CCM maji shingoni Igunga

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,211
1,744
Tangu kampeni zianze hapa Igunga chadema tumekuwa tukifanya mikutano mitatu kwa siku,huku CCM ikishindwa kufanya hata mkutano mmoj,zaidi ya ule wa ufunguzi uliofanyika Igunga mjini, tena baada ya kuleta watu kwa malori.

Katika hali ya kukata tamaa, CCM sasa imekubaliana kutumia dola kama njia ya mwisho, kujipatia ushindi.. Kimsingi wananchi wengi Igunga wanataka mabadiliko, na wapo tayari kwa mabadiliko.

Leo Chadema tunafanya mkutano wa 21.. picha baadae
 
Songa mbele songa mbele hakuna kulala: na pia kuwa tayari kwa Ulinzi wa kura jamani
 
asante kwa habari njema.....People's powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Chadema kwa mikakati ni balaa..ndiyo maana CCM wamepigwa na butwaa. Wenzako kama wamefanya mikutano 21 na wewe mmoja wa kuchakachua unategemea nini??. CDM ni mwisho wa matatizo...a very strategic party ever. Ikiwzekana msitumie helkopta
 
Labda bado wanaomboleza,si walisimamisha kampeni lakini?
nyie vipi hamku-stop kidogo?

All the best,play safe.
Vaa mawani makubwa maana naskia kuna acid lita 100 zimeletwa huko.
 
Hongereni sana, hata Miss Tanzania nayo iliendelea, CCM wajinga walisimamisha kampeni wakati wa maombolezo.
 
Hivi kapteni Komba hajaja huko la lile lori lake na band yake ya kwaya na taarabu?
Kweli mkuu umenikumbusha kale kawimbo ka magamba; ka kukejeli walalahoi; watanzania tieni, tieni tieni kwa moyo mmoja nambari wani ni --- watanzania twapendeza" siku hizi magamba yamenyujwa kishenzi! ni mafisadi na mijizi haithubutu kutuimbisha tena!!!
 
Nice info Nanyaro!
Msipumbazike na kushindwa kwao kufanya mikurtano!...Nyie ongezeni mbinu kila kukicha, ccm hawana muamana hao!
Kama wana Igunga wanataka mabadiliko then kazi imebaki kwenu kumsukuma mlevi!..
Kuna mtu alisema kama cdm ITAshinda Igunga atavaa magwanda!...naona sasa hivi anaukimbia mtandao!
 
wako busy kuunda tume kumshughulikia Nape, hata hivyo si wameshapanga matokeo
au IGUNGA hakuna rafu
 
Pigeni kazi kaka, chadema ndio tumaini pekee la watz! Wanajifanya wanaombeleze kwa mambo ya kizembe yanayofanywa na serikali yao. Wengine tunakuja kusimamia kura muda ukifika kama 2livyofanya ubungo na kawe.
 
Jimbo laini sana hili,na wanaIgunga wapo tayari kwa mabadiliko,kimsingi kwenye uchaguzi wa mwaka jana Chadema tulipata madiwani 2,wa kuchaguliwa na 1 wa viti maalum.Kila unayekutana nae anaonyesha ishara ya chadema hata watoto,ambayo ni ishara kuwa hata wazazi ndicho wafanyacho.,,ntaendelea kuwajuza
 
Mkuu Nanyoro, msibweteke na hii hali nyie ongezeni strategy ya kuchukua jimbo maana hapo ndo kwenye mshipa wa mwisho wa CCM mkiukata huo basi tena ndo CCM kwa heri!
 
Magawnda yanajifariji na kujilizawa!
Vipi hao vijana waliomwagwa na zile Fuso za CDM kutoka Moshi na Arusha ni wapiga kura wa jimbo hilo? Huko ni kujidanganya na sijui ni nani analipa gharama za chakula na malazi kwa vijana hawa zaidi ya 400 walioletwa na CDM ili kuongeza wingi wa watu katika mikutano yao
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom