CCM maji ya shingo! Baada ya Mkurugenzi wa Jiji kukataa kubariki wizi wa kura, ahamishwa!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757

Mkurugenzi ahamishwa kwa kukataa ‘bao la mkono’

na Moses Mseti, Mwanza

MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza, Hassan Hida, anadaiwa kuhamishwa katika jiji hilo kwa kile kinachodaiwa ni kukataa kucheza ‘bao la mkono’ katika Jimbo la Nyamagana mjini Mwanza.

Inadaiwa kuwa mkurugenzi huyo ameondolewa katika jiji hilo baada ya kukataa kucheza ‘bao la mkono’, huku akituhumiwa kumuunga mkono Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa anayeungwa mkono na Muungano wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Inaelezwa kuwa Hida kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo na kupewa kazi nyingine serikalini, baadhi ya viongozi wakubwa wa mkoa huo, waliitisha vikao vya kumlazimisha kucheza ‘bao la mkono’ jambo ambalo alipingana nalo na kibarua chake kuota mbawa.

Hata hivyo baada ya mkurugenzi huyo kukataa mchezo huo hatari, viongozi hao wa juu wa juu walianza kuwasiliana na viongozi wa kitaifa wakiomba kuondolewa kwake jambo ambalo halikuchukua muda mrefu na kuhamishwa.

Mtoa taarifa hizi amesema mkurugenzi huyo aliondolewa kutokana na kuwagomea viongozi hao wanaodaiwa kuunda mbinu chafu za kulazimisha ushindi katika jimbo la Nyamagana ambalo historia ya wabunge waliowahi kuongoza wamekaa kwa awamu moja.

Mtoa taarifa aliendelea kudai Chama cha Mapinduzi kimejipanga kulazimisha ushindi wowote ule hata kama ni wa kumwaga damu lakini washinde jimbo hilo kitendo ambacho kitasababisha uvunjifu wa Amani.
 
CCM wezi na sikatai hilo hata chembe ....ila bora CCM ya Magufuli kuliko Chadema ya Lowasa ....nilimkataa Lowasa akiwa CCM ninamkataa hata akiwa nje ya CCM ....Chagua J.P Magufuli na wabunge wa upinzani ....Mtanzania usifanye kosa ....
 
MTAZAMO wewe ndio msomi wa kweli angalia kiongozi bora
 
CCM wezi na sikatai hilo hata chembe ....ila bora CCM ya Magufuli kuliko Chadema ya Lowasa ....nilimkataa Lowasa akiwa CCM ninamkataa hata akiwa nje ya CCM ....Chagua J.P Magufuli na wabunge wa upinzani ....Mtanzania usifanye kosa ....
Rais Lowasa wabunge wengi CCM, hiyo ndiyo Tanzania ninayoitaka. Kuua nguvu za vyama kwa ghalama yoyote ili vyama vizaliwe upya.
Pia, unapaswa kutambua kuwa Magufuli hana CCM yake. Hiyo ni ya wenye nayo. Magufuli is just a joke na hatuhitaji miaka mingine ya aina hiyo baada ya kumi ya kihistoria.
 
Nitapiga kura jimbo la Nyamagana na nitampigia Wenje.
Hizi habari za kupika matokeo ya jimbo hili zimezagaa sana hapa jijini Mwanza.
Nachoweza kusema tu kwa sasa CCM na maswahiba zao waandae majengo mengi ya kutosha mahabusu kwa sababu nina uhakika 100% kura za wananyamagana hazitachakachuliwa na jiji hili na viongozi wa CCM wakasherehekea ushindi wa kupika alafu wabaki salama.
Never. Mi mwenyewe ntakuwepo mita 200 kuzuia uchakachuaji.

CC jingalao, MTAZAMO, IGP.
 
Last edited by a moderator:

Mkurugenzi ahamishwa kwa kukataa ‘bao la mkono’

na Moses Mseti, Mwanza

MKURUGENZI wa Jiji la Mwanza, Hassan Hida, anadaiwa kuhamishwa katika jiji hilo kwa kile kinachodaiwa ni kukataa kucheza ‘bao la mkono’ katika Jimbo la Nyamagana mjini Mwanza.

Inadaiwa kuwa mkurugenzi huyo ameondolewa katika jiji hilo baada ya kukataa kucheza ‘bao la mkono’, huku akituhumiwa kumuunga mkono Mgombea Urais wa Chadema, Edward Lowassa anayeungwa mkono na Muungano wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Inaelezwa kuwa Hida kabla ya kuondolewa katika nafasi hiyo na kupewa kazi nyingine serikalini, baadhi ya viongozi wakubwa wa mkoa huo, waliitisha vikao vya kumlazimisha kucheza ‘bao la mkono’ jambo ambalo alipingana nalo na kibarua chake kuota mbawa.

Hata hivyo baada ya mkurugenzi huyo kukataa mchezo huo hatari, viongozi hao wa juu wa juu walianza kuwasiliana na viongozi wa kitaifa wakiomba kuondolewa kwake jambo ambalo halikuchukua muda mrefu na kuhamishwa.

Mtoa taarifa hizi amesema mkurugenzi huyo aliondolewa kutokana na kuwagomea viongozi hao wanaodaiwa kuunda mbinu chafu za kulazimisha ushindi katika jimbo la Nyamagana ambalo historia ya wabunge waliowahi kuongoza wamekaa kwa awamu moja.

Mtoa taarifa aliendelea kudai Chama cha Mapinduzi kimejipanga kulazimisha ushindi wowote ule hata kama ni wa kumwaga damu lakini washinde jimbo hilo kitendo ambacho kitasababisha uvunjifu wa Amani.

Kama Magu anataka kuthibitisha uadilifu wake na wananchi tumwamini basi kesho ahakikishe huyo mkurugenzi anarudishwa kwenye nafasi yake na kituo kilekile cha kazi.
 
wewe umechanganikiwa mita 200 unalinda kwanini msiweke mawakala mnao waamo
ini. Yani hapo ni kama kumuweka mlinzi amlinde me wako ndanni alafu wewe unatoka mita miambili kumlinda mke wako. Hujui kwamba hapo hujalinda kitu Kama kweli ni una elimu hata ya kuzaliwa
 
wewe umechanganikiwa mita 200 unalinda kwanini msiweke mawakala mnao waamini. Yani hapo ni kama kumuweka mlinzi amlinde mke wako ndanni alafu wewe unatoka mita miambili kumlinda mke wako. Hujui kwamba hapo hujalinda kitu Kama kweli una elimu hata ya kuzaliwa?.
 
CCM wezi na sikatai hilo hata chembe ....ila bora CCM ya Magufuli kuliko Chadema ya Lowasa ....nilimkataa Lowasa akiwa CCM ninamkataa hata akiwa nje ya CCM ....Chagua J.P Magufuli na wabunge wa upinzani ....Mtanzania usifanye kosa ....
Utalijutia kosa unalotaka kufanya wewe na vizazi vyako
 
Wakuu sio Mkurugenzi tu aliehamishwa kuna watumishi wengi tu wanehamishwa hapo hasa wale waliokua wanaonekana hawaishabikii CCM.
Ila chanzo cha yote hayo ni Mkuu wa Mkoa huyu jamaa anachokitafuta atakipata na nishacoment humu kabla hajaanza ujuha wake amuulize Kabwe na RC aliekuepo 2010 ndipo ataelewa watu wa Nyamagana sio kama anavyowafikiria.
 
...ccm kushinda mwanza ni ndoto za mchana..........sasa kwa mfano unamtoa wenje au kiwia ili umweke nani..? hawa wabunge wa ccm wanaenda bungeni kuitikia ndiooooooooo.......
 
Back
Top Bottom