commonmwananchi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2011
- 3,377
- 1,957
Ndugu wadau na wananchi kwa ujumla,ni wazi kwanba sasa hivi vyama vyote vya upinzani nchini vinanyimwa vibali vya kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima.
Hii ni kwa kisingizio cha kwamba vinahatarisha amani nchini.lakini lkumbukwe kwamba tunatarajia kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji nchi nzima.
Wakati hayo yoye yakiendelea,ccm na serikali yake wako katika mchezo na mbinu chafu kama nitakavyoeleza hapa chini.
Wakati waziri mkuu anatangaza kufanyika uchaguzi huo mnamo mwezi desemba mwaka huu,bado hatujaona jitihada zozote zile za uboreshaji wa daftsri la wapiga kura,ikizimgatiwa kuwa ni muda mrefu tangia ufanyike uboreshaji kwa mara ya mwisho.
Na ieleweke kuwa tuna takribani watu milioni tatu au nne waliotimiza sifa na umri wa kupiga kura tangia uchaguzi mkuu 2010.
Wakati hayo yakitokea na tukiona vyama vingine kupigwa kufuli kufanya siasa nchi nzima.
Ccm na makada wao wakiongozwa na katibu mkuu wao kinana wanazunguka nchi nzima wakifanya kampeni kwa mgongo wa kuimarisha chama,
Lakini tunaonyeshwa katika vyombo vya habari wakihiza wananchi kukichagua chama chao.
JE huu si mchezo mchafu wa kisiasa????
Kwa nini msajili wa vyama halioni wala kulikemea hili?
Je wakilazimisha uchaguzi katika mazingira haya,huku si kuleta machafuko nchini?
Je nani wa kulaumiwa kama hili litatokea?
Tuiombee mema nchi yetu kwa kutendea wenzetu mema na haki sawa kwani nchi na amani ni jukumu letu sote