Mama shikamoo,naomba unisaidie kitu kimoja, unaweza kutuwekea majina ya BMk wote idadi na majina yao hapa kabla ya bunge kuanza tena ukiweza utenge wale wa bara na znz? Inaonekana watz hawajui hesabu ndio maana hata akidi inawachanganya, upigwaji wa hiyo kura huko kwa wananchi utasimamiwa na tume ya aina gani? Na hiyo tume itatumia mfumo uleule wa S. 6 kupata matokeo? Yaani kura ya hapana ikishinda itaundwa kamati ya maridhiano na wananchi wa hapana ama kura ya ndio itajaziwa na marehemu wa nchi hii akiwepo baba wa taifa? Je watakaopiga kura ya hapana mtawapa adhabu gani maana AG wa znz mmefukuza kazi, je wananchi wa kura ya hapana mtawafukuza nchini ama adhabu gani?
Kwa umri wako nategemea utaweza kutetea vifungu vyenye utata, eti ni kweli katiba hii imewajali sana wananchi kama wakulima, wafugaji, wasanii nk lakini hawatakuwa na nguvu ya kuwawajibisha viongozi kupata haki hizo? Hii 50/50 kwenye uwakilishi ina tija sana? Na mpaka sasa hivi hatujafikia 50/50 kwa sababu katiba ya zamani iliweka 80% wanaume na wanawake 20%? Je tukisema mliojipa wajibu wa kuandika katiba mlibeba jukumu kwa hila na msiloliweza tutakuwa tunakosea? Mama wewe nakuaminia utaweza kujibu maswali yangu maana hao waliokuwa wajumbe wa BMK hatuwaoni wakitoa ufafanuzi zaidi ya kusema hii ni katiba ya wananchi ipigiwe kura ya ndio.