CCM mlikosea, kubalini tuanze Upya

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
2,000
Kuna mambo ambayo Serikali na Bunge ambavyo kwa asilimia kubwa kumejaa wanachama wa CCM, yalikosewa na sio mbaya kukubali, kuomba Radhi na kuanza upya. Mfano:

1. Kupitisha sheria ya tozo kubwa za miamala ya simu kwa kisingizio cha makusanyo Bila kufikiria kwamba wengi wataachana na miamala na vijana wengi waliojiajiri katika sekta hiyo watakosa ajira.

2. Kupuuza suala la Katiba mpya kwa kisingizio cha kukuza uchumi ili hali uchumi una mahusiano ya Moja kwa moja na mamlaka ya kimaamuzi yaliyoko Kwenye katiba. Hivyo kupuuza Katiba mpya ni kupuuza mawazo yanayoukuza huo uchumi.

Katiba mpya haijawahi kuwa gharama, kama tunavyotaka kuaminishwa, ila ukweli ni kuwa gharama za kupuuza mawazo mapya na kung'ang'ania ya zamani zinaligharimu Taifa hili

3. Kumuona kila anayekosoa ni msaliti, mhujumu uchumi, gaidi, ni kukosa uelewa kuwa hajawahi kuzaliwa binadamu mkamilifu na mjuaji wa yote, hivyo kukubali kukosorewa na kuchukua yale yanayofaa kunakukomaza zaidi kisiasa na kiutendaji.

CCM KUBALINI MLIKOSEA, OMBENI RADHI WANANCHI, TUANZE UPYA.
 

Mkomavu

JF-Expert Member
Jan 25, 2016
11,612
2,000
Lengo la kuwa peke yao bungeni ndiyo hili kusiwe na wakuwapa changamoto za kuwapinga mle bungeni na kuhusu kukubali makosa yao na kuomba radhi hilo tusilitarajie
 

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
2,000
Hizi tozo mpka leo huwa najiuliza sijui waliwaza nini
Wao waliamini katika kanuni ya "ceteris peribus" kwamba kila kitu kitabaki kama kilivyo (e everything remain constant) yaani watu hawataachana na miamala baada ya kuweka makato maradufu, kwamba watakusanya fedha nyingi kisha watazipeleka huko vijijini walikokusudia.

LAKINI matokeo yake wananchi wengi wameachana na miamala ya simu, vijana wengi wa vibanda vya miamala wamekosa vipato na ajira, hivyo hayo mapato yaliyokusudiwa yatashuka, na Lengo litaathirika.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,556
2,000
Wao waliamini katika kanuni ya "ceteris peribus" kwamba kila kitu kitabaki kama kilivyo (e everything remain constant) yaani watu hawataachana na miamala baada ya kuweka makato maradufu, kwamba watakusanya fedha nyingi kisha watazipeleka huko vijijini walikokusudia. LAKINI matokeo yake wananchi wengi wameachana na miamala ya simu, vijana wengi wa vibanda vya miamala wamekosa vipato na ajira, hivyo hayo mapato yaliyokusudiwa yatashuka, na Lengo litaathirika.
Ni baada ya kuharibu uchaguzi na kujipa mamlaka kwa nguvu, sasa wanaona wanao uhuru hata wa kutuamulia tupumue mara ngapi kwa dakika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom