tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 25,995
- 25,388
Kitendo cha serikali ya CCM kuyapa kisogo majimbo yanayowakilishwa na UKAWA kinalenga kuwakomoa wananchi zaidi. Ipo mifano hai ya serikali kutoshughulikia kikamilifu miradi ya maendeleo iliyopo kwenye majimbo yanayoongozwa na wabunge wa upinzani ili kuwajengea wananchi dhana hasi kwamba wapinzani hawana lolote. Sina haja ya kuyataja majimbo hayo kwani yanajulikana wazi kwa kila mtanzania mwenye akili zilizotimia.
Kwa akili zao finyu wanadhani kwamba majimbo hayo yakikosa maendeleo wananchi watarejesha mioyo yao kwa CCM kumbe ndio wanazidi kujichimbia kaburi. Kila mtu ni shahidi jinsi wabunge wa UKAWA wanavyohangaika kuwaletea wananchi maendeleo lakini wanakosa ushirikiano kutoka serikali ya CCM. Kudhani kwamba kuwanyima wananchi maendeleo kutawafanya wawachukie UKAWA ni sawa na kuota ndoto ya mchana. Wananchi wa leo ni tofauti sana na wale wa enzi za "Zidumu fikra za Mwenyekiti".
CCM mkae mkijua kuwa kadri mnavyowanyima wananchi maendeleo ndio mnazidi kujichimbia kaburi la uongozi wa nchi.
:israel: