababu waliinadi na tuliwachagua ili waitekeleze, so kama mtu atapingana nao huyo ni adui wa maendeleo kutokana na ilani yao!NI kweli wao ndio mabosi
 
Ccm INA mabosi na mabosi hao ni familia za nape,mwinyi,karume,makamba,nyerere,kawawa,mafisadi
 
kiujumla katika kipindi hiki cha mfumo wa vyama vingi kauli ile ya rais haikuwa nzuri kwa kweli....
Ktk maisha haya ya mfumo wa vyama vingi ile ni kauli ya kuligawa taifa. Yaani wale wasio wana CCM au wasiyo wana chama wa chama chochote hawatakiwi ktk nchi hii.

Magufuli ana kauli chafu sana, anaropoka tu kama sijui nini. Sidhani kama anajitambua kama yeye ni Rais
 
Mmemtia doa na dhambi kuu mzee Lubuva wa watu.
Hilo liilani lenu kalitekelezeeni SUKITA!!!
Ilani imeahidi, elimu bure, maji, madawa , etc.

Sasa ajitokeze mtumishi wa serikali kigango Fulani wakupinga elimu tumuone
 
Ni wakali tu wa tambo na nahau ila ni weupe km theluji na wepesi km pamba situnaona mjengoni.
 
Kuna Mtu Hajakuja Kwenye Hii Thread Anaitwa Lizaboni
Kwenye Kupenda Haoni Chongo Cha Ccm Atasema Kengeza
 
Back
Top Bottom