CCM mabingwa wa viini macho

CCM mabingwa wa viini macho

mzalendokweli

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2012
Posts
579
Reaction score
138
Katika taarifa ya habar ya star tv inayoendelea sasa Nape anasema wamejipanga kupambana na rushwa ndani ya chama. Katika alizodai aina mbili za kupambana wao wameamua kupambana kwa kuzuia na si kuadhibu. Kah,mi najua moja ya njia muhimu kabisa za kuzuia uhalifu/makosa ni kuadhibu wakosaji ili kudiscourage wengine kutotenda. Ukisema unazuia bila kuadhibu wakosaji watu watatafuta mbinu mpya kila siku. Pia anadai watazuia kwa kubadili baadhi ya kanuni anazodai zinapelekea rushwa.

My take;

CCM inaogopa kuzungumzia kuadhibu wala rushwa kwakua wakigusa nyanja hiyo watavuruga chama mana kila mmoja kala rushwa kufika alipo. Pili, ku-amend kanuni ni bomu hilo linaandaliwa kuja kumlipua mtu. Hapa. Wanajipanga kutosa watu kwa kutumia kanuni 2015. Mazingaombwe ni mbinu ya mwisho chama kinatumia kinapoelekea kufa.
 
CCM SIIPENDI NA WAPINZANI WAO SIWAAMINI. Nitabaki na Tanzania yangu!
 
CCM ndo vinara wa rushwa hapa nchini sa sijui watafanikiwa vp wakati wao wanaogopana.
 
ccm ya kina nape haijawahi kuweza jambo lolote
 
Nape is weak like a prostute who once sees money she gets excited
 
Popote atakapoonekana mkamateni,mfungeni kamba mpelekeni hospital,hajamaliza dozi
 
Utabaki na Tanzania ipi? ya kwenye ramani?
Hivi yule aliyedanganya kamtibu Tundu Lisu Ugonjwa wa ajabu Dr.wa Vitumbua wa pale Nzega hajamuona Nape kwamba anaumwa ugonjwa wa ajabu sana...Aende akatuthibitishie kwamba yeye ni mganga maana sio Dr.yule kilaza tu
 
Katika taarifa ya habar ya star tv inayoendelea sasa Nape anasema wamejipanga kupambana na rushwa ndani ya chama. Katika alizodai aina mbili za kupambana wao wameamua kupambana kwa kuzuia na si kuadhibu. Kah,mi najua moja ya njia muhimu kabisa za kuzuia uhalifu/makosa ni kuadhibu wakosaji ili kudiscourage wengine kutotenda. Ukisema unazuia bila kuadhibu wakosaji watu watatafuta mbinu mpya kila siku. Pia anadai watazuia kwa kubadili baadhi ya kanuni anazodai zinapelekea rushwa.

My take;

CCM inaogopa kuzungumzia kuadhibu wala rushwa kwakua wakigusa nyanja hiyo watavuruga chama mana kila mmoja kala rushwa kufika alipo. Pili, ku-amend kanuni ni bomu hilo linaandaliwa kuja kumlipua mtu. Hapa. Wanajipanga kutosa watu kwa kutumia kanuni 2015. Mazingaombwe ni mbinu ya mwisho chama kinatumia kinapoelekea kufa.
ccm hila zao ni pembe la ngombe hazifichiki tena, tutakapopata serikali makini lazima wawajibike hata kama watakaokuwa hai ni wajukuu zao
 
Kama unaielewa CCM vizuri utaelewa kwanini Nape amesema hivyo. Ni bora kusema ukweli kuliko kudanganya. Ukiadhibu wala rushwa ya uchaguzi CCM utakuwa unajiadhibu wewe mwenyewe. Kwa mfano ukimwambia mwalimu awachape wanafunzi wa Mkoa mzima, hapo utakuwa unamuadhibu mwalimu sio wanafunzi maana mkono wake baada ya kutoa hiyo adhabu utakuwa hautamaniki...
 
CHAMA cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ni kansa inayoendeleza matatizo kwa wananchi.
Hayo yalisemwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Dakawa juzi, ukiwa na lengo la kuwapongeza wabunge wa upinznai kwa hoja nzito walizoziwasilisha bungeni kisha zikapuuzwa.
Viongozi hao waliongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu, Susan Kiwanga, akiambatana na wabunge wengine kadhaa wa chama hicho.
Wabunge hao ni Rose Kamil (Viti Maalumu), Sylvester Kasulumbai (Maswa Mashariki),Tundu Lisu (Singida Mashariki), Deo Munishi (Katibu BAVICHA Taifa) na aliyekuwa mgombea ubunge 2010, Matokeo Manyeta.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo wabunge hao waliwaambia wananchi kuwa hoja madhubuti kutoka vyama vya upinzani hazitapita kutokana na CCM kuhofia kuondolewa 2015.
“Umaskini, ufukara, ugumu wa maisha na ujinga unaoendelea kuwatesa wananchi ndiyo sababu ya hofu ya kuondolewa madarakani viongozi na chama kibovu cha CCM.
“Sasa wamebaki kuzuia kila kinachotokea mbele yao hata kama kina maslahi mazuri kwao wenyewe; mmeshuhudia kilichofanyika bungeni,” alisema Kasulumbai.
Wakifafanua juu msingi wa hoja ya elimu kama ilivyokuwa imewasilishwa na mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia (NCCR-Mageuzi, na hoja ya maji ya John Mnyika (CHADEMA-Ubungo), Lisu na Munishi kwa nyakati tofauti waliwaeleza wananchi hao kuwa CCM ni ukuta uliooza unaosubiri kimbunga cha kuuangusha.
“Kama wanasiasa wakosoaji hatutasita kuendelea kuwakosoa na hata kama wanajivunia kutufukuza bungeni, tunajua hukumu yao ni kwenu wananchi.
“Leo wananchi mnashindwa hata kula milo mitatu, watoto wanaendelea kupata elimu duni isiyo na mitaala ili wawatawale watakavyo, afya ndiyo usiseme na hii yote inatokana na ubovu wa serikali iliyo madartakani,” alisema Lisu.
Naye Rose Kamili akifafanua juu ya changamoto iliyo kwenye sekta ya kilimo na mifugo huku akionyesha kusikitishwa na serikali kuwamilikisha watu maeneo ambayo hawawezi kuyaendeleza aliwaahidi kurudi kutafiti na kuja na mwarobani wa changamoto hizo.



[TD="bgcolor: #ffffff"]
na Joseph Malembeka, Mvomero


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"]
amka2.gif
[/TD]
 
hizi ahadi na matamko yasiyotekelezeka yamekuwa kama wimbo anaoimbiwa mtoto ili apate usingizi. Its high time that we should do away with these CCM croocks.
 

Attachments

  • kp14022013.jpg
    kp14022013.jpg
    28.2 KB · Views: 40
Back
Top Bottom