CCM mnapiga kampeni za nini? Mnashindana na nani?

CCM mnapiga kampeni za nini? Mnashindana na nani?

upande mwingine wa karatasi ya kupigia kura wekeni picha ya tofali watu watalichagua.
 
Hawa ndugu zangu nawashangaa sana, wanajua kabisa kwa majimbo yote 3 yanayorudiwa uchaguzi kungekua na uchaguzi huru na wa haki wasingeambulia jimbo hata moja. Sasa wanazunguka kupiga kampeni ili washindane na nani? Mpinzani amejitoa, sasa sijui kwenye karatasi ya kupigia kura kutakua na sura ngapi. Wangejiamulia tu waweke kura ya ndio na hapana basi!

Nilikua natazama ufunguzi wa kampeni zao kule Longido, haloo watu hakuna.Peoples are so very demoralized! Utawaonea aibu aisee!!
bado nainyooshaa nchi niacheni
 
Ccm imechokwa sana ndg yangu, kinachowabeba ccm kwa sasa ni ubovu wa katiba iliyopo ambayo imeweka mifumo mibovu ya muundo wa jeshi la Polisi, Mahakama, na Tume ya uchaguzi ambavyo vyote hivi vinatii maagizo kwa mwenyekiti wa chama tawala, jambo linaloondoa uwanja sawa wa kufanya siasa kati ya vyama pinzani na chama tawala na matokeo yake jeshi la Polisi+Tume ya uchaguzi na Mahakama kwa upande mwingine+ccm vinaweka nguvu moja kupambana na vyama shindani, iwe kwa amani au kwa kumwaga damu za watu ili mradi ushindi kwa njia yoyote ile upatikane bila kujali matokeo hasi ama chanya kwa jamii husika.
Well said mkuu!
 
Mbaya zaidi Mwenyekiti ana fikra potofu ambazo zinaivuruga nchi lakini yeye anadhani anainyoosha. Sijaribiwi mimi! Usijaribiwe wewe umekuwa Mungu!?

Wanajifariji kuona nchi inarudi kwenye mfumo wa "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti".
 
Baba yenu wa Demokrasia Afrika Mashariki Mhe.Kenyatta hakuacha kupiga kampeni hata siku moja licha ya Odinga kutangaza kususia Uchaguzi.
 
Back
Top Bottom