Nishati ya Upendo wengi wanaipigania kufa kupona

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,884
NISHATI YA UPENDO WENGI WANAIPIGANIA KUFA KUPONA

Anaandika, Robert Heriel

Ili uweze kuishi utahitaji pumzi, Pumzi ni nishati inayotuwezesha kuishi. Pumzi itokapo katika miili yetu maisha yetu yanakoma.
Hata hivyo pumzi pekee yake haitufanyi tuwe hai. Zipo Nishati nyingine nyingi ambazo zinaisaidia pumzi kutufanya tuwe hai.
Lakini kabla hatujafika mbali huenda kuna msomaji wangu hafahamu maana ya nishati licha ya kuwa Neno hili analisikia mara Kwa mara. Taikon ni kukupa maarifa.

MAANA YA NISHATI
Nishati ni uwezo na nguvu ya kufanya mambo ya kimwili na kihisia katika maisha. Yaani uwezo na nguvu ya kufanya kazi kimwili na kihisia katika maisha.
Jambo lolote ambalo linakupa uwezo au nguvu ya kufanya mambo kimwili au kihisia huitwa Nishati.
Visawe vya istilahi nishati ni Nguvu, uwezo, kani, n.k.

Zipo Aina nyingi za nishati Kama vile
i. Nishati ya Umeme,
ii. nishati ya mwanga,
iii. nishati ya Nyuklia,
iv. Nishati ya Sauti
V. Nishati ya mwendo
V. Nishati ya mionzi

Nyingi Kati ya hizo tumefundishwa darasani, lakini Leo hii nitaitambulishwa kwenu NISHATI YA UPENDO ambayo ni uwezo au nguvu ya ndani ya mtu au kiumbe inayomfanya aendeshe maisha yake.

Kila nishati inachanzo chake, vyanzo vya nishati vinafahamika, mfano Jua, maji, upepo, nakaa ya mawe, Mafuta, geothermal n.k
Kwa upande wa nishati ya Upendo chanzo chake kikuu ni MOYO.
Moyo ndio chanzo kikuu cha Upendo.

Maisha bila nishati ya Upendo hayawezekaniki, hasa maisha ya mwanadamu mwenye utashi. Upendo ndio Jambo la pili baada ya nishati ya Uhai. Binadamu anaishi ili apendwe, na anapendwa ili aishi.
Sio ajabu watu kila kukicha wanahangaika Kwa jasho na damu ili kupata Upendo, aidha ni Upendo kutoka Kwa Wazazi, wenza wao au marafiki zao.

Hakuna kitu kizuri kwenye maisha Kama mtu akihisi anapendwa. Upendo humfanya mtu awe na furaha, ajihisi kujiamini, na aone maana halisi ya maisha.
Madhara mengi katika jamii hutokea zaidi na kusababishwa na watu waliopunjwa Upendo. Kisaikolojia naam ndio kiakili na kitabia mtu aliyepunjwa upendo huweza kufanya mambo mabaya ya kutisha.

Bado hujamuelewa Taikon? Subiri.

Nilisema kuwa Chanzo kikuu cha Nishati ya Upendo ni MOYO lakini lazima ieleweke kuwa katika maumbile ya kibinadamu kuna mioyo ya Aina mbili, nayo ni;
a) Moyo wa Mwanaume
b) Moyo wa Mwanamke
Kama ilivyo katika mbegu za uzazi, naam kuna mbegu ya mwanaume na mbegu ya mwanamke.

a) Moyo wa Mwanaume.
Hilo ndicho chanzo kikuu Ch Upendo katika maisha ya hapa Duniani. Moyo wa mwanaume ndio umezalisha moyo wa mwanamke. Hii ni kusema moyo wa mwanamke ulitoka katika moyo wa Mwanaume.
Katika mfumo wa kijenetiki Mwanaume ndani yake yupo Mwanamke, lakini ndani ya mwanamke hakuna mwanaume. Hivyo moja Kwa moja mwanamke anakuwa Pungufu.
Hata katika Mbegu za kiume kuna Gamete X na Y wakati mbegu za kike kuna Gamete X(ambayo ni mbegu ya kike tuu) hivyo mwanamke anakosa gamete Y(mbegu ya kiume).

Kwa maana hiyo Katika nishati ya Upendo Kama kuna mtu anahitaji upendo kamilifu ataupata Kwa Mwanaume na sio mwanamke, kwani Kwa mwanamke upo nusunusu.

b) Moyo wa Mwanamke.
Huu ni chanzo cha nishati ya Upendo ambao upo Kwa ajili ya mwanamke mwenyewe na watoto atakaowazaa.
Upendo huu haupo Kwa ajili ya jamii nzima Kwa sababu ni mdogo hautoshi.
Sio ajabu watu wengi huwaona wanawake Kama watu Wabinafsi au wenye kujipenda wenyewe. Sio kosa Lao wao natural wapo hivyo.
Hata katika mbegu zao Wana gamete X pekee. Yaani wapo kwaajili Yao wenyewe, wapo kujizaa wenyewe tuu.
Sijui Kama Taikon Naeleweka.

Sio kosa mwanamke kujipenda au kuwa mbinafsi Kwa ajili yake mwenyewe na watoto. Hiyo ni hulka Yao na maumbile Yao yapo hivyo. Ila ni kosa mwanaume kuwa mbinafsi na kutokuwa na upendo WA kutosha kwaajili ya watu wengine.

Sio ajabu mwanamke akawa anapenda tuu yeye ndiye afanyiwe Kwa asilimia kubwa huku yeye Mchango wake ukiwa ni mdogo au ukiwa haupo kabisa.
Mfano Mwanamke atataka wewe ndio umjali, umbembeleze, umdekeze, umhudumie, umpe attention yako lakini yeye hayo anaweza asiyafanye kwako.

Upendo wa mwanamke upo nusunusu hivyo usiutegemee Sana. Hana stock ya kutosha ya nishati ya Upendo ya kuweza kustahimili kukupenda wewe na watoto wako Kwa pamoja na Kwa kipindi kirefu.
Lakini mwanaume kutokana Yuko Full anauwezo wa Kupenda Mke na watoto, na mpira, na pombe na washikaji zake huko mitaani. Kwa miaka yote yaani full time.

Baba kama chanzo kikuu cha Upendo ndani ya familia anapopuyanga Kwa kushindwa kutoa Upendo Kwa familia yake. Hii inadhuru mapenzi ya Mkewe.
Taikon huwagana nasema, Baba au mwanaume ni Kama Jua, na Mama au mwanamke ni Kama mwezi.
Mwezi unaakisi mwanga kutoka kwenye Jua.
Vivyohivyo Mkeo anaakisi upendo wako wewe Kama Mume wake. Kama ukitoa upendo hafifu basi Mkeo ataakisi upendo hafifu na utamuona anaanza kukusumbua.

Hakunaga ulinganifu Kati ya mwanaume na Mwanamke. Mwanaume Kwa vile upo Full yaani umekamilika basi lazima utoe vitu vilivyokamilika. Yaani mwanaume lazima utoe kingi au mengi zaidi kuliko mwanamke. Hii ni kutokana na kuwa wewe ndiye chanzo cha upendo.

Kisaikolojia, wanawake wameumbwa kuamini kuwa Mwanaume unaweza, unacho, na unauwezo wa kufanya lolote ili kutatua tatizo Fulani.
Mwanamke hata umwambie huna pesa kamwe hataamini kuwa hauna pesa Ila atakachoweka akilini ni kuwa haumpendi.
Mwanamke mara zote anaamini unapesa na unauwezo wa kumsaidia hivyo kusema hunapesa au huwezi msaidia tafsiri yake ni kuwa umemfanyia makusudi.

Mwanamke hata umuonyeshe Kadi ya Bank na salio la Akaunti yako akaona unasifuri kwenye Akaunti yako. Bado ataamini kuwa unapesa sehemu Fulani Ila unamficha.
Kiufupi ni kuwa Mwanamke anajua mwanaume yupo Full yaani amekamilika.

Na Bora abaki katika State hiyohiyo ya kudhani kuwa umekamilika kuliko siku ahitimishe kuwa haujakamilika yaani haupo Full. Siku hiyo ndio siku atakayokudharau, atakayoanza matatizo.
Ndio maana inashauriwa sio mara zote unapaswa kusema Ukweli hasa kama ukweli huo hauna matokeo mazuri au hauna maana yoyote Kwa Mwanamke.

"Taikon unapenda Sana Makala ndefu"
Ndio ninapenda,

Upendo bila akili hauwezi kuwa na matokeo mazuri. Akili na maarifa vipo Kwa ajili ya kufanya maisha yawe mazuri. Lakini Upendo upo Kwa ajili ya kufanya maisha hayo mazuri yawe na FURAHA.

"Taikon unazungumzia nini tena?"
Kuna watu wanafikiri upendo pekee unatosha. Hapana Upendo pekee hautoshi.
Mara nyingi Taikon nawashauri wanawake hasa wanaonipigia simu kuwa wamepata Vijana Fulani wanaowapenda wanaomba ushauri.
Moja ya Ushauri ninaowapaga ni pamoja na Kuwa kijana ni kweli anakupenda lakini anaakili na maarifa?
Au kijana ni kweli anapesa na Utajiri lakini anaakili na maarifa?

Upendo bila akili huweza kugeuka Mateso makubwa sio tuu kwako mwanamke Bali mpaka Kwa watoto wako.
Upendo ndio msingi Mkuu wa mahusiano lakini kinachoendesha mahusiano na Akili na maarifa. Pesa na Utajiri ni vichocheo tuu katika mahusiano.

Mtu anaweza akawa anakupenda Kwa dhati yote lakini Kwa vile Hana akili na maarifa akawa anakutesa na kukunyanyasa Kwa hayohayo mapenzi Kwa kile kiitwacho Wivu.

Baba anayowajibu wa kuhakikisha anatoa nishati ya Upendo Kwa Mkewe/Mama ili matokeo ya Upendo huo yajionyeshe Kwa watoto watakaowazaa.

Nafahamu nyakati zinabadilika, wakati WA ndoa changa ni tofauti n wakati ndoa inamiaka kumi mpaka ishirini. Upendo pekee hautoshi kukabiliana na Mabadiliko ya nyakati, isipokuwa lazima kuwe na nyongeza ya Akili , maarifa na IMANI.

Baada ya nishati ya Uhai, upendo, akili na maarifa kinachofuata ni IMANI.

Asije akakudanganya Mtu yeyote, hakuna mahusiano yenye hatma nzuri mbeleni ikiwa Wenza watakuwa na tofauti za kiimani. Hakunaga kitu Kama hicho.

Mapenzi yasije yakakudanganya kuwa Kwa vile mnapendana basi mnaweza kuishi hata kama mnatofautiana kiimani. Huo ni Uongo mkubwa unaowazwa na watu wajinga wanaokaribia kuwa wapumbavu.

Akili na maarifa ndio inaendesha mahusiano hilo nilishasema, lakini akili huwa na ukomo. Katika maisha mnaweza kutana na changamoto matata ambayo akili zenu zinaweza kushindwa kuitatua. Hapo ndipo Imani inapoanzia kufanya kazi. Kama mnatofauti za Imani inaweza leta migogoro mipya ambayo haikuwepo na kuhatarisha mahusiano yenu.

Madhara ya watoto kukosa nishati ya Upendo kutoka Kwa Baba na Mama ni makubwa ndani ya jamii na Dunia Kwa ujumla. Hayo utayashuhudia kwenye jamii. Ubinafsi, dhulma, mauaji, ujambazi na Aina zote za ukatili ni matokeo ya kukosa nishati ya kutosha ya Upendo.

Nashauri; Wazazi hasa Sisi kina Baba, tuhakikishe tunawafundisha na kuwapa vijana wetu Nishati ya Upendo ili Kupunguza madhara katika jamii na taifa Kwa ujumla

Somo Hili ni refu mno. Nilitamani kuendelea Ila kuna Wale wenzangu na miye wataanza kupiga mayowe. Anyway tuishie hapa

Niwatakie SABATO NJEMA.
Ulikuwa nami Taikon master kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kisaikolojia, wanawake wameumbwa kuamini kuwa Mwanaume unaweza, unacho, na unauwezo wa kufanya lolote ili kutatua tatizo Fulani.
Mwanamke hata umwambie huna pesa kamwe hataamini kuwa hauna pesa Ila atakachoweka akilini ni kuwa haumpendi.
Mwanamke mara zote anaamini unapesa na unauwezo wa kumsaidia hivyo kusema hunapesa au huwezi msaidia tafsiri yake ni kuwa umemfanyia makusudi.

Mwanamke hata umuonyeshe Kadi ya Bank na salio la Akaunti yako akaona unasifuri kwenye Akaunti yako. Bado ataamini kuwa unapesa sehemu Fulani Ila unamficha.
Kiufupi ni kuwa Mwanamke anajua mwanaume yupo Full yaani amekamilika.
Hakika umenena vyema sana...
 
Katika maisha yangu nimewahi kutoa offer za pombe kwa mamia ya watu. Pia wanaume wengi wamekwisha ninunulia bia...ila ni wanawake wawili tu nakumbuka ndio waliowahi kuninunulia bia zisizozidi tano.
 
Back
Top Bottom