Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
- Thread starter
- #21
CCM wanadharau wananchi kuliko hata unavyofikiri.
Mkuu,karibu Kibaha ujionee Sobibor 2015
CCM wanadharau wananchi kuliko hata unavyofikiri.
Mleta uzi.hiv ukimleta diblo dibala,dally kimoko na wapiga gita wote maarufu halaf wawapigie mbuzi gita watawaelewa kwel
Si jambo jema. Kura zitanguliwe na ubinaadamu. Siku ya Jumamosi,kulitokea ajali iliyohusisha pikipiki na lori maeneo ya Visiga Kibaha Pwani. Ni kwenye kona mpya ya Visiga Seminari. Katika ajali hiyo,mwendesha pikipiki alifariki papo hapo huku pikipiki yake yote ikiteketea kwa moto.
Ni siku hiyo hiyo,msafara wa CCM ukiongozwa na Kinana na Nape ulikuwa unaelekea Mlandizi baada ya mkutano wa Mailimoja siku ya Ijumaa. Wakati watu wakikusanyika kumsitiri na kumuondoa marehemu kuelekea hospitali,msafara wa CCM ukapita.Wakati huo maiti ipo na pikipiki linawaka.
Pamoja na watu wengi kuwa eneo la ajali,msafara haukusimama. Kubwa zaidi,gari la matangazo lilizidisha sauti na kuweka taarabu. Hakika,marehemu alikuwa anaonekana pale. Wananchi waliguswa sana na jambo hilo. Hawakuamini walichokiona. Ajalini kweli ipigwe taarabu??!?
Wananchi wamefikia kuuliza,wangekuwa wa vyama vya upinzani wangepita wakipiga taarabu? Naomba wahusika wasirudie tena. Nasema,kura na sera zitanguliwe na utu.Wananchi wa Pwani sio cheap kihivyo!