Ndugu wana-jf,ninajiuliza maana ya kauli hizi za viongozi wa ccm ikiongozwa na Rais,pale aliposema"KATIBA HII NI NZURI WANANCHI MUIPIGIE KURA YA NDIO".hii inatoa tafsiri gani?
Nijuavyo mimi katiba pendekezwa inatakiwa iletwe kwa Wananchi,kila mmoja apewe nakala yake na apate muda wa kisoma ili aweze kutoa maamuzi sahihi. Sasa nawauliza viongozi wa CCM mnaopanda majukwaani na kuipigia debe katiba pendekezwa; mnadhani mnafanya sahihi wakati bado hata wananchi hawajaisoma? Swali linakuja; Kwani mnawasiwasi gani mpaka mnaanza kuipigia debe katiba hiyo ikiwa kama imezingatia maoni yaliyotolewa na wananchi?
Nawaombeni sana,Tanzania ya mwaka 1977 sio Tanzania ya leo!mmezoea kudanganyadanganya umma bila kutumia akili sasa mnaishia kubaya! Tumieni japo akili ili muendelee kijenga heshima ya Taifa letu kwani Tanzania si ya Chama chochote bali ni ya Watanzania.