Ccm marehemu mtarajiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ccm marehemu mtarajiwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mtweve, Dec 21, 2010.

 1. mtweve

  mtweve Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nikiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu,niliandika makala yenye kichwa hiki,nilipowaonyesha baadhi ya rafiki zangu,walinitisha,wakanidharau,wakaniona mwehu,wakaona mtu ninayetaka kuhatarisha maisha yangu ya shule,nikatishika,nikaachana na huo mpango.sijui kwa nini?,labda kwa vile nilikuwa 'form one' au kwa vile nilikuwa mwoga wa siasa. Leo nimepata ujasiri upya,nguvu mpya za kurudia kusema sisiem mfu anayeishi. Muda si mrefu tutamzika. Msiba ambao watakaohudhuria na kulia ni ndugu wa karibu tu. Cha ajabu,hata wale ambao ndugu wa karibu baadhi watacheka sana. Si kwa sababu nyingine,bali tu kwa sababu tu walibanwa,wakashindwa kuhema,wakakosa uhuru na mfumo wa kizandiki,kinafiki,kifisadi,kibinafsi wa marehemu. Najua wengi mtajiuliza kwanini nasema haya,ujasiri nautoa wapi? Kifo cha ccm si cha ghafla,dalili zote za kuonesha kuwa ugonjwa hauna tiba ziko wazi kabisa. Kila daktari wa siasa atakwambia hana uwezo wa kuitibu,ccm itakufa tu. Zama za ccm kushika hatamu zimekwisha,dalili ya kwanza. Kura zimepungua kama mgonjwa wa vvu anavyopungua kilo,ccm imekonda,imekwisha. CCM inapumulia mashine(tume ya uchaguzi). Kambi ya upinzani imepata nguvu bungeni,vigogo wamedondoshwa majimboni. Wameanza kutafunana wenyewe,wanatangaza nafasi ya uspika kwa wote wanaongeza sifa ya ziada ambayo haikutajwa popote kwenye fomu za maombi,kituko! Watu wanakesi mahakamani,mwenyekiti wake anasema ni watu safi,kichekesho kingine. Makamba,anasema wametumia wanasheria wao wamegundua watashinda. Moja kumbe kesi inajulikana hukumu,pili tangu lini sheria ya kuzuia kesi isijadiliwe nje ya mahakama ilifutwa?wanasema uchumi unakua,utemezi wa bajeti unaongezeka,unakuaje? Nilikuwa kusema,hizi shule za kata ndio kaburi la ccm,huwezi amini! Hakuna mwenye uccm hata mmoja anayetoka shule za hizi. Hakuna kinachofundishwa zaidi ya kuichukia ccm. Ndio wana haki,hawawezi wakaipenda kama wanafundishwa fizikia na mwalimu wa uraria.wanamaliza miaka minne hawajui test tube ina rangi gani. Hawajui kama kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na kiti chake.
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  pole sana mkuu kwa masaibu yaliyowapata pale makao makuu tamisemi.
  hongera sana kwa kukurupuka na simu yako (Posted via Mobile) kuna wenzako ambao walitupa au kuporwa na vijana wa kamanda mwema simu zipatazo 300 pale central police station na hakuna aliye tayari kwenda kukomboa simu yake kwa kuogopa kuwekwa ndani?

  kwa upande wa mada yenyewe huenda kuna ukweli lakini nakushauri wewe pamoja na wenzako mlioamua kukifanya hicho chuo kama mali ya chama hicho muanze kuwa wanachama wafu kama alivyoamua dk lwaitama.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mtweve, acha kulia kuna siku ya sisi akinakabwela kupata ahueni na kufurahi tena atika maisha haya. Usilie Mtweve, ukilia unatuliza Wa-Tanzania wenzio tulio wengi.

  Huo woga uliouzungumzia huko nyuma NDIO MTAJI MKUBWA kwa mdhalimu kuteka akili za watu. Tutakua HURU tena, tuongeze tu bidii ya mapigano kwani wajeraha yatapona na hata tukifa vita mbele kwa mbele ili watakaobaki wapate tulia.
   
 4. minda

  minda JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  hizo kwa sasa ni ahadi za mvuta bange mkuu; labda katiba mpya ipatikane vinginevyo...
   
Loading...