CCM mpo nyuma ya mchezo huu? Mwaitambua hatari iliyopo??

CCM mpo nyuma ya mchezo huu? Mwaitambua hatari iliyopo??

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,519
Nimeiangalia video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayosemekana ni kundi lililojitangaza kuwa ndilo lililotekeleza uvamizi wa vituo vya polisi na kupora silaha huku ukienda sambamba na mauaji ya polisi,

Imenilazimu kurejea nyuma kuyaangalia matukio yenye kufanana na haya (ugaidi) na siasa za nchi hii, ni ukweli usio na chembe ya shaka chama tawala kwa miaka mingi kimekuwa kikitumia mwavuli wa ugaidi kisiasa kujinufaisha kisiasa bila kujali athari za utumizi huo kijamii.

Nimeirudia mara kumi kuiangalia video ile, nikachangaya na "zangu", hakika video ni halisi, kwa lengo halisi, kwasababu feki. Video haina maandalizi ya kigaidi, haina ladha ya kigaidi na haina kusudio la matukio yaliyotokea hivi punde, ni video inayoleta picha ya kupangwa kisiasa zaidi ya uhalisia wa yaliyotokea. Huu ni muono wangu.

Mwaka 2000 IGP Omar Mahita akishirikiana na CCM ya Mkapa walikula njama za kuihusisha CUF na ugaidi kwakutengeneza visu vyenye mpini ya rangi ya bendera ya CUF kisha Mahita akaenda mbele ya vyombo vya habari na kuitangazia dunia kuwa wamekamata kontena la visu vya Chama cha CUF, ilihali akifahamu fika visu vile vilitokea sido tena havizidi 20,
Hii ilikuwa njia ya kuleta hofu kwa umma na watu wasiipigie kura CUF kwakuwa ni chama cha kigaidi,

Mwaka 2012 mchezo huo huo ulijirudia kwa Chadema kupakaziwa Ugaidi kupitia kwa mkurugenzi wake wa ulinzi na usalama Bwana Rwakatare, mchezo huu uliratibiwa na CCM ya Jakaya Kikwete, jeshi la polisi la Said Mwema na Idara ya Usalama wa Taifa ya Othuman Rashid, Kama sio uimara wa wanasheria wa Chadema tu, leo Chadema ingekuwa historia tu,

Baada ya Muungano wa UKAWA kumekuwapo na juhudi za kila aina za kuusambaratisha lakini zinagonga mwamba, Chama cha mapinduzi kimeishiwa sera na kukosa uhalali wa kuongoza kabisa, na sasa kipo kwa nguvu ya vyombo vya dola tu.

Harakati za kuuvuruga Ukawa zilianza kwa haribio la udini ambalo, kwamba mswada wa marekebisha ya sheria ili kutambua mahakama ya Kadhi nchini. Jaribio hili lilikuwa ovu na lilikuwa na lengo kuamsha mtazamo chanya na hasi ya UKAWA katika udini, lakini wakuu wa Ukawa waliuelewa mchezo na wakatulia tulii. CCM na serikali yake walipoona hakuna dalili za kutimia kwa lengo la kuwagawa UKAWA wakainuka na kutangaza kuwa wameuondoa mswada huo bungeni, lakini ukweli nikuwa hakuna mswada wenye kurekebishwa sheria ili kutambua mahakama hiyo ya kadhi. Ulikuwa ni uzushi wa lumumba tu.

Mpango mkakati mwingine ni huu unaoitwa uvamizi na uporaji silaha ndani ya vituo vya polisi, "inavyoonekana mpango huu uliandaliwa kwa mda mrefu, Kwakuwa mwaka 2014 uliandamwa na maandamano kila kuchapo, hivyo mwaka huu kupitia mkakati huu wa kinachoitwa tishio la wapora silaha, basi maandamano yote yatapigwa marufuku. Hili limeanza kufanikiwa.

Hatua ya pili nikuwa kundi hili la washirika wa ccm (muono wangu) lipo kwenye hatua ya kuhusisha UKAWA na UGAIDI kwamfumo wa mambo matatu, kwanza video hiyo iliyotolewa hivi sasa inayoonyesha kundi hilo lina chuki na Polisi na serikali,

Hatua ya tatu itakuwa video ya kundi hilo likiwataka watanzania kutoipigia kura ccm, na badala yake wapigie kura Ukawa. Na video hii inaweza kutolewa miezi miwili ama mmoja kabla ya uchaguzi mkuu,

Hapo ndipo ccm na washirika wake watakapo utangazia umma kuwa UKAWA inafadhiri ugaidi, na propaganda hii itapigwa kwa nguvu kubwa kupitia vyombo vya habari walivyoviteka karibu vyote hivi sasa.

Lakini je, jini ukilitoa kwenye chupa ni rahisi kulirudisha kama ccm wanavyoamini? CCM mnalitakia mema taifa hili kweli ama nyie mtaishi sayari nyingine kwa hilo jini mliloliunda likigoma kurudi chupani?
 
Kama wamepata video inakuwaje washindwe kuwakamata haomwatu wakati wana record video hii. Kama ulivyosema Yericko hii ni move ya CCM +Polisi+ TISS. Kama wasingekuwa wao kwa kutumia intelijensia wanayoihubiri kila kukicha eti wameona kuna ugaidi umepangwa kufanyika, wangekuwa wameshawakamata wahusika.

CCM +Polisi+ TISS ni wahuni tu, wanataka kutuchezea watanzania. Ila kwa uweza wa mungu hawatafanikiwa kamwe kuwavuruga watanzania kwa manufaa ya matumbo yao.

Mbona intelijensia yao huwa haioni mafisadi wa pesa za umma kama Escrow. Eti intelijensia yao ni kuona ugaidi utakaotokea kwenye maandamano. Wanadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho.
 
Possibly kwa sababu hii video ukiiangalia imekaa kimtego, mtego; Na anapoongelea Uvamizi wa Vituo vya polisi kama ushirombo si kweli maana Slaa zote walizikamata na watuhumiwa kutiwa mbaroni.

Hivyo hii Video inaweza kweli ikawa na malengo yale yale ya Majambia ya IGP Mahita kipindi CUF ipo kwenye Chart.
 
Hili nalo nenooo hawa watu washakula nyama ya mtu kwa hiyo ni vigumu kuiacha na ndio maana wanafanya juu chini kuudhoofisha upinzani lakini wameshindwa na wamelegea kila idara sisi tunasema tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu.
 
Hili nalo nenooo hawa watu washakula nyama ya mtu kwa hiyo ni vigumu kuiacha na ndio maana wanafanya juu chini kuudhoofisha upinzani lakini wameshindwa na wamelegea kila idara sisi tunasema tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu.

Mpaka u quote Habar nZima
 
Jericho, unaweza kuwa sahihi kwamba kwa hali yoyote ccm haiwezi kujitoa katika uhusika wake na uharibifu wowote Tanzania.

Iwe ni kwa hiyari au matokeo ya mikakati yao ya kishetani, ama kwa uzembe na kushindwa uongozi wa nchi.

Lakini hawa kusema kwamba chombo hiki kitahusishwa na ukawa moja kwa moja, inamaswali mengi. Hawa magaidi wamejibainisha kwamba wanalenga kupambana na Wakristo. Wanaua polisi kwa sababu diyo sehemu rahisi ya kupata silaha zisizolindwa. Wanahitaji silaha za ugaidi na polisi ndiyo sehemu loose pekee wanayoweza kwenda kupakua silaha zozote wanazozitaka bila upinzani. (According to them).

Wamesema wazi wanapanga kushambulia sehemu za Ibada. Si rahisi watu kuwashawishi kwamba UKAWA wanafadhili magaidi yaue waKristo.

Inawezekana ni serikali inajenga mazingira ya kupitisha mahakama ya kadhi kwa kisingizio kwamba isipopita magaidi watainuka. Ni serkali isiyokuwa na ujasiri wa kusimaima katiba na sheria za nchi.

Inawezekana pia ni namna ya maandalizi ya kuzuia mikusannyiko kwamba UKAWA wasifanye kampeni kwa sababu Kova atakkuwa anapata tarifa za kiinteligensia zikisema wale magaidi wanasema watashambulia mikkutano kama vile tulivyoona kipindi cha nyuma.

Ila lawama zote ziiendee ccm.
 
Hii video binafsi sijaona zaidi ya kusikia kwa Jamaa yangu akiielezea,sibishani na Yericko ila pia tusipuuze kuwa hawa Jamaa sio magaidi,pamoja na mbinu chafu za CCM lkn kwenye hili wanaweza wasihusike na ikawa kweli ni kikundi cha watu wenye hasira na hii serikali, udhalimu na udhalilishaji umekuwa mkubwa sana miaka ya hv karibuni.

Mifano ni mingi ila tutazame tu ule wa wale viongozi wa dini kwa Kile walichofanyiwa kule gerezani, tunadhani ni hasira ya namna gani wameipata Jamaa za wale viongozi au wafuasi wao,tutazame Lile la lipumba juzi na maandamano ya CUF,Binafsi nilitazama Ile video wakirushwa kichura pale station nikaumia roho,tazameni yaliyotokea mtwara kwenye ishu ya gas........

Haya machache yanatosha kabisa kumfanya mtu afure kwa hasira na kufanya maamuzi ya ajabu, CCM na SERIKALI yake wajitazame,ni kama masihara lkn ndio mwendo huo, Mnyonge anaamua kujitoa kwenye unyonge kwa staili anayodhani itamsaidia.

MUNGU ALIBARIKI HILI TAIFA.
 
Asante sana mkuu yeriko sasa nikuweka mitego yote hadharani ili maccm yashindwe pa kushika
 
Hili swala picha ananza kuja, alianza lema (chadema mmbunge) na kumuhusisha changonja leo yerico nyerere (chadema) anaihusisha ccm. Serikali anzeni na hawa watu wawili watakuwa na ushahidi wa kutosha kuhusiana na matukio haya ya kigaidi
 
mwisho na enzi za ccm watafanya kila mbinu ila ukweli utabaki kuwa ukweli tu
 
Yericko, CCM hawakujifunza kwa jini la udini walilitoa kwenye chupa ambalo leo linawasumbua limegoma kurudi kwenye chupa, kwa ujinga ule ule wanajaribu tena kulitoa jini lingine la ugaidi.

Niwaonye tu kuwa haya majini wanayoyatoa huwa hayachagui damu ya kunyonya yatakapoanza kunyonya damu za watoto wao wasije kimbilia kwa jirani kuomba msaada.
 
Back
Top Bottom