tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,864
- 3,851
Kuna mambo ambayo Serikali na Bunge ambavyo kwa asilimia kubwa kumejaa wanachama wa CCM, yalikosewa na sio mbaya kukubali, kuomba Radhi na kuanza upya. Mfano:
1. Kupitisha sheria ya tozo kubwa za miamala ya simu kwa kisingizio cha makusanyo Bila kufikiria kwamba wengi wataachana na miamala na vijana wengi waliojiajiri katika sekta hiyo watakosa ajira.
2. Kupuuza suala la Katiba mpya kwa kisingizio cha kukuza uchumi ili hali uchumi una mahusiano ya Moja kwa moja na mamlaka ya kimaamuzi yaliyoko Kwenye katiba. Hivyo kupuuza Katiba mpya ni kupuuza mawazo yanayoukuza huo uchumi.
Katiba mpya haijawahi kuwa gharama, kama tunavyotaka kuaminishwa, ila ukweli ni kuwa gharama za kupuuza mawazo mapya na kung'ang'ania ya zamani zinaligharimu Taifa hili
3. Kumuona kila anayekosoa ni msaliti, mhujumu uchumi, gaidi, ni kukosa uelewa kuwa hajawahi kuzaliwa binadamu mkamilifu na mjuaji wa yote, hivyo kukubali kukosorewa na kuchukua yale yanayofaa kunakukomaza zaidi kisiasa na kiutendaji.
CCM KUBALINI MLIKOSEA, OMBENI RADHI WANANCHI, TUANZE UPYA.