CCM Lazima Kufa Kiume

CCM Lazima Kufa Kiume

jnuswe

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,270
Reaction score
549
Nikifuatilia yanayoendelea kwa sasa kutoka chama tawala ambacho ni miongoni mwa vyama vikongwe barani Afrika, hakika CCM mmekubali kufa kiume

Baada ya kubanwa sana na chama makini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mmeamua kutokukubaliana na hali halisi ya mabadiliko ya dhati badala yake mmeanza propaganda nyingi zisizokuwa na maana. Propaganda hizo msipoziratibu vizuri mkaendelea na ujinga wa kupiga mayowe na kuandika kwenye vyombo vya habari mambo ya uzushi kifo chenu hakipo mbali

Angalizo
Mnachopaswa kufanya sasa baada ya kuona wananchi wanayakubali mabadiliko kwa kasi ni nyinyi kutulia na kutafakari ni wapi mlipoanzia kujikwaa na kisha mkatumbukia kwenye anguko kubwa hili

Natabiri mpaka ifike 2014 mtakuwa mmepotea kabisa kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania
 
Mtaji wa siasa ni kuwekeza kwenye miyo na imani ya watu ili waendelee kukuamini na kukupenda. Sawa na ilivyo kwenye biashara kuwa ni lazima uendelee kuongeza mtaji ili biashara isife. CCM hawakufanya hivyo bali ilifikiri wananchi wataendelea kuwa ndiyo mzee na wakajitenga ktk kikundi cha watu wachache na kujipambanua kuwa wao pekee ndio wenye haki ya kufaidi raslimali za nchi hii, na watoto wao pamoja na wapambe wao.
Sasa wanalia na kupiga mayowe bure na kutafuta mchawi. Mchawi mkubwa ni kushindwa kupambana na ufisadi ktk nchi hii ambao ndio umesababisha umaskini na ufukara kwa wananchi, Kwani ufisadi unachota zaidi ya 80% ya mapato yote ya nchi na ni 20% tu inayobaki kwa ajili ya maendeleo. Je kwa ufisadi huu nchi itasonga mbele?. Changamoto!.
 
Nikifuatilia yanayoendelea kwa sasa kutoka chama tawala ambacho ni miongoni mwa vyama vikongwe barani Afrika, hakika CCM mmekubali kufa kiume

Baada ya kubanwa sana na chama makini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mmeamua kutokukubaliana na hali halisi ya mabadiliko ya dhati badala yake mmeanza propaganda nyingi zisizokuwa na maana. Propaganda hizo msipoziratibu vizuri mkaendelea na ujinga wa kupiga mayowe na kuandika kwenye vyombo vya habari mambo ya uzushi kifo chenu hakipo mbali

Angalizo
Mnachopaswa kufanya sasa baada ya kuona wananchi wanayakubali mabadiliko kwa kasi ni nyinyi kutulia na kutafakari ni wapi mlipoanzia kujikwaa na kisha mkatumbukia kwenye anguko kubwa hili

Natabiri mpaka ifike 2014 mtakuwa mmepotea kabisa kwenye ulimwengu wa siasa za Tanzania
Bora umekuja! eti mna mpango wa kuingia msituni kama CCM wakishinda uchaguzi 2015 au wanawasingizia tu?
 
Kufa Kiume wanapigania nini? Hakuna kitu kinachofanyika Tanzania kwa maana kutoka serikalini Barabara zinajengwa na American Money ya Bush, Hospital Bill Gates Foundation, shule hazina hadhi wala walimu, serikali imejiingiza kwenye biashara za umeme na ndege kwa hasara na serikali imetawala mika 50. Ni wakati wa kujaribu mbinu tofauti hivyo kama wanapigana wanapigania nini hasa! sio maendeleo!!. Watanzania inabidi waachane na siasa na ku focus kwenye maendeleo nchi yetu masikini sana bado.
 
CCM Baada ya Kumleta huyu jangili naona rasilimali zetu za wanyama hususani tembo na Twiga itakuwa ni historia kwa vizazi vijavyo
Jangili.jpg
 
Swala la CCM kufa wala si option tena bali is a must. Juzi kwenye kikao ya CCM kilichomalizika ambacho wamefanya Recycling ya wazee aliopitwa na wakati mzee MANGULA na KINANA nilimsikiliza kwa makini retaired presida Mweshimiwa KARUME kwamba " We shall meet in December" Mzee huyu mstaafu na mkweli alikuwa akiwaeleza wenzake wanaccm kwamba watanzania tunawasubiri CCM 2015 na hapo ndo hasira za watanzania zitajulikana waziwazi kwenye sanduku la kura. Sina uhakika kama mweshimiwa LEMA waliyeporwa ubunge wake na mahakama sanii za Kibongo ametamuka kwamba CHADEMA itaingia Msituni ikishindwa Kihalali. Naamini LEMA kama ameyasema hayo alikuwa anamaanisha kwamba kama CHADEMA 2015 kitaporwa ushindi halali basi pana kila sababu ya kujaribu njia nyingine ya kuikomboa nchi toka mkoloni mweusi CCM na mafisadi wake.
Naamini LEMA anajaribu kukumbushia lile swali liloulizwa na Jenerali Ulimwengu kuhusu matokea ya uchaguzi ya urais ya 2010 alilouliza na kuchafua hali ya hewa kama alivyoliport MWIGAMBA , Jenerali " Ni nani kati yetu washiriki wa kongamano la Kutadhimini Utawala bora anaweza akatuambia Kura za Urais Tanzania bara 2010 zilikuwa ni ngapi na ni nani alipata nini?". Swali hili ni sawa na lile la Kenya aliloulizwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kenya 2008, kwamba hivi mshindi wa urais kati ya Raira na Kibaki ni nani kwa kura ngapi na zipi, jibu yeye akasema hata mimi sijui mshindi kati ya hao wawili,'' kumbuka wakati anajibu maswali hayo akiwa msimamizi mkuu wa uchaguzi kenya tayari kibaki alikuwa anaapiswa na jaji mkuu. Hizi ndo politics za kiafrica na Utawala bora Feki.
Sasa basi mbunge halali wa Arusha mjini LEMA maana yake ilikuwa ni kwamba kama 2015 utafanyika uhuni wa kuchakachua matokeo kama ilivyokuwa 2010 dhidi ya chama chake CHADEMA lolote laweza kutokea na uhakika ni kwamba watanzania wamechoka na ubabaishaji wa CCM so wanataka mabadiriko kwa njia yoyote ile iwapo Demokrasia itashindwa kuchukua mkondo wake.
Iwapo CCM watajidanganya kuwa nchi hii bila wenyewe haisongi mbele na kung'ang'ania madaraka basi wajue Moto utawaka kwani naamini kwa sasa ni kiongozi shupavu tu atakayeongozwa ukombozi wa chi hii ndo anasubiliwa tu.
Kwa kifupi ni swala la muda tu CCM si tu kitakuwa chama cha upinzani tu bali hata kufa KITAKUFA.
 
ukisema ukweli basi unaonekana unachochea gasia ndio tatizo la ccm na viongozi wake vilazi
 
Back
Top Bottom